EXIM Credit Cards-MasterCard | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

EXIM Credit Cards-MasterCard

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Dark City, Oct 20, 2009.

 1. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Nimejaribu kufuatilia suala la credit cards za Exim na kupewa utaratibu wao kwa muhtasari. Ingawa wamejitahidi sana kutoa hiyo huduma, bado nadhani kuna vitu ambavyo wanatakiwa kutuelimisha. Kwa sasa ningeomba wenye uzoefu watusaidie ili tupanue ufahamu wetu na tuweze kuchangamkia hii huduma.

  1. Wanatoa kadi za aina mbili (Silver na Gold)
  2. Ili uweze kupata Silver, lazima uweke fixed deposit ya Tshs 1m (or $1000) na unaweza kutumia kwenye credit card yako hadi 80% ya hizo pesa ulizoweka kwenye fixed deposit. Kwa upande wa Gold, fixed deposit ni 5m ($5000). Pia unaweza kutumia hadi 80%.
  3. Kuna gharama ya kujiunga (kama sijakosea ni 25000) na kuna gharama nyingine nimesahau. Pia unatakiwa kulipa 50,000/- kwa mwaka.
  4. Ukitumia kununa vitu hakuna gharama ila ukichukua pesa kwenye ATM au cash machine yoyote unalipishwa 3%.
  5. Utaletewa muhtasari wa matumizi kwa mwezi na ukichelewa kulipa utalipishwa penalty ya Tsh 2500/- kila siku.
  Inawezekana kuna taarifa nyingine lakini hizo ndizo nimekumbuka. Naomba kupata michango yenu wadau.
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  This is a direction this country must use!

  NMB, CRDB, NBC mko wapi??
   
 3. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,123
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Hii naona ni Debit Card inayojifanya ni Credit Card. Kwa sababu unaweza kutumia hela zilizopo kwenye account tu.
  Tena labda ni mbaya kuliko Debit Card kwa sababu inabidi uwe na hiyo minimum ya 1m au 5m kwenye account.
   
 4. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #4
  Oct 20, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Service hii ya Exim ni ya siku nyingi...

  Wala si Credit Card, ni Debit Card.

  Niliwahi kutumia Gold na niliumia vibaya (more than a year ago), card zinakuwa rejected sehemu nyingi!

  CRDB wao nasikia inafanya kazi vizuri, tatizo usi-deal na branches za nje ya Jiji la Dar es Salaam kama una-apply, nenda Premier Branch (Benjamin Towers) na wambie unachotaka kufanya, wao watakupa maelekezo ambayo naamini yatakusaidia kwa urahisi. Tatizo matawi ya mabenki yetu ni kuwa na customer service isiyojali wateja, wengine hata services hizi hawajui kama zipo na hata kuzielezea hawawezi.

  You can read this topic:

  Using PayPal and MoneyBookers with CRDB VISA Card
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ahsante sana mkuu kwa hii taarifa.

  Hilo likuwa swali langu la kwanza kwao na wakadai wanafanya hivyo kwa sababu sisi (Watanzania) hatuna utamaduni wa kulipa mikopo na pia hatuna anwani! Kwa hiyo wanaweka hiyo kitu kama dhamana.

  Nilipotaka kujua kwa nini wasitafute dhamana ya aina nyingine eg. mwajiri au mali zisizohamishika wakaruka na kusema kuwa hiyo haina uhakika kama kukalia pesa zako kwenye fixed deposit. Hilo limenitatiza sana kwani kama ninazo 5m kwa nini nitafute credit zao zenye gharama zaidi?
   
 6. C

  Chief JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2009
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Wizi mtupu. Unakopa hela yako tu. CRDB Visa card is the best.
   
 7. Mwamanda

  Mwamanda Senior Member

  #7
  Nov 4, 2009
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 132
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  wakuu ninaomba ushauri jinsi ya kupata crdb visa card au kama kuna benki nyingine yenye utaratibu kama huo
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kiongozi ni kweli.

  Ni majuzi tu hapa nimeenda tawi la CRDB la Mlimani City kuulizia kuhusu upatikanaji wa credit card mhusika anayehusika na kadi akanambia eti huduma ya credit card haipo CRDB! Nikapoteza appetite ya kuwa mteja wao. Naamini bongo kila kona wamejaa watu incompetent.
   
 9. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Mimi naunga mkono kauli ya Invisible kuwa hio ni Credit Card. Ukiwa na hio kadi unapewa kiasi fulani cha fwedha ili utumie ikiwa ni mkopo wa dharura, sasa inategemea na kipato chako cha kila mwezi katika current account yako.

  Pia katika nchi zilizoendelea watu wa benki hupenda kushauri wateja wenye kutumia akaunti mara kwa mara kwa kuwa na fwedha za kutosha kuchukua credit cards ili ziwasadie kwa matumizi mbalimbali ya dharura ambayo mengi yanakuwa yanahitaji kulipa kwa credit card.

  Kwa hio unapopewa kadi hizo kunakuwa na limit na ukitumia ama iwe ndani ya nchi au nje basi kunakuwa na charge na ndio naona Exim wanatandika 3%.

  Ila mtu huna haja ya kutaka credit cards ikiwa una uwezo wa kutumia debit card na pia kuwa na overdraft ya nguvu ambayo pia ni mtindo kama wa credit cards.
   
 10. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,123
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Ya CRDB sio credid card, ni Visa Debit card.
   
 11. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #11
  Dec 12, 2009
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  exim sasa hivi wametoa huduma mpya ya faida acc nimeifwatilia sijapata detail sana ila ina visa na credit card ila ni debit na unafungua kwa kuanzia elfu 5000 na inakuwa na insurence ya millioni moja aina makato unapochukua na unatumia kwenye mashine yoyote ndani na nje ya nchi
   
 12. M

  Mubii Senior Member

  #12
  Dec 12, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 149
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mimi nina kadi ya Exim Silver na Visa ya CRDB. Zote zinafanya kazi. Lakini nimekuwa napata shida kidogo na kadi ya Exim nyakati nyingine nikiwa nataka kununua kitu on line. Kadi inakuwa rejected. Ila kwa kutumia Visa card ya CRDB sijawahi kupata tatizo hilo.
   
 13. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #13
  Dec 16, 2009
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kajiunge na faida account hope tatizo litakwisha
   
Loading...