mmmh!, naona kama vile kichwa cha habari hakihusiani na dondoo ulizowakilisha. Mfamaji unafahamu vizuri lakini lengo na nia ya hii summit?
Mfanyabiashara hapaswi kulalamika iwapo mteji avutiwi na bidhaa yake, anachopaswa kufanya ni kubuni mbinu za kumvuta. Iwapo atashindwa yeye ndio mwenye matatizo sio mteja.
Somo nililosoma hapa ni kwamba wafanyabiashara hao wa Tanzania wanaolalamika hawajui the very basic principle of marketing!
Sorry, mkuu, naomba nikuulize, wakati walipoambiwa na waziri kwamba 'wachangamkie dili Arusha' na wajitokeze kwa wingi kuuza bidhaa kwa watalii watakaokuja, mbona hawakuongelea masuala ya viwango? Mimi sioni kama tatizo ni viwango, tatizo ni kuwa walidanganywa na kupewa matumaini. Wamepoteza pesa zao kulipia stalls na kusafiri na bidhaa zao Arusha, kumbe hakuna kitu!
This is a farce!
Hebu tueleze wewe vizuri lengo na nia ya hii summit, maana some of us just smell something is wrong, if you get my gist!!
Overiden by time brother. Hapa naeleza nilichoona na kusikia hapa kwenye hii summit Arusha. Sijasema mazuri yake ambayo yapo na ya kuapreciate maana wote mmeona na kusikia kwenye radio na Tv. Hili la kulalamika na kwamba watu wako kimisionari zaidi ya kibiashara linaweza likatupa challenge.
Good news ni kwamba saa 4.0 kamili asubuhi ya leo 5/6/2008 MC ametangaza kwamba leo mchana Delegetes wote watatemebelea mabanda na kwamba gari la matangazo litapita mjini kuwatangazia wananchi waende kwenye mabanda kuona na kunua bidhaa.Haikuwepo kwenye ratiba kabisaaaaa. Wametusoma fresh hapa hapa JF.
Love u JF .
Yesterday the summit themes were on education and electricity crisis in Africa. All went well except that Tanzanian business men and women compalined bitterly about the whole thing.
They complain about poor or no sales because the Americans have no time
or interest to even visit their pavilons. They lament that the fees paid were too high compared to the real situation and expectations.
While the enterpreners are complaining the following is the general observation.
1. Americans are looking more or less like religious group than business men
and women. Infact their African counterparts present more buisiness
deeminor than them . No body knows exactly who is who in this forum.
Ngoja tusubiri ya leo.
2. About 90% of exhibitors at AICC are baticks.
3. Very few americans have taken trouble to visit the pavilions. Hawana interest.
4. Waziri Sophia Simba aumbuliwa kwa kutaka kuingia kwenye maakuli bila Tag.
Aambiwa no Tag no food .Sorry madam even if you were a minister. Ili
uingie dinner au lunch unapaswa kuwa na tag ya delegete .Sophia hakuwa
nayo.
Registration fee kwa delegate ni dola 500 na participant ni dola 20.
5. Sumayi naye ajitambulisha kama Waziri Mkuu wa zamani kwenye registration desk. Aambiwa please get youself in to que .no priorities here.
6. Leo wanadiscuss about small and meduim business in Africa na America and how to. Ukumbi ni Mabayumabayu ambao unabeba watu wasiozidi 400. Nadhani hapatakalika kama hawakubadili venue iwe Simba maana kila mtu hapa anasubiri hilo. Ndio unaanza saa hii. Ngoja nisogee huko.
Mfanyabiashara hapaswi kulalamika iwapo mteji avutiwi na bidhaa yake, anachopaswa kufanya ni kubuni mbinu za kumvuta. Iwapo atashindwa yeye ndio mwenye matatizo sio mteja.
Somo nililosoma hapa ni kwamba wafanyabiashara hao wa Tanzania wanaolalamika hawajui the very basic principle of marketing!
Alafu naomba mtu aweke hapa article niliiona kwenye gazeti kwamba Waziri Mary Nagu wa Viwanda na Biashara amezomewa na kutimuliwa kwenye viwanja vya nane kwa kuwa viongozi mwaka huu wamekacha kwenda kwenye maonyesho (sijui ni maonyesho gani haya?) wakiwa huo Sullivan. Ni gazeti la kila siku la kiswahili. Sijui ni udaku? lakini hii inaonyesha ni kwa njia gani wananchi walivyochoka. Alama za nyakati....
Wakati naandika post hii mkuu Zemarcopolo. nilikuwa naangalia habari kuhusu sulivan na malalamiko ya wachuuzi wetu waliokamuliwa hela ili washiriki sulivan.
Kutokana na jina langu kuwa ni msanii naomb nikuingize ktk fani uone mapungufu kadhaa ambayo yangeweza kufanyiwa kazi awali.
1. maandalizi hayakulenga kuwahamasisha wajasiriamali kushiriki, na kwa tafsiri aliyonayo mama Nagu ni kuwa wajasiriamali ni wauza batik na vikoi na wine za ndizi....
2. culture tourism hikupewa nafasi ktk mkutano wa sulivan, kwani hata soundtrack za mkutanoni pamoja na zile za matangazo ya video hazikulenga kuuza muziki wa utamaduni au wa asili wa tanzania. Hebu fikiria Wimbo wa Taifa letu unaimbwa na Mmarekani ktk soil ya nchi yetu kwenye mkutano mkubwa vile inaita kweli akilini?
3. Ukiritimba wa SIDO na ujambazi wake wa kuwaibia wawekezaji wenye mitaji midogo kwa udanganyifu wa kuwakuzia masoko yao kwa kuwapeleka kwenye maonesho tena wakiwalipisha gharama kubwa.... Hii ndiyo factor mojawapo inayowapelekea wauza batik wetu kushindwa kuelewa somo (Arusha) kwani hawakuwahi kupewa somo la ujasiriamali na sido ingawa wanailipa wanaposhiriki ktk shughuli za sido...
4. Hii inaingia kweli akilini kwamba Mama Nagu anasema kuwa hajui hata ratiba ya mkutano tena mbele ya vyombo vya habari akijibu complains za waoneshaji? Na kwa nini Mkutano ule wenye malengo ya kiuchumi usimamiwe kiprotokali na Wizara ya mambo ya nje?? Serikali haikuwa makini ktk hilo kwani Wizara ya Viwanda na biashara, ya Maliasili ya Utalii, Ya mambo ya Ndani au hata ya fedha zingeshiriki ktk protokali za ajenda za mkutano. Waafrika wenzetu hasa wakenya walifanya booking za full delegates kibao wakati sie tulihamasishwa hasa za participants (vendors). Ndiyo maana hata kutokana na matatizo yaliyojitokeza kenya kuhusu uchaguzi hayakuweza kutupa mwanya wa kulead kiuchumi kwani tumejaa wakiritimba kila kona na kila nyanja. Kumbuka hotuba ya Kagame pale sulivan alitolea mfano wa Mombasa lakini dongo lilikuwa ni kwetu (mwenye akili afahamu)
5. Uzembe uliotokana na maafisa wa wizara ya nje ambao wanajua diplomasia (mahusiano) na si trade, ndio ulisababisha hata kipindi kile cha mkutano wa SADC uliofanyika Golden Tulip kutokuwa wa kimafanikio kiuchumi kwetu. Waliwakusanya vendors na kuwaweka upenuni mwa ukumbi wa mkutano, halafu wakawatelekeza hapo wala hawakuweka ktk ratiba kw delegates kutembelea hayo maonesho waliyoyaandaa sana sana sabotage waliyoifanya ni kuwakusanya delegates na kuwapeleka mtaa wa mkunguni kununua batik za bei poa zisizo na viwango ambazo zitakuwa zimetutangaza ktk nchi za SADC how low graded products we produce. Hivyo msitegemee kama kutakuwa na mabadiliko kwa miaka mingi ijayo endapo siasa itashika hatamu kila nyanja.
serikali lazima ifanye homework ya kuhakikisha kuwa uzalendo unaanzia kwa viongozi ili sisi wananchi tuweze kuiga. Kwa uzembe wa aina hii nadhani funzo tulilopata hapa linatosha kabisa kumwondoa mama Nagu ktk nafasi yake ya biashara na viwanda aletwe mchapakazi....
TUJISAHIHISJE (JK Nyerere)
JF IDUMU