Exhibitors Complaints Against Sullivan Summit

Mfamaji

JF-Expert Member
Nov 6, 2007
6,633
1,920
Yesterday the summit themes were on education and electricity crisis in Africa. All went well except that Tanzanian business men and women compalined bitterly about the whole thing.

They complain about poor or no sales because the Americans have no time
or interest to even visit their pavilons. They lament that the fees paid were too high compared to the real situation and expectations.

While the enterpreners are complaining the following is the general observation.

1. Americans are looking more or less like religious group than business men
and women. Infact their African counterparts present more buisiness
deeminor than them . No body knows exactly who is who in this forum.
Ngoja tusubiri ya leo.

2. About 90% of exhibitors at AICC are baticks.

3. Very few americans have taken trouble to visit the pavilions. Hawana interest.

4. Waziri Sophia Simba aumbuliwa kwa kutaka kuingia kwenye maakuli bila Tag.
Aambiwa no Tag no food .Sorry madam even if you were a minister. Ili
uingie dinner au lunch unapaswa kuwa na tag ya delegete .Sophia hakuwa
nayo.

Registration fee kwa delegate ni dola 500 na participant ni dola 20.

5. Sumayi naye ajitambulisha kama Waziri Mkuu wa zamani kwenye registration desk. Aambiwa please get youself in to que .no priorities here.

6. Leo wanadiscuss about small and meduim business in Africa na America and how to. Ukumbi ni Mabayumabayu ambao unabeba watu wasiozidi 400. Nadhani hapatakalika kama hawakubadili venue iwe Simba maana kila mtu hapa anasubiri hilo. Ndio unaanza saa hii. Ngoja nisogee huko.
 
mmmh!, naona kama vile kichwa cha habari hakihusiani na dondoo ulizowakilisha. Mfamaji unafahamu vizuri lakini lengo na nia ya hii summit?
 
Nilisema ktk thread fulani kuwa wengi waliokwenda silivan ni vendors mkakaa kimya. inaelekea biashara ya tanzania haina tofauti na za kimachinga.....

Shame to wizara ya viwanda na wizara ya utaliii..........
 
mmmh!, naona kama vile kichwa cha habari hakihusiani na dondoo ulizowakilisha. Mfamaji unafahamu vizuri lakini lengo na nia ya hii summit?

Hebu tueleze wewe vizuri lengo na nia ya hii summit, maana some of us just smell something is wrong, if you get my gist!!
 
Mfanyabiashara hapaswi kulalamika iwapo mteji avutiwi na bidhaa yake, anachopaswa kufanya ni kubuni mbinu za kumvuta. Iwapo atashindwa yeye ndio mwenye matatizo sio mteja.

Somo nililosoma hapa ni kwamba wafanyabiashara hao wa Tanzania wanaolalamika hawajui the very basic principle of marketing!
 
Sorry, mkuu, naomba nikuulize, wakati walipoambiwa na waziri kwamba 'wachangamkie dili Arusha' na wajitokeze kwa wingi kuuza bidhaa kwa watalii watakaokuja, mbona hawakuongelea masuala ya viwango? Mimi sioni kama tatizo ni viwango, tatizo ni kuwa walidanganywa na kupewa matumaini. Wamepoteza pesa zao kulipia stalls na kusafiri na bidhaa zao Arusha, kumbe hakuna kitu!
This is a farce!
 
Research ni sehemu ya investment, kama walikubali sentensi ya waziri wakainvest pesa yao bila kutafiti faida wanayoweza kupata basi walikubali risk kubwa kuliko waliyoweza kuafford.

Na huyo waziri naye simtetei kwa sababu mfanyabiasha wa Tanzania akipata hasara ni hasara kwa taifa hivyo basi waziri naye ametutia hasara kwa sentensi yake isiyokuwa backed up na research and fugures.

Kwahiyo, kama hawajafirisika kutokana na kuudhuria kwao maonyesho hayo, basi wajifunze kuwa ni somo kwa ajili ya kujiandaa vizuri zaidi baadae. Kama wapo ambao kuhudhuria kwao mkutano kumesababisha wafirisike basi wajitokeze ili tuangalie jinsi ya kuwasaidia.

Waziri aombwe kutoa ufafanuzi wa sentensi yake, akibainika kuwa lisema kihuni, awajibishwe.
 
Hebu tueleze wewe vizuri lengo na nia ya hii summit, maana some of us just smell something is wrong, if you get my gist!!

Overiden by time brother. Hapa naeleza nilichoona na kusikia hapa kwenye hii summit Arusha. Sijasema mazuri yake ambayo yapo na ya kuapreciate maana wote mmeona na kusikia kwenye radio na Tv. Hili la kulalamika na kwamba watu wako kimisionari zaidi ya kibiashara linaweza likatupa challenge.

Good news ni kwamba saa 4.0 kamili asubuhi ya leo 5/6/2008 MC ametangaza kwamba leo mchana Delegetes wote watatemebelea mabanda na kwamba gari la matangazo litapita mjini kuwatangazia wananchi waende kwenye mabanda kuona na kunua bidhaa.Haikuwepo kwenye ratiba kabisaaaaa. Wametusoma fresh hapa hapa JF.

Love u JF .
 
Hongera kwa kazi nzuri. Jamii itakumbuka na kuuenzi mchango wako.
 
Yesterday the summit themes were on education and electricity crisis in Africa. All went well except that Tanzanian business men and women compalined bitterly about the whole thing.

They complain about poor or no sales because the Americans have no time
or interest to even visit their pavilons. They lament that the fees paid were too high compared to the real situation and expectations.

While the enterpreners are complaining the following is the general observation.

1. Americans are looking more or less like religious group than business men
and women. Infact their African counterparts present more buisiness
deeminor than them . No body knows exactly who is who in this forum.
Ngoja tusubiri ya leo.

2. About 90% of exhibitors at AICC are baticks.

3. Very few americans have taken trouble to visit the pavilions. Hawana interest.

4. Waziri Sophia Simba aumbuliwa kwa kutaka kuingia kwenye maakuli bila Tag.
Aambiwa no Tag no food .Sorry madam even if you were a minister. Ili
uingie dinner au lunch unapaswa kuwa na tag ya delegete .Sophia hakuwa
nayo.

Registration fee kwa delegate ni dola 500 na participant ni dola 20.

5. Sumayi naye ajitambulisha kama Waziri Mkuu wa zamani kwenye registration desk. Aambiwa please get youself in to que .no priorities here.

6. Leo wanadiscuss about small and meduim business in Africa na America and how to. Ukumbi ni Mabayumabayu ambao unabeba watu wasiozidi 400. Nadhani hapatakalika kama hawakubadili venue iwe Simba maana kila mtu hapa anasubiri hilo. Ndio unaanza saa hii. Ngoja nisogee huko.

Somo kubwa pia hapa ni kwamba viongozi wetu Sumaye zamani kiongozi na Simba wote wame prove kwamba hata heshima na utawala bora hawauwezi kwa kuwa wanatanguliza vyeo na majibvuno wakakumbana na kisiki .Kitendo cha mtu kusema eti mimi napita najulikana ni waziri mkuu wam zamani ama mimi ni waziri ni majivuno ya kijinga na huu si utawala bora .Kama wanashindw akuheshimu utaratibu wa kuingia mahali je wanaweza kusimamia mambo makubwa ?

Ujinga huu ndiyo unarudisha nyuma maendeleo ya Tanzania kwa watu kutumia majina na vyeo kila mahali .
 
heheh safi Mfamaji kwa update ni kweli inaelekea haikuwepo ratiba maalum ya delegates kutembelea mabanda mana kuingia tu kwenye mkutano kama tunavojua ilikua kaseheshe.
so i hope wana mabanda watajiuza hata kama nafasi ni moja tu basi waitumie.
 
nadhani "mabayumabayu" ni makosa ya maandishi. ukumbi uliopo aicc unaitwa 'mbayumbayu" ambaye ni ndege

macinkus
 
Ili kumaliza complain hii na kujaribu kusawazisha mabonde President Jk atatembelea mabanda hayo mchana huu na yeye. Habari za kuaminika ni kwamba wafanyabiashara walipanga kuandamana leo hii.HAta hivyo haijafahamika kama watendelea na mpango au la maana hata kama wageni wote watatemeblea hizo pavilon chances za wao kuuza bighaa zao kwa wingi ni sifuri. Na kesho ni mwisho wa mchezo.
 
Hili la maadamano!!!

Hata kama nitashio tu na hatakama haikutokea...Ni ujumbe tosha kuwa ...hu si muda wa kipuuzi Tanzania....Its time viongozi na uongozi uliopo wajifunze...kuwa Uongozi ni Dhamana...Sio kuropoka mambo siyokuwepo na kutendeka.

Kama maadamano yatakuwepo ni swala la jema ...Nikweli habari za malalamko toka wa wajasiriamali wadogo...ni nyingi!

lets wait and get the final outcome of this SS
 
Mfanyabiashara hapaswi kulalamika iwapo mteji avutiwi na bidhaa yake, anachopaswa kufanya ni kubuni mbinu za kumvuta. Iwapo atashindwa yeye ndio mwenye matatizo sio mteja.

Somo nililosoma hapa ni kwamba wafanyabiashara hao wa Tanzania wanaolalamika hawajui the very basic principle of marketing!

Wakati naandika post hii mkuu Zemarcopolo. nilikuwa naangalia habari kuhusu sulivan na malalamiko ya wachuuzi wetu waliokamuliwa hela ili washiriki sulivan.

Kutokana na jina langu kuwa ni msanii naomb nikuingize ktk fani uone mapungufu kadhaa ambayo yangeweza kufanyiwa kazi awali.

1. maandalizi hayakulenga kuwahamasisha wajasiriamali kushiriki, na kwa tafsiri aliyonayo mama Nagu ni kuwa wajasiriamali ni wauza batik na vikoi na wine za ndizi....

2. culture tourism hikupewa nafasi ktk mkutano wa sulivan, kwani hata soundtrack za mkutanoni pamoja na zile za matangazo ya video hazikulenga kuuza muziki wa utamaduni au wa asili wa tanzania. Hebu fikiria Wimbo wa Taifa letu unaimbwa na Mmarekani ktk soil ya nchi yetu kwenye mkutano mkubwa vile inaita kweli akilini?

3. Ukiritimba wa SIDO na ujambazi wake wa kuwaibia wawekezaji wenye mitaji midogo kwa udanganyifu wa kuwakuzia masoko yao kwa kuwapeleka kwenye maonesho tena wakiwalipisha gharama kubwa.... Hii ndiyo factor mojawapo inayowapelekea wauza batik wetu kushindwa kuelewa somo (Arusha) kwani hawakuwahi kupewa somo la ujasiriamali na sido ingawa wanailipa wanaposhiriki ktk shughuli za sido...

4. Hii inaingia kweli akilini kwamba Mama Nagu anasema kuwa hajui hata ratiba ya mkutano tena mbele ya vyombo vya habari akijibu complains za waoneshaji? Na kwa nini Mkutano ule wenye malengo ya kiuchumi usimamiwe kiprotokali na Wizara ya mambo ya nje?? Serikali haikuwa makini ktk hilo kwani Wizara ya Viwanda na biashara, ya Maliasili ya Utalii, Ya mambo ya Ndani au hata ya fedha zingeshiriki ktk protokali za ajenda za mkutano. Waafrika wenzetu hasa wakenya walifanya booking za full delegates kibao wakati sie tulihamasishwa hasa za participants (vendors). Ndiyo maana hata kutokana na matatizo yaliyojitokeza kenya kuhusu uchaguzi hayakuweza kutupa mwanya wa kulead kiuchumi kwani tumejaa wakiritimba kila kona na kila nyanja. Kumbuka hotuba ya Kagame pale sulivan alitolea mfano wa Mombasa lakini dongo lilikuwa ni kwetu (mwenye akili afahamu)

5. Uzembe uliotokana na maafisa wa wizara ya nje ambao wanajua diplomasia (mahusiano) na si trade, ndio ulisababisha hata kipindi kile cha mkutano wa SADC uliofanyika Golden Tulip kutokuwa wa kimafanikio kiuchumi kwetu. Waliwakusanya vendors na kuwaweka upenuni mwa ukumbi wa mkutano, halafu wakawatelekeza hapo wala hawakuweka ktk ratiba kw delegates kutembelea hayo maonesho waliyoyaandaa sana sana sabotage waliyoifanya ni kuwakusanya delegates na kuwapeleka mtaa wa mkunguni kununua batik za bei poa zisizo na viwango ambazo zitakuwa zimetutangaza ktk nchi za SADC how low graded products we produce. Hivyo msitegemee kama kutakuwa na mabadiliko kwa miaka mingi ijayo endapo siasa itashika hatamu kila nyanja.

serikali lazima ifanye homework ya kuhakikisha kuwa uzalendo unaanzia kwa viongozi ili sisi wananchi tuweze kuiga. Kwa uzembe wa aina hii nadhani funzo tulilopata hapa linatosha kabisa kumwondoa mama Nagu ktk nafasi yake ya biashara na viwanda aletwe mchapakazi....

TUJISAHIHISJE (JK Nyerere)

JF IDUMU
 
Last edited:
Alafu naomba mtu aweke hapa article niliiona kwenye gazeti kwamba Waziri Mary Nagu wa Viwanda na Biashara amezomewa na kutimuliwa kwenye viwanja vya nane kwa kuwa viongozi mwaka huu wamekacha kwenda kwenye maonyesho (sijui ni maonyesho gani haya?) wakiwa huo Sullivan. Ni gazeti la kila siku la kiswahili. Sijui ni udaku? lakini hii inaonyesha ni kwa njia gani wananchi walivyochoka. Alama za nyakati....
 
Mambo yote hadharani, ni kweli Waziri Nagu alikiona cha moto kama gazeti la Tanzania Daima - Sauti ya Watu lilivyotanabaisha.

Wajasiriamali wamtimua Waziri Nagu

na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima - Sauti ya Watu

WAJASIRIAMALI zaidi ya 500 kutoka mikoa 17 nchini na nchi jirani za Kenya na Uganda, jana walimtimua kwa hasira Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Mary Nagu, ambaye aliwatembelea katika viwanja vya maonyesho vilivyopo katika viwanja vya Nane Nane mjini hapa.

Wafanyabiashara hao walifikia hatua ya kumtimua waziri huyo, kutokana na hasira za kususwa na viongozin wa serikali tangu kuanza kwa mkutano wa nane wa Leon Sullivan, Jumatatu.

Waziri Nagu aliokolewa na polisi kutoka kwa wananchi hao wenye hasira, ambao baadhi yao walitishia kumdhuru wakidai kuwa serikali imewasababishia hasara kubwa kwa kuwaleta Arusha kwa ajili ya maonyesho na kisha kuwasusa.

Aidha, wajasiariamali hao wametishia kuandamana leo hadi ikulu, kumuona Rais Jakaya Kikwete, wakilalamikia kutapeliwa katika ushiriki wa maonyesho ya biashara ya kimataifa.

Awali, wakizungumza na waandishi wa habari na Mbunge wa Ngorongoro, Vincent ole Telele, wajasiriamali hao walisema hadi jana, maonyesho yao yalikuwa hayapati watembeleaji wa kutosha miongoni mwa washiriki wa mkutano wa Leon Sullivan.

Walisemsa hali hiyo inawafanya wahisi kuwa wametapeliwa na serikali, kwani wao walifika Arusha kushiriki maonyesho hayo baada ya kuhamasishwa mikoani na maofisa wa serikali kuwa katika maonyesho hayo watapata biashara kutoka kwa Wamarekani hao.

Wajasiriamali hao wanaotaka kuandamana wapo katika viwanja vya Chama cha wakulima (TASO), ambako maonyesho yao yamedorora licha ya uwanja kuandaliwa na kuwekewa huduma muhimu zikiwepo taa za usiku. Baadhi yao, wanaouza vyakula vya asili, jana walilazimika kuvimwaga baada ya kuanza kuharibika.

Khadija John, kutoka mkoani Iringa, Rahel Fredy wa Manyara na Mariam Hamadi wa Zanzibar, walisema kwa nyakati tofauti kuwa wamefika katika maonyesho hayo wakitarajia kutembelewa na wageni, lakini badala yake wageni hao kutoka Marekani juzi jioni wamepelekwa katika kituo binafsi cha Cultural Heritage cha mjini hapa.

“Sisi tumekuja huku Arusha baada ya kuhamasishwaa mikoani kuwa kuna maonyesho na Wamarekani na washiriki wengine wa mkutano watakuja kututembelea lakini tunashaa kwua hadi leo, siku moja kabla ya mkutano kwisha, hatujatembelewa na wageni hao,” alisema Hamadi.

Hamadi alisema tangu wafike mkoani Arusha wakitokea Zanzibar, hawajauza bidhaa yoyote na wamekuwa wakiishi kwa taabu kutokana na kutotembelewa na watu katika mabanda yao.

“Walikuja hadi Zanzibar wakatuomba tuje huku, tena tutengeneze business card nyingi, tumekuja nazo hata hao wa kuwapa hawapo,” alisema Hamadi ambaye ni mwanakikundi cha BAMITA.

Alisema sasa wahajui hata watarudi vipi Zanzibar kwani hakuna biashara walizofanya na hakuna hata watazamaji ambao wangeweza kuona bidhaa zao.

Khadija John, ambaye ni mkurugenzi wa kikundi cha KHG cha Iringa, ambacho kinajihusisha na bidhaa za ufumaji, alisema tangu wamefika Arusha wameshindwa kuuza bidhaa zao.

“Kama hali hii ikiendelea kesho itabidi tuandamane twende kwa rais, aeleze nani atalipa gharama zetu,” alisema John.

Akizungumza mara baada ya kutembelea mabanda yote, Telele alisema anashangazwa na maofisa wa wizara zinahohusika na mambo ya ndani, biashara na utalii kuwatelekeza wajasiriamali hao.

Hadi jana, Telele alionekana kuwa ndiye kiongozi pekee wa juu kutembelea maonesho hayo tangu yalipotembelewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na kuridhishwa na maandalizi, alisema kinachoonekana ni wajasiriamali hao kutelekezwa.

“Hata mimi namuomba Rais Kikwete kuwaagiza wahusika kuwaleta hapa washiriki wa Sullivan badala ya kuwapeleka katika maduka binafsi,” alisema Telele.

Akizungumzia hali hiyo, Mwenyekiti wa kamati ya Mkoa wa Arusha ya maonyesho hayo, ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha wenye viwanda, wakulima na wafanyabiashara wa Mkoa waArusha, James Kangaro, naye alionyesha kushangazwa na hali hiyo.

“Mimi binafsi nimeonana na Katibu Mkuu kiongozi, Philemon Luhanjo na kumueleza hali hii, lakini anasema watakuja tu na tunashangaa kuambiwa jana walikwenda Cultural Heritage na kuwatelekeza wajasiriamali hawa,” alisema Kangaro
 
Wakati naandika post hii mkuu Zemarcopolo. nilikuwa naangalia habari kuhusu sulivan na malalamiko ya wachuuzi wetu waliokamuliwa hela ili washiriki sulivan.

Kutokana na jina langu kuwa ni msanii naomb nikuingize ktk fani uone mapungufu kadhaa ambayo yangeweza kufanyiwa kazi awali.

1. maandalizi hayakulenga kuwahamasisha wajasiriamali kushiriki, na kwa tafsiri aliyonayo mama Nagu ni kuwa wajasiriamali ni wauza batik na vikoi na wine za ndizi....

2. culture tourism hikupewa nafasi ktk mkutano wa sulivan, kwani hata soundtrack za mkutanoni pamoja na zile za matangazo ya video hazikulenga kuuza muziki wa utamaduni au wa asili wa tanzania. Hebu fikiria Wimbo wa Taifa letu unaimbwa na Mmarekani ktk soil ya nchi yetu kwenye mkutano mkubwa vile inaita kweli akilini?

3. Ukiritimba wa SIDO na ujambazi wake wa kuwaibia wawekezaji wenye mitaji midogo kwa udanganyifu wa kuwakuzia masoko yao kwa kuwapeleka kwenye maonesho tena wakiwalipisha gharama kubwa.... Hii ndiyo factor mojawapo inayowapelekea wauza batik wetu kushindwa kuelewa somo (Arusha) kwani hawakuwahi kupewa somo la ujasiriamali na sido ingawa wanailipa wanaposhiriki ktk shughuli za sido...

4. Hii inaingia kweli akilini kwamba Mama Nagu anasema kuwa hajui hata ratiba ya mkutano tena mbele ya vyombo vya habari akijibu complains za waoneshaji? Na kwa nini Mkutano ule wenye malengo ya kiuchumi usimamiwe kiprotokali na Wizara ya mambo ya nje?? Serikali haikuwa makini ktk hilo kwani Wizara ya Viwanda na biashara, ya Maliasili ya Utalii, Ya mambo ya Ndani au hata ya fedha zingeshiriki ktk protokali za ajenda za mkutano. Waafrika wenzetu hasa wakenya walifanya booking za full delegates kibao wakati sie tulihamasishwa hasa za participants (vendors). Ndiyo maana hata kutokana na matatizo yaliyojitokeza kenya kuhusu uchaguzi hayakuweza kutupa mwanya wa kulead kiuchumi kwani tumejaa wakiritimba kila kona na kila nyanja. Kumbuka hotuba ya Kagame pale sulivan alitolea mfano wa Mombasa lakini dongo lilikuwa ni kwetu (mwenye akili afahamu)

5. Uzembe uliotokana na maafisa wa wizara ya nje ambao wanajua diplomasia (mahusiano) na si trade, ndio ulisababisha hata kipindi kile cha mkutano wa SADC uliofanyika Golden Tulip kutokuwa wa kimafanikio kiuchumi kwetu. Waliwakusanya vendors na kuwaweka upenuni mwa ukumbi wa mkutano, halafu wakawatelekeza hapo wala hawakuweka ktk ratiba kw delegates kutembelea hayo maonesho waliyoyaandaa sana sana sabotage waliyoifanya ni kuwakusanya delegates na kuwapeleka mtaa wa mkunguni kununua batik za bei poa zisizo na viwango ambazo zitakuwa zimetutangaza ktk nchi za SADC how low graded products we produce. Hivyo msitegemee kama kutakuwa na mabadiliko kwa miaka mingi ijayo endapo siasa itashika hatamu kila nyanja.

serikali lazima ifanye homework ya kuhakikisha kuwa uzalendo unaanzia kwa viongozi ili sisi wananchi tuweze kuiga. Kwa uzembe wa aina hii nadhani funzo tulilopata hapa linatosha kabisa kumwondoa mama Nagu ktk nafasi yake ya biashara na viwanda aletwe mchapakazi....

TUJISAHIHISJE (JK Nyerere)

JF IDUMUNimekupata mkuu, I salute you!

Kuhusu wimbo wa Taifa, unazungumzia wale wadada wawili (mmoja alikuwa na titi kubwa)? Were they Americans, mbona uimbaji wao ulikuwa tofauti sana? Sikupenda wimbo wa Taifa letu ulivyoimbwa, dunno who trained her..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom