EXCLUSIVE;Kamanda wa M23 ajisalimisha Uganda

mwekundu

JF-Expert Member
Mar 4, 2013
21,859
19,700
131105144849_m23_304x171_getty.jpg

Waasi wa M23 wametimuliwa kutoka katika maeneo waliyokuwa wamekita kambi

Maafisa wa Serikali ya Uganda wanasema kuwa kamanda wa kijeshi wa wapiganaji walioshindwa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, M23, amejisalimisha kwa utawala wa Uganda.
Ripoti kutoka Uganda zinasema kuwa mamia ya wapiganaji wamejisalimisha pamoja na kiongozi wao, Sultani Makenga.
Wapiganaji hao wamejisalimisha katika eneo la hifadhi ya Wanyama ya Pori ya Mgahinga, kwenye mpaka wa Uganda na DRC.
Mnamo Jumanne M23 walisema kuwa wamesitisha maasi yao ya miezi 20 Mashariki mwa Congo, baada ya kutimuliwa katika ngome zao Mashariki mwa Congo na wanajeshi wa Serikali wakishirikiana na askari wa kudumisha amani wa Umoja wa Mataifa.

SOURCE :Kamanda wa M23 ajisalimisha Uganda - BBC Swahili - Habari
 
KAMPALA, Uganda – A Ugandan military official says at least 1,700 Congolese M23 rebels, including the top commander, have surrendered to Ugandan authorities.

The official said Thursday M23's Gen. Sultani Makenga and his fighters were being held by the Ugandan military in Mgahinga, near the Congo border.


The official, who spoke on condition of anonymity because he was not authorized to give this information, said the rebels had been disarmed and were being registered by Ugandan officials.

Full: Official: 1,700 M23 Rebels Surrender to Uganda
 
kweli nimeamini vijana walichapika, watu zaidi 1700 wenye silaha kunyanyua mikono juu si mchezo, hali ilikua tete sana kwa upande wao
 
Tuna hamu sana na new DRC, isiyokuwa na vita, yenye kuenjoy rasimali sana wenyewe!
 
haitoshi tunataka wakamatwe ili wawataje ni akina nani walikua wanawafadhili kifanya upuuzi huo;ili wakamatwe wafidie gharama za vita.ikumbjkwe katika upuuzi wao wamesababisha maisha ya watu kibao kjpotea askar wetu wamepoteza maisha.lazima wawajibishwe
 
Tuna hamu sana na new DRC, isiyokuwa na vita, yenye kuenjoy rasimali sana wenyewe!
Nimesoma report moja ya World Bank na pia The East African. Ukiisoma unaweza ukatoka machozi!
Inakadiriwa kuna utajiri wa madini including rare earth minerals kule DRC yenye thamani ya 33 Trillion USD. This is more than the GDP of USA and all EU combined! Kila mtu analijua hilo
DRC wakitulia na kuwa makini basi hakuna cha S. Africa, Kenya, EAC, China, US wala nchi yoyote duniani itaweza kuipata kiuchumi.................lakini ndio hivyo tena...........pengine ni kweli wabantu tumelaaniwa. Somentimes jinsi mambo yanavyoendelea ktk nchi zetu inanifanya niamini ni kweli watu weusi tumelaaniwa.
 
Hawa m23 si walisema wanajeshi wetu wote watarudi wkiwa kwenye majeneza? Hii safari haitakiwi kuishia Uganda inatakiwa kwenda mpaka ICC.
 
Back
Top Bottom