Excel kupanga matokeo, divisions na points

Asante sana, ngoja nijaribu kuwasiliana naye anipe ujanja wa kufanya hivyo maana njia hii ya kuandika, hata mi inaniwia nzito kidogo
mkuu vp bado hujawasiliana nae
 
Mkuu nashukuru sna nimefanya nimefanikiwa nikitumia Point,Ila nikibadiri kuwa Grades mfano A,B,C.. inakuja hivi tatizo ni nini hapa mkuu?
 

Hiki kipengere kimenivuruga mkuu cha ku copy columns za points na divison nazi copy alafu nazi paste wapi maana hpa ni kweli nikibadiri huu mfumo wa point kuja katika Alama katika columnsv za Points na divison zinajivuga na kuja maneno ya ajabu
 
Hiki kipengere kimenivuruga mkuu cha ku copy columns za points na divison nazi copy alafu nazi paste wapi maana hpa ni kweli nikibadiri huu mfumo wa point kuja katika Alama katika columnsv za Points na divison zinajivuga na kuja maneno ya ajabu

Saaafi sana. Kwa kweli umekwenda vizuri sana. Kimsingi umesha maliza.
Ndio, hii ya mwisho ni changamoto, kwamba Points (1,2,3, etc) ndio zinazo kokotolewa na kuleta jumla ya points (18) na division (II). Sehemu zote hizo zinakua zimeunganika kimahesabu, hivyo unapobadili sehemu moja, kwa mfano ukiweka sasa alama (A,B,C etc), inaleta jambo hilo la ([HASHTAG]#NUM[/HASHTAG]!).
Kinachofanyika hapo, ni kuachanisha column hizo za Points na division kutoka katika utaratibu mzima. Hiyo inakupa sasa uhuru wa Kubadili sehemu ya nyuma kutoka katika utaratibu wa (1,2,3 nk) kwenda katika utaratibu wa (A,B,C nk)
Ukiclick cell ya division au ya points utaona inaonekana ina function badala ya namba.

Hii inatakiwa iondoke.

Inafanyikaje.
1. Select column zote mbili za Points na Division.
select kutoka juu, ili kama una wanafunzi 500 uwe ume-select wote

2. Right click selection kisha Copy
4. Ikiwa hivyo hivyo right-click tena
paste special

paste values



Sasa uki-click tena cell utaona values sio formula. Manake umezi-disconnect.



Sasa endelea, badili za ndani kuwa (A,B,C etc) bila kuathiri points na division.

Hii ni njia ya kwanza na ni ya kienyeji kidogo. Ubaya wake ni kwamba, labda unahitaji kubadilisha marks ya mwanafunzi, haitaleta mabadiliko kwenye points na divisions maana umesha ziachanisha. Ipo njia nyingine ambayo, unaweza kuzifanya bado ziwe zimeunganika zote. Na njia hiyo ni kwa kuvitenganisha vipengele na kuviunga kwa njia ambayo ukibadili marks za mwanafunzi zinabadili pia points na division. Ngoja nitayarishe maelezo yake nita-attach pia na excel.
 
Njia ya pili na ambayo itabadilisha points na division ukibadili marks za mwanafunzi.
Sasa kwanza download excel yangu hapo inayoitwa "Mfano Marks" halafu tuelekezane. (Kwa bahati mbaya office yangu ni 2007, pengine tunaweza kupishana kama una version ya mbele).
Utaona ina tabs tatu (Original, Points na Final) Kwenye excel tabs zinaweza kuongezwa na kupewa majina.


1. Kwenye Tab ya kwanza, utaona nimeweka table original zenye marks za wanafunzi, pamoja na vi-refference table viwili. Kimoja cha points na kingine cha divisions.
(By the way :- Unaweza pia kuweka kila kitu kwenye tab moja ila kazi itakua pana sana, kama unajua mbinu za kuhide cells inakua vizuri pia)
2. Kwenye tab ya Pili nimetengeneza Table ya vlookup.
Nimefanyaje.
Kwanza nikiwa hapo kwenye "tab" ya "points", nimeclick cell ya kwanza kabisa ambayo ni A1. Nikaweka alama ya swasawa "=". Nikaenda kwenye tab ya Original, nikaclick cell ya A1 ambayo ni "Student name" kisha nika bonyeza enter, Student name ikaja kwenye A1 ya tab ya Points. Nika click cell hiyo na kuivuta kwa kikona kwenda pembeni hadi mwisho. kama 0 zikitokea umepitiliza, zifute.

Kisha nika-select Student name na Sex hapohapo, nikazivuta kwenda chini kwa mtindo huo huo.

Nikaenda kiboksi cha kwanza juu kushoto C2 kenye tab hiyo hiyo ya Points, nika-click na nikaanza kuandika formula yangu ya vlookup.
Nikaandika hivi
=vlookup( kisha nikaclick tab ya original, halafu nikaclick C2 pale original, nikabonyeza mkato (coma). Baada ya hapo natakiwa niweke table array, nikaselect table B yote isipokua heading yake, kisha nikaboyeza F4 kuweka alama ya Dollar, nikabonyeza mkato tena, halafu nikaandika 3 kwamba ninachotakiwa kupata hapo ni points column ya tatu, mkato tena, halafu nikaandika true Nikafunga mabano. nikapress enter. Kwenye kiboksi C2 kwenye tab ya points ikaja point. Nikaiselect kisha nikaidrag kushoto kisha chini kama kawaida kujaza viboksi vya points vilivyo baki.
Kisha hapo hapo kwenye tab ya points nikaongeza column za columns za Points na divisions
3.Kwenye divisions nikatumia utaratibu wa Sum na small kama maelekezo awali.

4. Kwenye division nikaandika vlookup namna hii
Kwanza nikaclick kiboksi cha kwanza ambacho ni M2, kisha nikaandika =vlookup( kisha nikaclick kiboksi cha nyuma yake ni L2, nikabonyeza mkato, kisha nikaclick tab ya original, nikaselect table C yote isipokua heading, kisha nikabonyeza F4 kuweka alama za dola, kisha nikaweka mkato tena, nikaandika 2 kisha mkato, nikaandika true kisha, nikafunga mabano, kisha nikabonyeza enter. Division ikaja kwenye kiboksi cha M2 kwenye tab ya points. Nikaishika kwa kona nikaidrag chini kama kawaida kujaza viboksi vyote.

5. Kwenye tab ya final cell A1, nikaweka alama ya "=" Kisha nika-click tab ya points, na pale nikaclick cell ya kwanza yaani A1, nikabonyeza enter, Student name ikaja kwenye cell ya A1 kwenye tab ya final. Nikadrag kushoto, kujaza, kisha nika select student name na Sex, nikadrag chini kama nilivyo fanya awali kwenye tab ya points.
Nikaenda kwenye tab ya points tena. nikaclick cell ya somo ya kwanza juu kushoto, yaani C2. Nika-right click kisha nika-copy. Nikaenda kwenye tab ya final kwenye C2 nika-paste. Ikaja function ya vlookup niliyotumia kwenye tab ya points. Nikaenda kwenye kipengele cha 3 cha function hiyo ya vlookup, nikabadili 3 kuwa 2, kisha nikabonyeza enter. Kwenye kiboksi cha C2 kwenye tab ya final ikaja "A" ambayo ni mark ya mwanafunzi Chungwa Tamu katika somo la Biology.

Nika drag kushoto kisha chini kama kawaida kujaza viboksi vyote

6. Kwenye kiboksi cha L2 kwenye tab ya final, ambacho ni points za mwanafunzi Chungwa, nikaweka alama ya sawasawa "=" , kisha nika-click tab ya points nikaclick pale kiboksi L2, kisha enter. Points za mwanafunzi chungwa zikatokea pia kwenye kiboksi cha L2 kwenye tab ya final. Nikadrag kushoto hadi usawa wa division, kisha nikadrag zote chini hadi mwisho kujaza points na division kwenye tab ya final. Kitu kikawa kimetokea na mabadiliko yoyote ya marks yatakayo fanyika kwenye tab ya original tatatokea kila mahali.

Ndefu sana, lakini jaribu kuielewa. Usisahau kudownload excel yenyewe
 
Kumbe hawajamaa hawapokei excel, nai-upload namna gani sjui. Pengine kwa dropbox naileta baadae kidogo
 
Mkuu nmepiga kazi nimekwama kwenye division yan sijakupata hapo kwenye vlookup ya mwisho ili nipate división, nmejaribu inaniletea wanafunzi wote wamepata zero
 
Mkuu nmepiga kazi nimekwama kwenye division yan sijakupata hapo kwenye vlookup ya mwisho ili nipate división, nmejaribu inaniletea wanafunzi wote wamepata zero


Vlookup imegawanyika katika sehemu nne, kama unavyoona hapo
sehemu zimegawanywa kwa mikato


Vlookup kwenye upande wa division inakwenda namna hii:-
Kwenye namba moja ya function ni cell ile yenye jumla ya points ulizopata baada ya kukokotoa sum na small jumla points za mwanafunzi.
Kwenye namba mbili, weka cells range ya kale katable kanakoonyesha utaratibu wa divisions, kwamba division one inaanzia kwenye ngapi, division two inaanzia kwenye ngapi nk.
Kwenye namba tatu, weka 2, pengine hapa ndipo unapokosea labda unaweka 3. Weka 2 kwasababu katable kale ka utaratibu wa divisions kana columns 2 tu. Ukiweka 3 columna ya 3 haina kitu ndio maana pengine inakuletea zero.
Kwenye namba nne weka true, kwasababu ni relative, inayo karibiana.
Pia usisahau kudownload excel yangu na kuangalia nilivyo fanya. Click hapa kudownload excel ni ya mwaka 2007
 
Shukrani mkuu nimekuelewa sana hapa...naomba uelezee na pivot table
 
Mkuu mungu akubarik kazi nimekamilisha vizuri na sio ngumu kama nilivyokua nazani
 
Sijaelewa kwa kweli (Kiswahili kigumu!!) yaani hapo labda ungetumia lugha ya Malikia Elizabeth ndio ningelikuelewa!
 
Mimi nafanya sales,nina routes 5 na product 10 of different size (liter) nahitaji kuwa na template ambayo nikiingiza mauzo ya siku ya kila route na kila product na ujazo wake inipatie volume ya siku,wiki na mwezi kwa route,product,volume.
Naomba kueleweshwa tafadhali mkuu.
 
Hiyo iko poa! Ila bado ni manual work mimi nina mfumo (full automatic) kwa ajili ya management ya shule nzima kuanzia udahili kuchakata matokeo (mzazi au mlezi anaweza kuona matokea hayo) , tarifa za walimu (hr na finance ) makusanyo ya ada na n.k kwa maelezo zaidi anayetaka anione pm
 
Hayo mabano kama ya kwenye set katika formula ya sum(small(1,2,3,4,5,6,7)). Nayapata wapi mkuu.
 
Nashukuru kwa darasa ulilotoa. Binafsi nilikuwa natumia zaidi IF function kwenye kazi za hivyo ila nitajaribu hiyo function ya vlook
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…