Ex-wangu nakukumbuka sana, natamani urudi

JMF

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
1,735
2,686
Nilikuchezea sana miaka ile uliponitembelea. Sikukuchukulia serious. Niliamini tungekaa pamoja hadi kifo, kumbe ulikuwa unapita tuu. Sikujua ilivyo vigumu kukupata. Umeniachia kumbu kumbu nzuri na nyingine uliondoka nazo. Kwasasa ni machungu tuu nikikumbuka nilivyokuchukulia wa kawaida. Nilikuona wa kawaida na ndio maana nilidiriki kukurusha kwa Mr Nice stejini (naye anakukumbuka pia sababu hakukutuliza uishi nae) na hata kwa wasanii wengine wakutumie kujifutia jasho kazi ambayo ilikuwa ni ya kitambaa.

Sikumbuki kwa idadi ni mara ngapi tulitoka wote pamoja kwenda bar na kukuacha hata kwa wahudumu eti waku keep. Wale washkaji zangu niliokuwa nakutambishia kwao nao wakawa wanakumezea mate na kujaribu kukutongoza uachane na mimi uende kwao, leo hii hawaji tena kwangu na wamenitenga. Unamkumbuka Aire? Yule aliyekujaga kuniomba uende ukamsaidie kununua kiwanja? Tena nikakusahau kwake miaka pasipo kujali wala kukuulizia akurudishe nyumbani? Leo hii kile kiwanja kina uzio na walinzi ambao hata nijieleze vipi kwao kuwa mpenzi wangu ndiye aliyesaidia upatikanaji wake tena bure, hawataniruhusu kuingia.

Kuna wale wavivu waliolionea wivu penzi letu hata kudiriki kusema kuwa nimekuendea kwa mganga kukupata na hata alipofariki mama mkwe wako wakadai eti nimemtoa kafara na hata kuniogopa? Mimi leo ndo nawaogopa kwa maana Bado wapo vilevile ingawa wameshazeeka zeeka na wanavuta wote fegi moja watu watatu na double kick ya kupima kijiweni. Kila wanayemuona na mpenzi wanazusha vilevile. Hata Diamond nae wamemzushia.

Hivi una habari kule tulipokutana na wewe kwa mara ya kwanza na kuanzisha uhusiano pamezungushwa ukuta unaolindwa na askari ili nduguzako wasitoroshwe kama nilivyokutorosha?. Nasikia sikia umeolewa na jirani wa maeneo yale anaitwa Laizer, tena ni mzee na amekuoa wewe na pacha wako. Hadi kwenye TV ilirushwa tukashuhudia na una umbo kubwa sana, siyo kama nilipokupata mimi. Toroka uje mamii. Achana na wazee. Njoo hata na pacha mwenzako please! Tayari nimekua na siyo mtoto tena kama enzi zile. Tambua nilikuchezea sababu ya utoto wangu. Sikuwa na maarifa wala sikujua thamani yako. Sikujua kuna kitu kinaitwa kuachana. Labda sababu hukunisumbua sana kukupata ndiyo maana. Kwa nilivyopambana kukutafuta turudiane, hakika ukirudi hautojutia maamuzi yako. Save the date my love. Nimezunguka nchi 9, taasisi na makampuni mengi sana nikikutafuta na sijafanikiwa kukupata. Nakutana tuu na wanaofananafanana na wewe ila hawana uzuri kama ule wako na wengi wao kwao huwa naishia tuu kupungiwa mkono kwa mbali au kuniachia ile harufu nzuri ya manukato yako nikiwagusa au huiacha mkononi mwangu endapo imetokea kusalimiana katika mizunguko ya maisha.

Popote ulipo, ukiona ujumbe huu ujue kuwa bado nakukumbuka na nakuhitaji sana urudi mpenzi wangu.
With love
Boss Mtoto
(your ex)
 
Dear x anakumbukwaaa.
Vijana hawajaacha kulinganisha walipotoka na walipo ndo maana wanapata tabu
 
Nilikuchezea sana miaka ile uliponitembelea. Sikukuchukulia serious. Niliamini tungekaa pamoja hadi kifo, kumbe ulikuwa unapita tuu. Sikujua ilivyo vigumu kukupata.Umeniachia kumbu kumbu nzuri na nyingine uliondoka nazo. Kwasasa ni machungu tuu nikikumbuka nilivyokuchukulia wa kawaida. Nilikuona wa kawaida na ndiyomaana nilidiriki kukurusha kwa Mr Nice stejini (naye anakukumbuka pia sababu hakukutuliza uishi nae) na hata kwa wasanii wengine wakutumie kujifutia jasho kazi ambayo ilikuwa ni ya kitambaa. Sikumbuki kwa idadi ni marangapi tulitoka wote pamoja kwenda bar na kukuacha hata kwa wahudumu eti waku keep. Wale washkaji zangu niliokuwa nakutambishia kwao nao wakawa wanakumezea mate na kujaribu kukutongoza uachane na mimi uende kwao, leo hii hawaji tena kwangu na wamenitenga. Unamkumbuka Aire? Yule aliyekujaga kuniomba uende ukamsaidie kununua kiwanja? Tena nikakusahau kwake miaka pasipo kujali wala kukuulizia akurudishe nyumbani? Leo hii kile kiwanja kina uzio na walinzi ambao hata nijieleze vipi kwao kuwa mpenzi wangu ndiye aliyesaidia upatikanaji wake tena bure, hawataniruhusu kuingia.
Kuna wale wavivu waliolionea wivu penzi letu hata kudiriki kusema kuwa nimekuendea kwa mganga kukupata na hata alipofariki mama mkwe wako wakadai eti nimemtoa kafara na hata kuniogopa? Mimi leo ndo nawaogopa kwa maana Bado wapo vilevile ingawa wameshazeeka zeeka na wanavuta wote fegi moja watu watatu na double kick ya kupima kijiweni. Kila wanayemuona na mpenzi wanazusha vilevile. Hata Diamond nae wamemzushia.

Hivi una habari kule tulipokutana na wewe kwa mara ya kwanza na kuanzisha uhusiano pamezungushwa ukuta unaolindwa na askari ili nduguzako wasitoroshwe kama nilivyokutorosha?. Nasikia sikia umeolewa na jirani wa maeneo yale anaitwa Laizer, tena ni mzee na amekuoa wewe na pacha wako. Hadi kwenye TV ilirushwa tukashuhudia na una umbo kubwa sana, siyo kama nilipokupata mimi. Toroka uje mamii. Achana na wazee. Njoo hata na pacha mwenzako please! Tayari nimekua na siyo mtoto tena kama enzi zile. Tambua nilikuchezea sababu ya utoto wangu. Sikuwa na maarifa wala sikujua kujali hisia zako. Sikujua kuna kitu kinaitwa kuachana. Labda sababu hukunisumbua sana kukupata ndiyo maana. Kwa nilivyopambana kukutafuta turudiane, hakika ukirudi hautojutia maamuzi yako. Save the date my love. Nimezunguka nchi 9, taasisi na makampuni mengi sana nikikutafuta na sijafanikiwa kukupata. Nakutana tuu na wanaofananafanana na wewe ila hawana uzuri kama ule wako.

Popote ulipo, ukiona ujumbe huu ujue kuwa bado nakukumbuka na nakuhitaji sana urudi mpenzi wangu.
With love
Boss Mtoto
(your ex)
Ex nenda salama.... Mwenzako Nampa nyama aichomi anaila hata kama ikiwa mbichi

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Hivi ni kwanini kwa upande wangu inakuwa tofauti? Sjawai kaa nikakumbuka matapishi mimi
 
Ulinde Sana moyo wako kuliko vitu vyote maana huko ndiko zitokako chemchem za uzima.....na hakina kitu kingine kinaweza kuingia huko kwenye chem chem zaidi ya mapenzi. So bro acha tu mapenzi yaku drive
 
Back
Top Bottom