Ex kamuambikiza HIV

Naelewa kuhusu habari za kuusoma huu ugonjwa hakuna usichoelewa.

Sasa nahitaji urely kwenye kitu kinachokufanya usiamini uwepo wake
Sijawahi kuona Mtu anaumwa UKIMWI,
ila nimeona wagonjwa wa TB, KANSA, HOMA YA INI, MALARIA, TYPHOID, PRESHA, SUKARI, INI, MOYO, FIGO, GONO, KASWENDE, KICHWA, KIPINDU PINDU, KUHARA, n.k
 
Sijawahi kuona Mtu anaumwa UKIMWI,
ila nimeona wagonjwa wa TB, KANSA, HOMA YA INI, MALARIA, TYPHOID, PRESHA, SUKARI, INI, MOYO, FIGO, GONO, KASWENDE, KICHWA, KIPINDU PINDU, KUHARA, n.k
Safi sasa umekuja vizuri .
Rafiki Dream Queen hongera kwa kutowahi kuwaona wagonjwa wa hivyo ila pole pia maana hakika umekuwa nyuma.

Actually nimeanza kuona watu wa magonjwa hayo 200.. alikuwa ni mama yangu mzazi , sikujua mpaka alipofariki .

Akafuata mdogo wangu 200.. nilijua maana alikuwa akitumia dawa za maji alizokuwa anapimiwa kutokana na vipimo husika sababu alikuwa bado mdogo .

Finally miaka ya mbele kidogo, my late Father , wote walishafariki .

Twende sawa sasa , hapo juu nilikuwa najaribu kukuonesha UKIMWI upo na nilianza ushuhudia mda kidogo.

Sasa leo nakuleta kanda za juu kusini niko huku nahusika moja kwa moja na hawa watu vijijini huku hasa ushauri nasaha , kuwapa dawa , kuwafariji pale panapowezekana .

Utamjuaje mtu aliyeathirika ?
Mpenzi rafiki itakuchukua muda sana kumjua mtu aliyeathirika akawa anatumia dawa , rafiki unaweza usimjue kabisa pia .

Ila akiwa hajaanza dawa na CD4 yaani kinga mwili zikishuka sana basi ni rahisi kumtambua haraka kwa mambo yafuatayo.
1/Kuhara kusiko kwa kawaida au kusikokoma .

2/Upungufu wa uzito kwa kasi

3/Ngozi kukosa uangavu asilia .

4/Magonjwa nyemelezi kwa mtu huyo .

5/Vipere mparazo hasa sehemu zenye kupatwa na joto muda mwingi , basi wahenga wakasema mkanda wa jeshi .

6/Mabadiliko ya ute wa mate yake kuwa mzito kuliko kawaida.

Dada Dream Queen sikutumi ukawachunguze ila ukawe msaada maana kwa ulimwengu wa sasa UKIMWI si lolote na wala chochote.

Nakuona unaniuliza mbona unasema huu ugonjwa si lolote wala chochote ni kweli rejea miaka anuwahi katika mifano yangu hapo juu kwa hiyo miaka hali ya mtu mwenye hili gonjwa ilikuwa ni mbaya sana kiasi cha kuwapiteza watu wengi ila leo dawa zinasaidia sana kiasi cha kuwa mpaka viral load zinapungua YES

Unaniuliza ndiyo nini hiki ? Hiyo ni idadi ya virusi mwilini .
Ukiendelea kujifunza utakutana na watu wanasema mbona fulani ni muathirika ila ukimpima unakuta yupo negative

Hapo ndiyo tunasema viral load ziko chini sana sababu ya matumizi sahihi ya dawa japi ni rahisi kumgundua kwa kipimo kilicho kikubwa zaidi.

Natamani nikutumie mafile ya idadi ya waathirika ili walau ujue ni vipi huu ugonjwa uko nao katika jamii yako ila sasa mamlaka na sheria haziniruhusu.

Ndugu itoshe kusema UKIMWI upo jihadhari sana kwa kumlinda umpendaye na akupandaye.

Nipo kijiji ambacho nyumba nne basi tatu ni waathirika wote .

Nipo sehemu ambayo UKIMWI ni jambo la kawaida maana wengi wanao .

Nipo sehemu ambayo alhamisi ni siku ya kuwagawia dawa na ushauri na si ajabu kuhudumia watu zaidi ya mia saba mpaka mia tisa.

Na pia hawajifichi tena .
Najua haujayashuhudia haya sababu ya sehemu ulipo walio positive hawako tayari kujulikana.
 

Bado hujanionesha mgonjwa wa UKIMWI,
Sababu Kinga ya Mtu ikishuka ni rahisi kupata magonjwa hilo lipo wazi, ndio maana nikasema nimeshuhudia wenye magonjwa niliyoyataja hapo juu lakini sijashuhudia mwenye UKIMWI,

Labda nikuulize swali, UKIMWI ni Ugonjwa?
 
Sio ugonjwa
Hapana mpaka hapo nimeelewa ni nini unahitaji aisee iam sorry sina uwezo huo mkuu wa kukuonyesha mgonjwa mwenye maambukizi

Nje ya haki za wagonjwa.
 
Sio ugonjwa
Hapana mpaka hapo nimeelewa ni nini unahitaji aisee iam sorry sina uwezo huo mkuu wa kukuonyesha mgonjwa mwenye maambukizi

Nje ya haki za wagonjwa.
Kama sio Ugonjwa inakuaje watu wanameza dawa?

Hapana wewe twende taratibu tu utaelewa point yangu, nakukumbusha huko juu nimekuorodheshea aina za Magonjwa kama TB, KANSA, INI, HOMA YA INI, MOYO, MALARIA, PRESHA, n.k

Nikakwambia binafsi nimeona wenye hayo magonjwa ikiwemo mimi mwenyewe nishawahi kuugua Malaria, Kichwa, Homa, kwa hiyo naelewa ugonjwa ni nini lakini sijawahi kuona ugonjwa wa UKIMWI bali naona mtu anaumwa TB wanasema ana UKIMWI, anaharisha wanasema UKIMWI.....

Nipo tayari unieleweshe mtaalam.
 
Ni kweli UKIMWI sio ugonjwa ila ni upungufu wa kinga mwilini ambao moja kwa moja ni lazima ukupeleke kwenye kupata ushambuliwaji wa magonjwa nyemelezi kama uliyoyataja katika mifano yako anuwahi japo sio yote utayapata kutokana na upunguaji wa kinga mwilini mfano KANSA

Najua hapa point ambayo mimi na wewe bado tunapishana ni hapa kwenye UKIMWI ni ugonjwa au sio ugonjwa ukweli ni kuwa sio ugonjwa ila ni kama nilivyoeleza hapo awali .

Sasa kwanini utumie dawa ?
Dawa unatumia kujaribu kuraise up huo upungufu wa kinga mwilini.

Natanguliza shukrani [emoji120]
 
Now tumeanza kuelewana,
Kwanini nitumie madawa tena makali kupandisha Kinga zangu za Mwili wakati zinaweza kupandishwa kwa virutubisho vilivyopo kwenye chakula, kwa kuondoa msongo wa mawazo, kwa kufanya mazoezi, na mengine kama hayo ambayo nyie wataalam mnatuelekeza???

Huoni kama Dawa ndio zinazofanya kuzorotesha mwili wa muhusika?

Huyo mgonjwa wa Presha au Moyo yale madawa mwisho wake hua yanamfanya vibaya.....
 
Mkuu Dream Queen unajua ya kuwa mwisho wa kuwapa madawa bado wanashauriwa kutumiwa vyakula vyenye atleast mlo kamili yaani vyakula vinavyokuwa na virutubisho vya kutosha mwilini ?

Sasa embu twende nje ya taaluma kidogo
Ni mara ngapi umesikia kuna watu wanaishi na virusi ila bado hawajajijua ila wako fit tu ?

Basi iko hivi mara nyingi kinachomdhoofisha mgonjwa sio dawa ila ni mawazo na stress baada ya kuwa mwenye virusi hivyo maana wasio na stress hizo wapo salama na afya tele.

Kwanini dawa na sio vyakula kuraise kinga ?
Ndugu maisha ya mtanzania unayajua mlo kamili ni mtihani na uelewa wa vyakula vyenye mlo kamili bado ni mtihani .

Swali la kizushi
Toka asubuhi mpaka muda huu umekula matunda ?
Je ni rita ngapi za maji umekunywa ?
Jibu baki nalo.

Sitaki kukuaminisha wala kukubaliana na Wewe ati vyakula vyatosha kurudisha kinga
Kwanini nisikubaliane na wewe ?

Rafiki , kinga za mwili ukisema irudishwe kwa virutubisho vya chakula tutauwa watu wengi , kwanini ?

Sababu kinga zinakuwa zimeshuka sana kiasi ambacho sio rahisi kuzipandisha kwa hivi vyakula vyetu hata kama vina virutubisho .

Ila nakubaliana na wewe ikiwa mtu anatumia dawa basi akawa anakula vyakula vyenye virutubisho basi anaweza kuziacha kwa muda na asione madhara mapema kama kwa wale wenye lishe duni.

Asante , nahisi umenielewa .
Natanguliza shukrani [emoji120]
 

Hapana sijakuelewa hata kidogo,
Umesema UKIMWI sio Ugonjwa nikakuuliza kwanini Watu wanapewa Dawa na sio Virutubisho? Umejibu Dawa wanapewa lakini wanashauriwa wapate na Virutubisho bado tupo pale pale "Kama sio Ugonjwa kwanini wapewe Dawa!??"

Hoja ya kusema Watanzania hatufati Mlo kamili hii ina maana ya vipato vyetu na uelewa wa huo mlo kamili wenyewe, kwa hiyo Watanzania wengi tuna UKIMWI??? Je tukapange foleni kupandisha hizo kinga??

Bado tupo pale pale Mtu hana Ugonjwa kwanini atumie DAWA?? tujuavyo Dawa ni kwa ajili ya kutibu ugonjwa vipi huu Ukosefu wa Kinga Mwilini mtu apewe Dawa badala ya vitu vya kupandisha Kinga yake?? Umegusia kuhusu stress watu wengi tuna stress je tukipata stress kinga za mwili zikashuka basi tukimbilie kupanga foleni kupewa ARV???
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 yanachekesha ila kuna kitu hapo"""Pimaneni Jamani Kuacha ngono sio easy. Mimi hadi damu itaniishia, kila goli Moja tunapima Tena."""
 
Story hizi mtu utaacha mpaka yakupate.... 🤣🤣🤣🤣 Omba tuu uwe safe hivo ila mambo yapo oooh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…