Ex girlfriend wangu anaolewa lakini bado nampenda naombeni ushauri wenu

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,183
3,547
Licha ya sasa nina mpenzi mwingine ambae tunapendana Kwa dhati na ninampenda na Ananipenda tuu

Leo nimepata taarifa girlfriend wangu wa zamani ambaye tuliachana nikiwa bado nampenda, Na bado naendelea kumpenda baada ya kupewa taarifa na mtu
Wa karibu anaolewa roho inaniuma Sana yaani nashidwa kuvumilia

Natamani niende kufanya vurugu
Ukumbini
 
Licha ya sasa nina mpenzi mwingine ambae tunapendana Kwa dhati na ninampenda na
Ananipenda tuu

Leo nimepata taarifa girlfriend wangu wa zamani ambaye tuliachana nikiwa bado nampenda
Na bado naendelea kumpenda baada ya kupewa taarifa na mtu
Wa karibu anaolewa roho inaniuma
Sana yaani nashidwa kuvumilia

Natamani niende kufanya vurugu
Ukumbini
mwache aende futa kabisa mazoea naye vinginevyo utashikishwa ukuta
 
Kama ulikua unampenda Kwa nini mliachana... Mwache aolewe na usiende kutia fujo.... Ndo nyinyi wakati wa mahusiano mnajitia kiburiii Hamna cha maana mnachofanya ila ukisikia binti anaolewa unakuja kulialia...... Pambana na maumivu yako umeyataka mwenyewe
 
Kwanini ulimuacha wakati ulikuwa bado unampenda?tamaa itakuponza,acha tu roho ikuume, na huyo ulie naye pia muache uone wenzako wanavyojichukulia kiulaini,unajifanya selective ona sasa hata uliekua naye unaejifanya unampenda tayari umeshaanza kumuona bomu,nenda kafanye fujo uone kama hujaishia jela,mwenzio kashakufuta kwenye akili yake siku nyingi na anajutia hata kwanini alikosea kuwa na mtu kama wewe usiejielewa..
 
Usifanye vurugu ukumbini maana utapewa dozi ya kukutosha.

Njia rahisi kamteke kabla ya harusi, game over!!
 
Licha ya sasa nina mpenzi mwingine ambae tunapendana Kwa dhati na ninampenda na
Ananipenda tuu

Leo nimepata taarifa girlfriend wangu wa zamani ambaye tuliachana nikiwa bado nampenda
Na bado naendelea kumpenda baada ya kupewa taarifa na mtu
Wa karibu anaolewa roho inaniuma
Sana yaani nashidwa kuvumilia

Natamani niende kufanya vurugu
Ukumbini
Nenda kafanye vurugu tu usihofu lakini vaa kofia ngumu na makoti manne.
 
Nenda kafanye vurugu mkuu piga balimi zako za kutosha kavuruge hiyo ndoa ndo itapendeza zaidi WAHI KUFANYA HIYO FUJO
 
Unapaswa kumpenda anaekupenda asie kupenda muache aende zake, unamng'ang'ania kwani Mama yako huyo?
 
Vurugu ndio itakufanya uonekane mjinga zaidi....
mwanaume jikaze... unalia lia nini brother!! jifunze ku-Let go, Move on ,Let life hapen
 
Back
Top Bottom