EWURA yafafanua kutoshuka bei ya mafuta nchini

EWURA yafafanua kutoshuka bei ya mafuta nchini

Huku kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia kumeanza zaidi ya miezi miwili sasa. Lakini EWURA wamekuwa wagumu sana kushusha na hii inawezekana inatokana na hayo "ma capacity charge" yao kama ya Tanesco
 
Mafuta yatashuka mwezi March sasa hivi tunatumia mafuta ya mwezi November 2015

Kwa nini mkisikia mafuta kwenye soko la dunia yamepanda bei na nyie wakati huo huo mnapandisha.

Kwa nini sasa hivi mnahitaji muda kidogo upite ili muweze kushusha bei?
 
Kwenye kulinganisha bei, wanataja bei ya juu ya kigoma halafu bei ya chini watangaza bei ya chini ya Dar. Naona wako kiwizi zaidi hawa watu.
 
Huku kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia kumeanza zaidi ya miezi miwili sasa. Lakini EWURA wamekuwa wagumu sana kushusha na hii inawezekana inatokana na hayo "ma capacity charge" yao kama ya Tanesco
mkuu mafuta pia yananunuliwa kwa usd currency yetu against usd inaweza ikawa kikwazo pia bei isishuke
 
Linapokuja swala la kushusha bei ya mafuta mnatafuta sababu nyingi mno. Hata zilizopo chini ya uvungu mtazileta.

Pipa moja la mafuta limeshuka kutoka wastani wa USD 50 mpaka sasa hipo kwenye USD 30. Lakini amuishiwi sababu.
 
MAMLAKA ya Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia kutaendelea kushusha bei nchini.
Katika taarifa yake kwa umma, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi alisema, licha ya kushuka kwa bei hizo za mafuta katika soko la dunia, hazitakuwa zikishuka kwa wakati huo huo nchini.
“Kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia kutaendelea kushusha bei hapa nchini japo si kwa wakati huo,” Ngamlagosi alisema.
Ngamlagosi alisema kumekuwa na upotoshaji kwamba Ewura haishushi bei za mafuta kwa kuwa kushuka kwake kutaathiri mapato yake, lakini ukweli ni kwamba tozo ya Mamlaka hii inatokana na lita za mafuta na si bei.
“Iwapo Ewura ingetaka mapato mengi, basi ingeongeza wingi wa lita za mafuta yanayoingia hapa nchini, na si kutegemea kupanda kwa bei. Hivyo basi kushuka au kupanda kwa bei hakuna uhusiano wowote na ongezeko la tozo kwa Ewura,” alieleza.
Alisema, Mamlaka hiyo itaendelea kutimiza wajibu wake kisheria katika sekta ndogo ya mafuta hapa nchini, ikiwemo upangaji bei kikomo za mafuta na kuzisimamia katika maeneo yote nchini.
Mkurugenzi huyo alisema kwa mwaka huu, bei ya petroli ilishuka toka kiwango cha juu zaidi, Septemba 2014, Sh 2,267 kufikia Sh 1,898 kwa lita ikiwa ni kupunguka kwa Sh 369 kwa lita. Bei ya dizeli ilishuka toka kiwango cha juu zaidi, Aprili 2014, ilipokuwa ikiuzwa Sh 2,149 na kufikia Sh 1,747 kwa lita Januari 2016, hii ikiwa ni kupungua kwa Sh 402 kwa lita.
Bado maelezo haya hayajitoshelezi kama taarifa zilizoko hata huku jf kwamba pipa moja la mafuta limeshuka kwa zaidi ya Nusu ya bei ya zamani harafu kwetu inashuka sh.200kwa Lita.
Tunategemea kuyaona Mafuta yakishuka hadi kufikia sh.1200 kwa Lita. Walau kwa kuanzia.
 
Kwenye kulinganisha bei, wanataja bei ya juu ya kigoma halafu bei ya chini watangaza bei ya chini ya Dar. Naona wako kiwizi zaidi hawa watu.

Mkuu EWURA madarali wa wauza mafuta.

hiyo bei sijuwi yawapi? maana anaongea uwongo.
 
EWURA ni taasisi inayomilikiwa na wafanya biashara ya mafuta.
 
***** zenu shirika lenu lifutwe tu halina faida yoyote kwa sie watanzania wa vijinini, ni ushoga kupandisha bei ya mafuta ya taa kuliko petroli huku mkijua huku vijijini hatuna gesi wala umeme, yaani hayo majipu anayotumbua rais wetu kipenzi bado hatujaona faida yake huku vijijini
 
M
MAMLAKA ya Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia kutaendelea kushusha bei nchini.
Katika taarifa yake kwa umma, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi alisema, licha ya kushuka kwa bei hizo za mafuta katika soko la dunia, hazitakuwa zikishuka kwa wakati huo huo nchini.
“Kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia kutaendelea kushusha bei hapa nchini japo si kwa wakati huo,” Ngamlagosi alisema.
Ngamlagosi alisema kumekuwa na upotoshaji kwamba Ewura haishushi bei za mafuta kwa kuwa kushuka kwake kutaathiri mapato yake, lakini ukweli ni kwamba tozo ya Mamlaka hii inatokana na lita za mafuta na si bei.
“Iwapo Ewura ingetaka mapato mengi, basi ingeongeza wingi wa lita za mafuta yanayoingia hapa nchini, na si kutegemea kupanda kwa bei. Hivyo basi kushuka au kupanda kwa bei hakuna uhusiano wowote na ongezeko la tozo kwa Ewura,” alieleza.
Alisema, Mamlaka hiyo itaendelea kutimiza wajibu wake kisheria katika sekta ndogo ya mafuta hapa nchini, ikiwemo upangaji bei kikomo za mafuta na kuzisimamia katika maeneo yote nchini.
Mkurugenzi huyo alisema kwa mwaka huu, bei ya petroli ilishuka toka kiwango cha juu zaidi, Septemba 2014, Sh 2,267 kufikia Sh 1,898 kwa lita ikiwa ni kupunguka kwa Sh 369 kwa lita. Bei ya dizeli ilishuka toka kiwango cha juu zaidi, Aprili 2014, ilipokuwa ikiuzwa Sh 2,149 na kufikia Sh 1,747 kwa lita Januari 2016, hii ikiwa ni kupungua kwa Sh 402 kwa lita.

Mbona bei ya mafuta opec imeshuka kutoka $110 kwa pipa hadi $30 kwa pipa ?
 
Hawa ni wapumbavu tena sana tuu, wanaona watz ni wajinga wakudanganywa kama vile hawakwenda shule. Katika miezi 14 iliyopita bei ya mafuta imeshuka sana tuu karibia nusu ya bei ya zamani, sasa mbona ni zaidi ya miezi miwili na Hakuna tofauti kwa wateja.
 
Inabidi wenye magari wafanye maandamano wafunge bara bara mpaka kieleweke, jazeni magari barabarani halafu hao wajinga waje waeleze huu utumbo wanaoleza sasa hv.
 
Ndiyo mana kwangu mimi nimekuwa niki-kidifine hiki chombo kinachijiita EWURA Chombo kisichoaminika hata kwa 1%.... EWURA utendaji kazi wake umekuwa ukiniacha na bumbuwazi kwa miaka yote... Kipo pia na chombo kingine kinachitwa SUMATRA nacho ni pasua kichwa kiutendaji kwa 100%.
 
Hili la ewura ni jipu, Baba Magufuli tunaomba ulishughulikie mapema
 
Hawa jamaa ni majanga kila mtu anajua tangia mafuta yaanze kushuka bei (at $ 126 a barrel) na sasa yalipo bei ya soko la dunia imeporomoka kwa karibu asilimia 79% nchi zilizo sceptic kwamba iwapo yakipanda ghafla mafuta for whatever un-imagined reasons hizo nchi wameshuka kwa karibia asilimia 35% na sasa kunafaida za deflection that is the pessimistic view ambazo consumers wanafaidika and industries.

Wakati EWURA wao ndio kwanza wapo at 17% ya kushusha bei halafu wanataka waonekane wanafanya jitihada za kuwasaidia watanzania ambao wengi wao hela zenyewe za kuunga kuunga halafu anakuja mtu kama huyu kutuambia kuwa faida zao azipo affected based on price bali litres sales sasa nani asiejua hilo.

Tatizo la Tanzania ni uwezo, vyama vya siasa visivyo na watunga sera uwezi kuamini despite age ya Wassira ni mmoja ya watu wachache sana waliobaki kama vipanga wa CCM its about time tuwe na watu wenye uelewa kwenye siasa zetu sio huu upuuzi uliopo sasa wajinga tu na wapiga debe kuwa promoted wasio na maarifa yoyote; jumlisha na usalama wa taifa wa ovyo hivi kwanza utakuwa vipi afisa wa usalama wa nchi katika ngazi za juu wakati ata akili zenyewe auna; afisa wa usalama anatakiwa awe smart I know a lot ambao ni useless,
 
Kila ninapoiona NEMBO ya EWURA Mahali popote pale nashikwa na HASIRA... EWURA HAIJAWAHI KUFANYA KAZI HATA SIKU MOJA ILIYOWANUFAISHA WATANZANIA KWA UJUMLA HASA HUKU KWENYE MAFUTA AMINI USIAMINI KWA MIAKO YOTE HIYO.
 
Back
Top Bottom