Ewura cuts fuel prices by 27%

Nadhani kama sijasahau, kuna kituo kimoja cha mafuta pale kariakoo Kilijaribu kufungiwa kwa kuuza mafuta yaliyochanganywa lakini uwezo wa EWURA kusimamia maamuzi yake kisheria ni mdogo na kile kituo kinaendelea kuuza hayo mafuta mpaka kesho. Je kwa maamuzi haya tunadhani yataweza kutekelezeka?
 
Hehe! Nilishangaa hiyo nguvu ya kupanga bei wameitoa wapi, kumbe hakuna kitu!!
 
..muswada wa sheria itakayowapa 'meno' ya kudhibiti bei ya mafuta utapelekwa ktk kikao cha bunge mwezi huu au mwezi februari.

..nadhani TPDC pia wataruhusiwa kuagiza mafuta ili kuweza ku-stabilize supply.

NB:

..lawama nyingi zinapaswa kwenda kwa Bunge ambalo lina jukumu la kuandika sheria. EWURA ni watekelezaji tu.
 
..lawama nyingi zinapaswa kwenda kwa Bunge ambalo lina jukumu la kuandika sheria. EWURA ni watekelezaji tu.

Kama ndivyo Masebu alitoa wapi nguvu za kusema bei ni zile alizokokotoa na atayezidisha atatozwa faini na kunyang'anywa leseni ya baishara? Au ni mdomo wake ulikuwa unawasha? Haya basi, na je Waziri mwenyewe wa Nishati alivyoongea kwa hasira na makunyanzi kibao usoni jana usiku kwene taarifa ya habari tumweleweje?

Mimi nilisema naamini hii ni siasa kwa sababu hakuna haswa mwenye kusema na kutekeleza alilolisema, wanatuzungusha tu ili muda uende. Hata hivyo tunapenda kujua ni nini hatima ya viongozi wa taasisi na mashirika ya serikali au serikali yenyewe kubwabwaja hovyo hovyo?

Bei ziko palepale na leo Masebu ushahidi kuhusu siasa zao na serikali yetu, ati Masebu anasema yeye hana menu ya kuwauma wale waliozidisha bei. Siasa ni zilezile kwamba EWURA haina meno..!
 
akilimtindi,

..tatizo ni waandishi wa habari uchwara. ni gazeti moja tu ndiyo liliripoti kwamba sheria itakayowawezesha ewura kutekeleza amri ile itapitishwa na kikao kijacho cha bunge.

..lakini wa-Tanzania na sisi tunapenda mno kulalamika. hivi kwanini watu hawadai risiti kwenye hivyo vituo vya mafuta na kushtaki mahakamani.

..sisi ni nchi ya aina gani hatuna hata consumer advocates groups? tunauziwa nyanya mbovu, mchele mbovu, etc etc. halafu tunasubiri serikali ututetee.

NB:

..na katika sakata hii kwanini mbaya aonekane ewura na siyo hao wafanya biashara wanaorusha bei?
 
akilimtindi,

..tatizo ni waandishi wa habari uchwara. ni gazeti moja tu ndiyo liliripoti kwamba sheria itakayowawezesha ewura kutekeleza amri ile itapitishwa na kikao kijacho cha bunge.

..lakini wa-Tanzania na sisi tunapenda mno kulalamika. hivi kwanini watu hawadai risiti kwenye hivyo vituo vya mafuta na kushtaki mahakamani.

..sisi ni nchi ya aina gani hatuna hata consumer advocates groups? tunauziwa nyanya mbovu, mchele mbovu, etc etc. halafu tunasubiri serikali ututetee.

NB:

..na katika sakata hii kwanini mbaya aonekane ewura na siyo hao wafanya biashara wanaorusha bei?

EWURA hakuna kitu pale, wametangaza kuwa bei itashuka kuanzia Jumatatu na atakayepuuza atapewa faini ya 300 million!! Sasa zitashuka vipi kama sheria haijapitishwa bado? na sheria isipopita itakuaje?

Kilichotoke ni EWURA wamejaribu kuwapiga wafanyabishara mkwara, wao wakaputa, sasa EWURA wamenywea.

Mimi siwezi kuwalaumu wafanyabiashara sana, hii ndio capitalism, kama unaweza kuuza stock yote at 1600/litre kwanini waiuze at 1200/litre? Hiyo isingeleta maana kibiashara.
 
Hapa suala la msingi ni kuwa kulikuwa na sababu gani kwa EWURA kukurupuka kutangaza bei ambazo hawana uwezo wa kuzisimamia? Si wangefanya taratibu za kisheria kwanza halafu ndio watangaze? Mi naona kuna kitu zaidi ya siasa. Leo asubuhi nimesikia TV zikinukuu baadhi ya magazeti kwamba viongozi wakubwa serikalini wana hisa kwenye kampuni za kuagiza na kuuza mafuta (labda ni wakurugenzi pia) na kwamba ndio kikwazo cha utekelezaji wa agizo la EWURA. Je, hili ni kweli kwa kiasi gani? Tunaomba wenye taarifa wasaidie kutuhabarisha. Kwani hii inaweza ikawa vurugu kama za daladala Dar ambapo ilikuja kufahamika kuwa wamiliki wakubwa ni vigogo hadi ex-PM.
 
Wengi hatufahamu hizi bei zinaaza kutumika kuanzia siku gani kwani tarehe 05/01/09 imepita na hatuoni mabadiliko yoyote.
 
Hii serikali inakuwa kama wacheza mieleka! hakuna "team work" nilitegemea serikali ingejipanga nakutizama trend nzima ya fisco policy na national macro-economy strategy.

Wakati Ewura wakihangaika na waagizaji wa mafuta, Sumatra nao wangekuja na mkakati wa kushusha nauli, FCC waje na mkakati ya kushusha bei ya sukari na ngano, ikiwezekana Waziri Hawa na prof.Kapuya waje na mkakati wa kupunguza posho za safari.

Hatimae tungejikuta inflation nayo inashuka, kwamantiki hiyo impact ya unafuu wa maisha ingeonekana kwa mwananchi wa kawaida.

Baada ya hapo ndo prof.Ndullu angekuja na monetary masterplan.
 
Hii serikali inakuwa kama wacheza mieleka! hakuna "team work" nilitegemea serikali ingejipanga nakutizama trend nzima ya fisco policy na national macro-economy strategy.

Wakati Ewura wakihangaika na waagizaji wa mafuta, Sumatra nao wangekuja na mkakati wa kushusha nauli, FCC waje na mkakati ya kushusha bei ya sukari na ngano, ikiwezekana Waziri Hawa na prof.Kapuya waje na mkakati wa kupunguza posho za safari.

Hatimae tungejikuta inflation nayo inashuka, kwamantiki hiyo impact ya unafuu wa maisha ingeonekana kwa mwananchi wa kawaida.

Baada ya hapo ndo prof.Ndullu angekuja na monetary masterplan.
Kwa hiyo tuachane na free market kabisa?
 
bei zimepangwa na EWURA regardless ya kama kampuni ina stock iliyonunua kwa bei ya juu na hivyo ikiuza kwa bei za EWURA inapata hasara.Swali: EWURA itatoa compensation kwa kampuni hizo baada ya kuhakiki documents za importation?
Mkulu swali la muhimu sana hilo.
 
..muswada wa sheria itakayowapa 'meno' ya kudhibiti bei ya mafuta utapelekwa ktk kikao cha bunge mwezi huu au mwezi februari.

..nadhani TPDC pia wataruhusiwa kuagiza mafuta ili kuweza ku-stabilize supply.

NB:

..lawama nyingi zinapaswa kwenda kwa Bunge ambalo lina jukumu la kuandika sheria. EWURA ni watekelezaji tu.
Ni aibu unapokuwa na chombo so-called Regulatory Authority wakati hawana uwezo wa kisheria wa kusimamia maamuzi yake kisheria.Ukiuliza unaelezwa kuna muswada unapelekwa bunge kuipa EWURA " meno " . Then hiyo sheria ya kuanzisha EWURA in the first place walikimbilia kuipitisha kwa malengo gani?.DUH... HII INATOKEA TZ TU.
 
Nchi za kiarabu kwa muda mrefu zilikuwa zikitumia mafuta kama kombora lao la kivita.Miaka ya nyuma walikuwa wakitumia mafuta kugomea kuwauzia mafuta wale ambao hawataki kuwaunga mkono waarabu au wapalestina au wale ambao walikuwa na uhusiano wa Kibalozi na Israeli.Ilikuwa ukikataa kuwaunga mkono wanakunyima mafuta.

Tanzania chini ya Nyerere ilijikuta ikilazimika kuvunja uhusiano na Israeli kwa shingo upande kwa kulazimishwa ili iweze kuendelea kupata mafuta toka nchi za kiarabu.Ndiyo maana kipindi kile Nyerere akajifanya kinara wa kuunga mkono wapalestina na kundi lao la PLO.

Mapesa ya mafuta toka uarabuni pia yamekuwa yakituhumiwa kutumika kufandhili makundi ya magaidi kama Hamas,hizbollah,n.k katika nchi mbalimbali na makundi yaliyolipua Trade centre marekani, balozi mbalimbali za Marekani na mataifa mengine,n.k Pia mapesa hayo ya mafuta yamekuwa yakitumika kugharimia vikundi vyenye imani za itikadi kali vinavyoleta shida na mauaji katika nchi mbalimbali dunian ikiwemo Pakstani,Bali,uarabuni,Misri,Africa,n.k

Ili kupambana na vita ya kutumia mafuta mbinu kadhaa zimebuniwa na makomandoo wa vita za uraiani zisizohusisha vita za silaha za moto.Mojawapo ya silaha hiyo ni kuhakikisha kuwa mafuta yanatafutiwa teknolojia mbadala ili kuyafanya yasiendelee kuwa na soko na kupunguza jeuri ya waarabu kuitumia silaha hiyo.Baaddhi ya Mbinu hizo ni kama:

(a) Ugunduzi huo ni pamoja na kutumia mimea mbalimbali ya kuzalisha mafuta ikiwemo mbono,n.k

(b) Pia magari na mitambo ya viwanda kutengenezwa inayotumia gesi ambayo tayari imeshaanza kufanya kazi hata Tanzania viwanda vimeanza kutumia gesi badala ya songosongo badala mafuta ya waarabu.Magari mengi muda si mrefu yatakuwa yakitumia gesi zaidi badala ya mafuta ya waarabu

(c) Kuachilia teknolojia ya ugunduzi wa mafuta holela ili kila nchi iweze kufanya utafiti wake na kuona kama inayo mafuta na ikiyaona iweze kuyachimba na kuacha kutegemea waarabu.Tanzania na hata Pemba mafuta yapo nadhani muda si mrefu hatutakuwa na la kujikomba kwa waarabu tutawaachia mafuta yao wayanywe wakitaka kwani tutachimba yetu.

(d) Nchi kubwa kama marekani N.K kuacha kuagiza mafuta kutoka uarabuni na kuanza kutumia reserve zake na kuchimba yake kumeleta pigo kubwa la ajabu kwa waarabu ambalo limesababisha bei ya mafuta kuporomoka kwa kasi ya kutisha hadi Tanzania.Bush kawashikisha adabu waarabu Marekani mnunuzi mkubwa wa mafuta kawapiga chini sasa waarabu wako tayari kuuza kwa bei ya kutupwa mafuta yao na bei yao itaendelea kuporomoka .Wauza mafuta wameanza kugeuka kama machinga wanahaha kusaka soko kuuza mafuta popote kwa bei za kutupwa.Mapipa na mapipa yameanza kujazana kwenye maghala yao bila wanunuzi.

Vita hii ya mafuta ni kali. Inavyoelekea miaka michache ijayo Uarabuni litakuwa bara maskini kuliko yote.Watakuwa maskini kuliko hata bara la Afrika sababu wao hawalimi,hawajaendelea kiviwanda,teknologia wala madini. Tegemeo lao ni silaha ya mafuta tu ambayo sasa inapigwa makombora ya nguvu kuisambaratisha silaha hiyo

Muda si mrefu waarabu wataiheshimu Afrika na watakuja na bakuli la kuomba kama la omba omba Matonya yule ombaomba maarufu kuja kutuomba misaada tuwasaidie walau chakula wale.

Watanzania tujipange tuimarishe na kuijali sekta ya madini,kilimo na viwanda tutafika mbali sana muda si mrefu tukichachamaa na viongozi wakijipanga vizuri kujali maslahi ya nchi na wananchi ili raslimali zilizopo zisimamiwe vizuri kwa maslahi ya wananchi tutafika mbali.

Mafuta ya waarabu ni bomu ambalo halitakuwa na nguvu yoyote ya kumtisha yeyote muda wa miaka michache tu ijayo.Tanzania tutakuwa huru hata twaweza kulala na kuamuka TEL AVIV ISRAEL bila kuogopa muuza kombora la mafuta mwarabu anasemaje au anatuwazia nini kwa sababu atakuwa muuza kombora lisilolipuka lisiloweza kulipua hata inzi mdogo.
 
Oil dealers give in

2009-01-10 11:30:53
By Angel Navuri and Correspondent Njonanje Samwel​

Pump prices were down by more than 16 per cent in most petrol stations in Dar es Salaam yesterday as the government continued to blacklist filling stations which are reluctant to lower the prices.

In most filling stations in Dar es Salaam, petrol was being sold at 1,230/- per litre down from 1,450 to 1,500/-, while diesel was being sold at 1,200/- per litre from 1,350/- to 1,450/-.

Motorists woke up yesterday to find lower prices on billboards of most filling stations.

``It was a surprise to me when yesterday morning I found prices to have been lowered because on Thursday night the prices were still high. This is good,`` said Ali Issa a daladala driver.

Some few filling stations, however, were still selling fuel at higher prices.

The government early this week issued indicative pump prices and ordered all filling stations in the country to abide by the new prices.

It said that it would never be driven by investors who wanted to reap windfall profits from the oil business by giving government and people`s interests a second priority.

The Minister for Energy and Minerals, William Ngeleja gave the government\'s stance when commenting on the on-going oil pricing tug of war between Ewura and oil companies.

He said there was no basis for oil prices in Tanzania to be higher than those of other countries, adding that, that was a distortion of the facts.

The Energy and Water Utilities Regulatory Authority (Ewura)`s indicative and cap prices released this week set the price of petrol down by around 400/- per litre, an almost 30 per cent drop from the old price, while that of diesel goes down by 300/- per litre and kerosene by around 15/-.

Indicative and cap prices announced by Ewura for Dar es Salaam are supposed to be petrol 1,166/-, diesel 1,271/- and 814/- for kerosene.

Indicative and cap prices for Petrol announced by Ewura for upcountry zones are as follows: Arusha 1,262/-, Dodoma 1,235/-, Iringa 1,251/-, Bukoba 1,423/-, Kigoma 1,423/-, Moshi 1,244/-, Lindi 1,262/-, Mbeya1,269/-, Musoma 1,406/-, Babati 1,282/-, Morogoro 1,204/-, Mwanza 1,375/-, Mtwara 1,246/-, Kibaha 1,196/-, Sumbawanga 1,309/-, Songea 1,284/-, Singida 1,298/-, Tabora 1,298/- and Tanga 1,235/-. Price for Diesel: Arusha 1,367/-, Dodoma 1,340/-, Iringa 1,356/-, Bukoba 1,528/-, Kigoma 1,528/-, Moshi 1,349/-, Lindi 1,367/-, Mbeya 1,374/-, Musoma 1,511/-, Babati 1,387/-, Morogoro 1,309/-,Mwanza 1,480/-, Mtwara 1,351/-, Kibaha 1,301/-, Sumbawanga 1,413/-, Songea 1,388/-, Singida 1,358/-, Shinyanga 1,403/-, Tabora 1,402/- and Tanga 1,340/-.

Kerosene supposed to be: Arusha 910/-, Dodoma 883/-, Iringa 899/-, Bukoba 1,071/-, Kigoma 1,071/-, Moshi 892/-, Lindi 910/-, Mbeya 917/-, Musoma 1,054/-, Babati 930/-, Morogoro 852/-, Mwanza 1,023/-, Mtwara 894/-, Kibaha 844/-, Sumbawanga 957/-, Songea 932/-, Singida 901/-, Shinyanga 946/-, Tabora 946/- and Tanga 883/-.

At first, however, oil dealers refused to lower the price saying they would only do so after the indicative prices have been gazetted.

But yesterday, Ewura Director General Haruna Masebu said the indicative prices have been gazetted and that filling stations which would not abide by the set prices would be dealt with.

The Secretary General of the Tanzania Association of Oil Marketing Companies Salum Bisarara confirmed yesterday that they had been issued with a copy of the government Gazette regarding the issue.

He said with the official notice in place prices of oil would now go down.

He said oil dealers who will defy the government order would face justice without sympathy because they have been given enough time to adjust to the new pricing system.

Masebu said yesterday that they had been recording those oil stations that have not yet obeyed the indicative price and that they will face charges soon.

While prices in Dar es Salaam have gone down, upcountry pump prices have not changed much.

With the exception of Iringa and Singida regions where petrol is now sold at 1,325/- and 1,320/- respectively from 1500/- and diesel 1300/- from 1,450/- most filling stations in the other regions sold petrol at between 1,450/- and 1,500/- and diesel at 1,400/ to 1,450/-

SOURCE: Guardian
 
Wakuu leo nimepita katika vituo kadhaa vya kuuzia mafuta.....ila hakuna mafuta, kuanzia BP (Patco Shekilango), Total (Shekilango/Morogoro road), BP (Kimara)......hakuna mafuta (nilikua natafuta petrol).
Inaelekea kuna mgomo baridi wa wauzaji wa mafuta....sijui hili serikali inalichuliaje.
 
Wadau hivi hili suala limeishia wapi????

Bei za mafuta sasa zikoje??????

Je uhaba kwenye vituo vya mafuta umeisha?????
 
Back
Top Bottom