Evodius Mtawala aachia ngazi TFF

Evodius Mtawala aachia ngazi TFF

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
attachment.php

Evodius Mtawala ameachia ngazi ya ukurugenzi wa sheria na wanachama wa shirikisho la mpira wa miguu nchini -TFF, Taarifa kutoka ndani ya shirikisho hilo zinasema katibu mkuu huyo wa zamani wa Simba SC zinasema ukilitimba uliokithili ndani ya shirikisho hilo ikiwa ni pamoja na miundo mbinu mibovu ya utendaji ndani ya TFF ndio chanzo cha mwanasheria huyo kuamua kujiweka pembeni.

==============

Mkurugenzi wa wa Vyama na Masuala ya Kisheria katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Evodius Mtawala, amelazimika kuachia ngazi kutokana na sababu mbalimbali.

Taarifa ambazo tumezipata, zinaeleza kuwa Mtawala ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Simba, alikuwa na hali ya kutokuelewana na uongozi wa shirikisho hilo na ndiyo chanzo kikubwa cha kumfanya ang'atuke TFF.

Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa, alithibitisha kuachia ngazi kwa Mtawala lakini akasema ni kutokana na sababu mbalimbali za taaluma yake ya uanasheria.

"Ni kweli Mtawala hataendelea kufanya kazi TFF lakini ameamua kuchia ngazi mwenyewe kutokana na sababu mbalimbali alizodai kwamba ni kujikita na taaluma yake zaidi kwa sasa, lakini mambo mengine juu ya hilo yatabaki kuwa siri baina yake na mwajiri wake.

"Ila mpaka makubaliano ya mwisho yalieleza kuwa itakapofika mwisho wa mwezi wa nane (jana 31, Agosti) atakuwa tayari ameshakabidhi ofisi na kuendelea na masuala ambayo alidai anahitaji kujikita zaidi kulingana na taaluma yake," alisema Mwesigwa.

Mtawala amedumu kwenye wadhifa huo kwa miezi nane tu tangu alipoteuliwa Desemba 24, mwaka jana chini ya uongozi wa rais mpya, Jamal Malinzi.

Chanzo: Saleh Jembe
 
Attachments

  • mtawala.JPG
    mtawala.JPG
    21.3 KB · Views: 1,089
Wakuu, hivi yale magari yaliyochukuliwa na madalali yamerudi?
 
hakupewa ofisi,kompyuta na usafiri ama miundombinu gani hasa kwa maana ya ukosefu wa miundombinu? tiririka mkuu.
 
Ubarikiwe kwa kuliona hilo japo ungetoa suluhisho la nn kifanyike ili soka letu lipande juu
 
Kwa hiyo solution ya ukosefu wa miundombinu ni kukaa pembeni?

Lazima Kuna matatizo kibao tu hajayaweka wazi.

Au ndo"if you can't face it,give it your back"
 
Evodius Mtawala ameachia ngazi ya ukurugenzi wa sheria na wanachama wa shirikisho la mpira wa miguu nchini -TFF, Taarifa kutoka ndani ya shirikisho hilo zinasema katibu mkuu huyo wa zamani wa Simba SC zinasema ukilitimba uliokithili ndani ya shirikisho hilo ikiwa ni pamoja na miundo mbinu mibovu ya utendaji ndani ya TFF ndio chanzo cha mwanasheria huyo kuamua kujiweka pembeni.
hapo kwenye underline kuna maswali, ni majuzi tu nimesikia kitu ambacho sikuwahi kukijua hapa kabla, kuwa TFF ya uongozi uliopita ilikuwa ikipanga PPF Tower (???) na hii ya sasa wameamua kuiachia hiyo ofisi na kurudi 'nyumbani' yaani uwanja wa Karume. Je, hii habari ni kweli au nilisikia vibaya!?
Kama ni kweli basi ni wazi watu wengi wanaweza kuikimbia TFF kwa maana inaelekea palikuwa ni michongo ya ulaji. Utawezaje kupanga ofisi za kifahari kwa kutegemea pesa za FIFA huku mpira kwenye ground ukiwa hoi!? Sio ajabu hata tickets zilikuwa zikichapishwa kiujanjaujanja kitu kilichopelekea magari ya TFF kukamatwa na madalali.
Kwa kifupi ni kuwa hata mwanasheria anaweza kuachia ngazi kama mawazo yake yalikuwa ni ya ki-TFF iliyopita.

Mkuu Chachu Ombara, kwanini imekuwa ghafla hivyo. Kulikuwa na dalili zozote za huyu bwana kuachia ngazi?
Tupe na chanzo cha habari yako kama hutajali.
 
Last edited by a moderator:
Sijapata kufuatilia kwa undani zaidi ila ukweli kaachia ngazi,nimeonana na ndugu yake wa karibu kanithibitishia hilo.Pia suala jingine alilosema ni kuhusu usajili wa Okwi kwa jinsi ulivyogubikwa na sintofahamu.
 
Suala la Okwi bado halijajadiliwa, anaachiaje ngazi?! Lazma kuna sababu nyngne na si Okwi.
 
Suala la Okwi bado halijajadiliwa, anaachiaje ngazi?! Lazma kuna sababu nyngne na si Okwi.
Huwezi kukataa moja kwa moja. Inawezekana Simba wamewekeza matumaini yao kwake juu ya swala hili, naye anahisi ni mzigo mkubwa kwake. Kuliko kusubiri lawama, huenda ameona ni vyema kujiondoa.
inawezekana pia kwamba anahisi Simba haitendewi au haitatendwa haki kwenye swala hilo, na kwa hivyo hataki kuhesabika kama Mwanasimba aliyechangia kuiuma Simba.
Mtu unalazimika kuamini hivyo kwa sababu kabla ya hapo hatkupata kumsikia akilalamikia uendeshaji ndani ya TFF. Tulichosikia ni wafanyakazi kulia njaa kwa kukosa mishahara. Lakini hili si miongoni mwa sababu alizozitaja za kuondoka kwake.
 
by omujubi;
hapo kwenye underline kuna maswali, ni majuzi tu nimesikia kitu ambacho sikuwahi kukijua hapa kabla, kuwa TFF ya uongozi uliopita ilikuwa ikipanga PPF Tower (???) na hii ya sasa wameamua kuiachia hiyo ofisi na kurudi 'nyumbani' yaani uwanja wa Karume. Je, hii habari ni kweli au nilisikia vibaya!?
Kama ni kweli basi ni wazi watu wengi wanaweza kuikimbia TFF kwa maana inaelekea palikuwa ni michongo ya ulaji. Utawezaje kupanga ofisi za kifahari kwa kutegemea pesa za FIFA huku mpira kwenye ground ukiwa hoi!? Sio ajabu hata tickets zilikuwa zikichapishwa kiujanjaujanja kitu kilichopelekea magari ya TFF kukamatwa na madalali.
Kwa kifupi ni kuwa hata mwanasheria anaweza kuachia ngazi kama mawazo yake yalikuwa ni ya ki-TFF iliyopita.

Mkuu omujubi hapo penye red ni kinyume chake!

yaani tff ya sasa ya huyu nshomile ndio iliyoenda kupanga ppf tower kwa kisingizio kuwa ofisi za karume hazina hadhi yao....si unajua tena sisi tuliosoma saaaana tulivyo?
 
Last edited by a moderator:
ameangalia kashfa ya okwi aliona alimdanganya kuwa yanga wavunja mkataba kumbe sivyo
 
Huwezi kukataa moja kwa moja. Inawezekana Simba wamewekeza matumaini yao kwake juu ya swala hili, naye anahisi ni mzigo mkubwa kwake. Kuliko kusubiri lawama, huenda ameona ni vyema kujiondoa.
inawezekana pia kwamba anahisi Simba haitendewi au haitatendwa haki kwenye swala hilo, na kwa hivyo hataki kuhesabika kama Mwanasimba aliyechangia kuiuma Simba.
Mtu unalazimika kuamini hivyo kwa sababu kabla ya hapo hatkupata kumsikia akilalamikia uendeshaji ndani ya TFF. Tulichosikia ni wafanyakazi kulia njaa kwa kukosa mishahara. Lakini hili si miongoni mwa sababu alizozitaja za kuondoka kwake.

Kwahiyo unahisi kuondoka kwake, kunaashiria Simba imekula kwao kwenye usajili wa Okwi?
 
anakimbia issue ya okwi huyo imekaa vibaya................
 
Bwana Evodius Mtawala hadi ninaandika post hii ni mfanyakazi wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania na anaendelea na wadhifa wake wa Mkurugenzi wa sheria na vyama wanachama.

Wewe ndiye au ni mtu anatumia id ya raisi
 
Jamal Malinzi, Itanichukua muda kuamini maneno yako,habari hizi nimethibitishiwa na ndugu yake wa karibu ambaye ni rafiki yangu pia.Ni bora kuweka wazi suala hili kuliko kuendelea kukumbatia uongo.
 
Last edited by a moderator:
Jamal Malinzi, Itanichukua muda kuamini maneno yako,habari hizi nimethibitishiwa na ndugu yake wa karibu ambaye ni rafiki yangu pia.Ni bora kuweka wazi suala hili kuliko kuendelea kukumbatia uongo.
Kaka unabishana na Muajiri wake? unaamini maneno ya rafiki yako?mmmmh pole sana.
 
Back
Top Bottom