Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 10,509
- 16,734
Aliyekuwa Rais wa Bolivia Bw. Evo Morales amerudi nchini mwake Bolivia baada ya kulazimika kukimbia mwishoni mwa mwaka jana.
Kiongozi huyo mwenye roho ngumu ya upinzani alitokana na makabila ya kijadi ya kaskazini ya nchi hiyo maarufu kwa kilimo cha cocoa.
Katika kipindi cha miaka 14 ya uongozi wake nchi hiyo ilipata mafanikio makubwa sana ya kiuchumi na ilijenga uhasama mkubwa na taifa la Marekani.
Kurudi kwake nchini humo kumekuja wakati mmoja na kumalizika uchaguzi wa Marekani na kushindwa kwa bw.Trump aliyekuwa daima akikwaruzana naye katika masuala ya kisiasa.
Rais wa Argentina, Alberto Fernandez alimfanyia hafla ya kumuaga bw.Morales muda mfupi kabla ya kuvuka mpaka na kuingia Bolivia atakakopokelewa na kiongozi mpya rafiki yake aliyeapishwa kushika madaraka nchini humo hivi karibuni.