Jamani, maada hii si kuhusu Maximo, bali mwajiri wa Maximo. Nimemtumia Maximo kama mfano mwingine wa kuonyesha ni jinsi gani mwajiri wake anavyoridhishwa na ukawaida wa kila kitu.
Mwajiri wa Maximo anamlipa Maximo na waajiriwa wengine wengi ambao ni Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Taasisi, Mabalozi, lakini hakuna Ufanisi au mafanikio ya kweli.
Imebakia ni vipodozi na kauli za mwajiri kuwa ana imani nzuri na aliowaajiri.
Je mmesahau alitoa kauli gani kuhusiana na Lowassa?