Kwa takribani miaka 2 kabla ya kuanza kampeni za uchaguzi mwaka 2015, nilikuwa napata nakala ya kila wiki ya RaiaMwema. Huwa wanaweka makala zao kwenye mtandao siku kadhaa ya baada ya gazeti kutoka, lakini bado nilikuwa nanunua gazeti hilo ili kuonyesha shukrani kwa makala zao nzuri. Hivyo 'tone' yao ilivyobadilika nilitambua kirahisi. Kuna makahaba jana yalibisha, lakini leo mmoja wa waandishi waliobadilisha 'tone' ya gazeti kakiri hadharani kuwa waliiandika habari 'nzuri' za CCM. Ni matumaini yangu hata ndugu yetu Mwanakijiji akili zitamrudia maana nae hawezi kuenea kwenye 'chupa' kwa muda mrefu.
Ndugu zangu, wengine tunachokipigania ni kikubwa kuliko Lowassa, Mbowe, Sumaye wala Dr. Slaa. Hatuna shida na rais wa sasa na tunapenda afanikiwe ktk mikakati yake, kushinda kwake ndo kushinda kwetu. Kikubwa ni kwamba tunahitaji mageuzi makubwa nchini mwetu, mageuzi ya kukata matawi. Mageuzi hayo hayawezi kuletwa na watu walioyakalia matawi hayo. That is the least we can do for our descendants.