Euro 2020: Upigaji wa penati ni tatizo. Mpaka sasa zimetolewa penati 11 na zaidi ya nusu goli halikufungwa!

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,663
18,037
Mpaka sasa kuna penati 11 zimetolewa, lakini upigani wa penati bado ni tatizo sugu!! Zaidi ya nusu ya penati hizo hazikufungwa. Tatizoni nini? Je kikwazo ni umahiri wa magolikipa au ni mbinu mbovu za wapigaji wa penati? tujadili! Ukiangalia jkubwa wa majina ya wapiga penati usingetazamia wengi wakose kiasi hicho!! Siku hizi kupata penati hakukuhakikishii kufunga goli!! bado ni hamsini kwa hamsini au bado ni patapotea! Wanakwama wapi? Tatizo ni nini? Tujadili.
Lakini cha kushangaza ni kuwa wakati kwa wengine kufunga penati ni kama pata potea kwa Ronaldo mambo ni tofauti kabisa!! Kwake penalt = goal!! Anawazidi kipi wenzake? Katika mashindano haya kwa wengine tumeona 8 penalties=2 goals lakini kwa Ronaldo 3 penalties=3 goals!!
Mkeka mzima wa penati mpaka sasa Euro 2020 huu hapa:
  • Pierre-Emile Hojbjerg (missed) - DENMARK vs Finland
  • Cristiano Ronaldo (scored) - PORTUGAL vs Hungary
  • Gareth Bale (missed) - WALES vs Turkey
  • Ezgjan Alioski (missed) - NORTH MACEDONIA vs Ukraine
  • Ruslan Malinovskiy (missed) - UKRAINE vs North Macedonia
  • Memphis Depay (scored) - HOLLAND vs Austria
  • Emil Forsberg (scored) - SWEDEN vs Slovakia
  • Patrik Schick (scored) - CZECH REPUBLIC vs Croatia
  • Gerard Moreno (missed) - SPAIN vs Poland
  • Artem Dyzuba (scored) - RUSSIA vs Denmark
  • Alvaro Morata (missed) - SPAIN vs Slovakia

Karibuni tujadili. Wachambuzi mliomo humu jamvini tunawategemea sana kwenye mjadala huu wa tatizo la kufunga penati.​

Penalty ni ngumu sana kufunga ndo maana hata wanaombeza CR7 akifunga penalty mim nawashangaa maana kuna wachezaji kibao wanakosa penalty ambazo yey anafunga
 
Halafu mtu anapopiga penati unamwona kabisa hana amani! Anamwona kipa amejaa golini!! Anaona goli limekuwa jembamba!!
 
Penaldo ndo maana anawazidi wenzie
Hakosi penalty..

Morata bure kabisa..kakosa mbili hadi sasa..
 
Hata penalty inakanunu zake mkuu za kupiga
Bahati mbaya au nzuri wachezaji karibu wote wamewahi kukosa penati tena kwenye mechi muhimu. Cristiano - man utd vs chelsea UCL final.messi nae kakosa sana.

Hakuna kanuni, ni utundu na mazoezi. Mfano zile panenka za pirlo au ramos ni utundu na kubahatisha. Rejea panenka ya arguero juzi juzi hapa ilibuma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama umewahi kucheza mpira hizi ligi ndogo ndogo tu utajua penati ipo vipi.asilimia 90 makipa wanabahatisha upande wa kuruka na siyo kupotezwa na mpigaji.ila hao asilimia kumi tu ndiyo wale ambao anakaa mpaka mwisho anaangalia mpira unaenda wapi.kwa mpigaji pia analiona goli dogo.ila pia kama shule za mpira unafundishwa penati ipige pembeni tena juu kwa sababu asilimia hizo 90% za makipa wanaotea upande wanaojua wao huwa ni chini na siyo juu na ndiyo maana kipa unamuona anaelekea upande mwengine mpira unaenda kwengine ila kule anapojirusha siyo juu ni chini.penati ya kati kati ubaya wake mpira unaweza kukutana na kipa wakati ananyoosha miguu kuruka upande mwengine.kwa hiyo ukipiga pembeni halafu iwe chini inabidi mpira wako uwe na kasi zaidi ya kipa pia.kipa akiruka huwa anajinyoosha mikono na miguu kwa hiyo kuna uwezekano pia mara nyengine hata kwa kidole tu akauelekeza nje na kama ukiwa na kasi tena ndiyo anaugusi ila kwa nguvu ya mpira anashindwa kuuokoa.kwa hizi penati ambazo sasa zinapatikana kwa njia ya madhambi uwanjani kwa kipa unashauriwa kama unapangua upangue mpira uende nje yaani kona kuliko ujaribu kuudaka na ile kasi ukahsindwa wapinzani wakaja kumalizia.ila zile penati za mchezo kuamuliwa kwa njia za penati kwa sababu timu mbili zimeshindwa kufungana kipa unashauriwa uupangue kuelekea popote mradi usirudi tena wavuni kwa sababu mpigaji haruhusiwi kuucheza mara ya pili.
 
Pembeni napo ni risk vile vile,kumbuka kuna kugongesha mwamba au kutoa nje,juu kuna kugongesha mwamba au kupaisha,kukosa penati sio lazima kipa aokoe.

Mazoezi ,mazoezi ndio jambo la msingi sana,hata karim benzema jana amesema kwenye intavyuu baada ya mchezo kwamba hata alipookita mpira kwenda kuuweka kwenye doti ya penati hakuwa na wasiwasi,kwasababu ya mazoezi ya mara kwa mara.
Mimi nakataa, penati haina kanuni,na unaweza kuipiga popote ukafunga au kukosa.
Unazijua panenka wewe? Unampigia kipa pale pale aliposimama matokeo yake yeye kipa ndio anaukimbia mpira
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zidane anapiga penati vizur na kila siku anapiga kwa style tofauti.
 
Pembeni napo ni risk vile vile,kumbuka kuna kugongesha mwamba au kutoa nje,juu kuna kugongesha mwamba au kupaisha,kukosa penati sio lazima kipa aokoe.

Mazoezi ,mazoezi ndio jambo la msingi sana,hata karim benzema jana amesema kwenye intavyuu baada ya mchezo kwamba hata alipookita mpira kwenda kuuweka kwenye doti ya penati hakuwa na wasiwasi,kwasababu ya mazoezi ya mara kwa mara.
Mimi nakataa, penati haina kanuni,na unaweza kuipiga popote ukafunga au kukosa.
Unazijua panenka wewe? Unampigia kipa pale pale aliposimama matokeo yake yeye kipa ndio anaukimbia mpira
Sent using Jamii Forums mobile app
Jambo kubwa kwa mpigaji penati ni utulivu asiwe mwenye presha
 
Huo utulivu unatokana na mazoezi ya kuzipiga hizo penati,presha ya mchezo n.k
Kuna kipindi hata messi pamoja na ubora wake presha ya mchezo huwa inaathiri utulivu na kujiamini kwake.
Kitu kingine kinachowapa presha,imejengeka kwamba kila penati basi lazima iwe goli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo utulivu unatokana na mazoezi ya kuzipiga hizo penati,presha ya mchezo n.k
Kuna kipindi hata messi pamoja na ubora wake presha ya mchezo huwa inaathiri utulivu na kujiamini kwake.
Kitu kingine kinachowapa presha,imejengeka kwamba kila penati basi lazima iwe goli.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unataka kusema kuwa hao wachezaji wakubwa wanaokosa penati huwa hawafanyagi mazoezi ya upigaji wa penati?
 
Kama umewahi kucheza mpira hizi ligi ndogo ndogo tu utajua penati ipo vipi.asilimia 90 makipa wanabahatisha upande wa kuruka

Kuna mchawi mmoja wa penati anaitwa Pirlo wa Italy aliposimama kipa ndo mpira unapita hapohapo wakati huo kipa kesharuka kulia au kushoto.
Nakubaliana na wewe kwenye penati kuna ufundi wa kupiga.
 
Huwa napendaga penalti za akina Salah na David Luiz upigaji wao ni kwa kutumia nguvu kipa akikutana nao lazima kasi yake imshinde bila kumsahau Milner na mwamba wa zamani wa Kijerumani Michael Ballack
 
Back
Top Bottom