lucley
JF-Expert Member
- Jun 15, 2016
- 728
- 2,012
Wiki sasa zimepita tangu tuondokewe na baba yetu kipenzi, bado siamini kama sitaweza kukuona tena maishani ingawa najitahidi kumuomba Mwenyezi mungu anijaalie subra na aniepushe na kufuru hususani katika wwakati huu wa majonzi.
Nakushukuru kwa malezi yote uliyonipa, na namna ulivyoniandaa kuishi ki-ume na kwa kupambana bila kutegemea cha kuomba, na daima nimtumainie allah kwani yeye ndiye mpaji na m-bora wa wapangaji. Maisha bila uwepo wako siyo rahisi hata kidogo, mazoea bado yanatutesa na simanzi hurudi upya kila tuwapo karibu na kumbukumbu zako.
Nakumbuka wosia wako, nitatilia maanani mengi tuliyoyazungumza katika siku za mwisho za uhai wako na pia nitatimiza ombi lako la kuwa nisiache kukuombea dua kwa Mwenyezi mungu akupe wepesi katika hali yoyote utakayokuwa nayo.
Nitajitahidi kufuata mienendo yako, uchapakazi, ucha mungu, uadilifu, upendo na zaidi ni siha nzuri iliyokufanya uwe kipenzi cha jamii yetu iliyotuzunguka. Kuna wakati katika uhai wako tuliona ni kama unatutesa kwa ukali wa mafunzo yako, ila sasa tutaona maana halisi ya maandalizi uliyokuwa ukitupa.
Kumbukumbu zako daima nitazienzi, na kumbukumbu bora zaidi ulizoniacha nazo ni namna ulivyopambana kuhakikisha natambua umuhimu wa elimu. Nakumbuka namna ambavyo ulikuwa ukinipeleka maktaba na kunirudisha nyumbani ili niweze kwenda kujisomea, hakika hii sitaisahau.
Nakuombea kwa mwenyezi mungu akupe kauli thaibiti, akuondoshee kila gumu na pia akufanyie wepesi katika maisha yako mapya ya akhera. Mpaka siku ambayo kiama kitasimama, tufufuliwe hali ya kuwa ni waumini na tukutanishwe tena hali ya kuwa tumeridhiwa na mwenyezi mungu in shaa allah.
Hakika ya kila nafsi itaonja umauti, na wamebashiriwa mema wale wenye subra, ambao wanapopatwa na misiba husema hakika sisi ni wa mwenyezi mungu na hakika kwake tutarejea.
inna lillahi waina ilayhi raajiun