EU yakasirishwa na marufuku ya Libya

EU yakasirishwa na marufuku ya Libya

jamadari

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2010
Posts
295
Reaction score
92
Tume ya bara Ulaya imeshtumu uamuzi wa Libya wa kusitisha kutoa viza kwa raia wa bara Ulaya ambao wanaruhusiwa kwenda nchi moja hadi nyengine bila kizuizi.
Tume hiyo inasema "imesikitishwa na uamuzi huo usiyo mzuri" wa Libya na nchi zilizo katika mpango wa Schengen zitatafakari "hatua watakayochukua".

Libya ilichukua hatua hiyo baada ya Uswisi kudaiwa kuwanyima ruhusa ya kuingia kwao viongozi 188 wa Libya.

Marufuku ya Uswisi inasemekana kujumuisha kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi na jamii yake.

Uswisi ni moja kati ya nchi 25 zilizoko kwenye eneo la Schengen -nchi za bara ulaya zilizoondowa masharti ya kupita kwenye mipaka yao.

http://www.bbc.co.uk/swahili/news/story/2010/02/100216_eu_libya.shtml
 
Hivi hawa EU wao wanfikiri ni superior kwenye hii dunia? wanawatishia watu kuhusu viza zao, na wao wanaamua nani asiingie kwao na nani asiingie, kwa nini wao wakifanyiwa wanakasirika?

Well done Gaddafi huu ndio uzalendo wa kweli
 
Back
Top Bottom