EU yaitaka Uingereza kuondoka kwa haraka

Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
63,466
88,825
EU yaitaka Uingereza kuondoka kwa haraka

Viongozi wa muungano wa Ulaya wamesisitiza kuwa Uingereza inafaa kujiondoa kwa haraka katika muungano huo wakidai kuwa kuchelewa kwake huenda kukazua wasiwasi miongoni mwa mataifa yaliosalia.

Kamishna wa tume ya Ulaya Jean Claude Juncker amesema kuwa muungano wa mataifa 27 yaliosalia utaendelea.

Uingereza ilipiga kura ya aslimia 52 dhidi ya 48 kuondoka katika muungano wa Ulaya huku waziri mkuu David Cameron akisema kuwa atajiuzulu ifikapo mwezi Oktoba.

Bw Juncker alifanya mkutano wa dharura na rais wa bunge la Ulaya Martin Schulz ,rais wa baraza la Ulaya Donald Tusk na waziri mkuu wa Ujerumani Mark Rutte na kutoa taarifa hiyo siku ya Ijumaa.


160624092524_brexit_640x360_afp_nocredit.jpg

David Cameron na Jean Claude Juncker

Baadaye walitoa taarifa wakisema wanajuta lakini wanaheshimu uamuzi huo wa Uingereza.

Wameitaka Uingereza kuondoka haraka licha ya mpango huo kuwaathiri na kwamba kuchelewa kwake kutazua mgogoro ndani ya muungano huo.


Chanzo: BBC Swahili
 
Muungano imara duniani umebaki ule wa US peke yake. Ule wa USSR ndio ulikuwa wa hovyo zaidi kupata kutokea.
Hata marekani ipo siku kitanuka hasa ikitoka kwenye super power tena itakuwa ni hatari kuwahi kutokea dunia ogopa sana mataifa yaliungwa kwa vipande vipande
 
Hahaha kama "tokeni haraka tuendelee" mnatumalizia mda"naiangalia sauti ya msemaje jinsi ilivyokata tamaa huku akiombea iwe ndoto aamke!!!
 
hahaha kweli watoke haraka,maana Cameron hii ya kusema atastep down October halafu ndo negotiationa zianze ,ni muda mrefu.Halafu nimeona mayor wa Calais kasema UK wachukue boarder yao,na lille jungle wadeal nalo wenyewe wa UK,hahahahaaha sasa sijui watawarudisha wapi hao waarabu wanaotaka kuingia Uingereza kupitia Calais
 
Back
Top Bottom