EU yaipa Tanzania Sh252 bilioni

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
Claud Mshana
UMOJA wa Ulaya (EU) kupitia tume yake inayoshughulikia maendeleo imeipatia Serikali ya Tanzania msaada wa Euro 126.5 millioni sawa na takriban (Sh252 bilioni.


Fedha hizo zitaisaida Tanzania kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwamo miradi ya maji safi, barabara na miundombinu mihimu.

Makubaliano ya kupatiwa msaada huo yalifanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam kati ya Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa na Kamishina wa Maendeleo wa EU, Andris Piebalgs.

Hafla ya makubaliano hayo ilishuhudiwa pia na Rais Jakaya Kikwete pamoja na Mwenyekiti wa EU, Jose Manuel Barroso.


Taarifa iliyotolewa na Ikulu kwa vyombo vya habari jana, ilisema fedha hizo zitasaidia ukarabati wa kilometa 200 za barabara pamoja na kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi zaidi ya 500,000.

Hata hivyo, taarifa hiyo haikuweka bayana maeneo miradi ambayo hiyo itatekelezwa na kipindi chake. EU yaipa Tanzania Sh252 bilioni
 
Back
Top Bottom