Eti watz tunajivunia brash za kupaka rangi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti watz tunajivunia brash za kupaka rangi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Simba Mkali, Oct 17, 2012.

 1. Simba Mkali

  Simba Mkali JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 589
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Nimekaa na kutafakari sana, tena nilijaribu kuwashirikisha hata baadhi ya watu, wengine wakaniambia kuwa Watz tuna brashi nzuri za kupakia rangi ambazo hazipatikani sehemu nyingine duniani. Lengo langu ni kutaka kujua kuna kitu gani kama bidhaa ambayo hata siye wenyewe huwa tunaitumia na kujivunia.

  Mfano; Tanzania kuna mafuta ya Alezeti (pamoja kwamba yapo na sehemu nyingine) je serikali yetu imewezaje kuyafanya yawe bora kwa wananchi wake, yaani kuhakikisha kuwa yanakuwa katika 'pakeji' nzuri na kusambaa kila kona ya nchi kiasi kwamba hata mtu akitoka nje aseme ukifika Tz kuna mafuta ya Alizeti mazuri naomba uniletee kama zawadi.

  Wananchi wa Tz wanajivunia maziwa ya Tanga Fresh? kama ilivyokuwa kwa KCC na Maziwa Mara kama zamani? au kama ilivyokuwa kwa Mkate wa Siha uliokuwa ukitengenezwa na NMC? zamani Wakenya walikuwa wakitusifu kwa Kahawa ya Africafe na pombe aina ya Konyagi, je bado tunaendelea na sifa hiyo mpaka leo hii?

  Hivi kuna kitu gani, bidhaa gani ambayo mtu anaweza kusema jamani Tz kuna kitu kizuri? sipendi tabia ya kusema kuwa Tz tunazalisha mashati mazuri ambayo yanapelekwa nje, sipendi hiki kitu, nataka kusikia kitu ambacho watu wa kawaida huwa tunakitumia.
   
 2. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  Nchi hii kila mtu chukua chake mapema (CCM). watawala wangelikuwa hata siku moja wakawa na mawazo kama ya kwako, tungelipiga hatua. Kazi unafiki wa kulia!
   
 3. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Tuna raisi na mawaziri wanaoongoza kwa kushangaa makasri ya oman
   
 4. Simba Mkali

  Simba Mkali JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 589
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Huwa ninaumia sana ninaposhuhudia matangazo ya bidhaa za Kenya,matangazo yao yanakushawishi mkubwa wa kukufanya kununua sabuni, dawa au kitu kingine lakini Watz tuna kitu gani ambacho tunaweza kukiweka katika tangazo? tangazo likawa zuri na kumshawishi mtu kuipata hiyo bidhaa na zaidi na akiipata inakuwa na ubora uleule?
  Nilikuwa napenda sana kula mtindi fulani hivi ambao unapatikana katika super market nyingi niikijua ni bidhaa ya Tz, nilihisi labda unatengenezwa na Bakheresa, ASAS au unatoka kule Iringa wanapotengeneza Tanga Fresh... wee nilipokagua kopo lake nilijisikia kizunguzungu na hapohapo nikaacha, kumbe unatengenezwa Kenya bana!
   
Loading...