Eti watoto wa siku hizi ni vichwa ngumu! Unamjua Kaini wewe

Mtukutu wa Nyaigela

JF-Expert Member
Sep 4, 2018
6,519
11,039
Kuna watu wamekuwa wakijenga hoja kuwa siku hizi watoto wamekosa maadili na hawana heshima. Na wanafika mbali wanalaumu kuwa wazazi ndio chanzo.

Mimi nina mawazo tofauti. Hivi kuna mtoto jeuri kuliko mtoto wa kwanza kuzaliwa hapa duniani kwa mujibu wa Biblia, yaani Kaini. Huyu alimuua mdogo wake. Alitakiwa kutoa sadaka ya kuchinja wanyama, yeye kwa ujeuri wake akasema anaweza kutoa hata mazao ya shambani kwani sadaka ni sadaka tu. Mwisho wa siku sadaka yake ilikataliwa na akawa na hasira

Kuna hawa mapacha waligombana toka tumboni na mwisho mmoja wapo alienda kuishi kwa mjomba wake, naongelea Esau na Yakobo.

Kuna hawa watoto wa Yakobo walimuuza Yusuph, kisha wakamdanganya baba yao kuwa wameokota nguo zake zikiwa na damu kuashiria kuwa kaliwa na wanyama wakali.

Watoto wamekuwa changamoto miaka yote hiyo. Na humo humo utakuta watoto watiifu na wazuri. Changamoto walizopitia wazazi wa zamani kulea watoto ndio hizo hizo wazazi wa leo wanapitia. Tusikate tamaa
 
Mtoto au watoto wangu watakuwa wa kibabe sana, adabu na heshima kama zote.
Sitaruhusu mtu wa uzao wangu awe tepe tepe.
 
Kuna watu wamekuwa wakijenga hoja kuwa siku hizi watoto wamekosa maadili na hawana heshima. Na wanafika mbali wanalaumu kuwa wazazi ndio chanzo.
Mimi nina mawazo tofauti. Hivi kuna mtoto jeuri kuliko mtoto wa kwanza kuzaliwa hapa duniani kwa mujibu wa Biblia, yaani kaini. Huyu alimuua mdogo wake. Alitakiwa kuotoa sadaka ya kuchinja wanyama, yeye kwa ujeuri wake akasema anaweza kutoa hata mazao ya shambani kwani sadaka ni sadaka tu. mwisho wa siku sadaka yake ilikataliwa na akawa na hasira

Kuna hawa mapacha waligombana toka tumboni na mwisho mmojawapo alienda kuishi kwa mjomba wake, naongelea Esau na Yakobo.
Kuna hawa watoto wa Yakobo walimuuza Yusuph, kisha wakamdanganya baba yao kuwa wameokota nguo zake zikiwa na damu kuashiria kuwa kaliwa na wanyama wakali
Watoto wamekuwa changamoto miaka yote hiyo. Na humo humo utakuta watoto watiifu na wazuri
Changamoto walizopitia wazazi wa zamani kulea watoto ndio hizo hizo wazazi wa leo wanapitia. Tusikate tamaa
Si bure Kaini alikuwa anamoka kitu cha Arusha maana tunaambiwa kwenye bustani ya Edeni palikuwa na kila mmea!
 
Muombe sana Mungu awaongoze vyema, vinginevyo utajuta kuwazaa
Na miongoni mwa misingi nitakayo wawekea wanangu, ni kuwajengea misingi ya kutenda mema, kuishi vizuri na watu, pasipo kushirikisha Mungu.
Kwa ufupi waamini katika mambo mazuri / mabaya pasipo kumshirikisha Mungu, Mungu awe ni ziada kwao.
 
Back
Top Bottom