Eti wasomi

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
948
1,092
Heri ya tarehe 28 mwezi 12 mwaka 2019.

Hivi nyinyi wenye taasisi za vyuo vikuu hamuoni aibu kuweka masomo ya astashahada (Certificate) na stashahada (Diploma) kwenye vyuo vyenu hamjui mnajishusha hadhi au mnaona sifa kuwa na wingi wa namba ya wanafunzi na kufanya elimu biashara.

Eti ndio kunawasomi mpaka nchi inawategemea, sasa hivyo vyuo vya kati wao wafanye nini au nawao waanze kutoa taaluma ya ufundi kama vyuo vya ufundi wafanyavyo? Acheni tamaa kuweni wabunifu wa kozi bwana.

Jikiteni na utoaji wa shahada na kuendelea acheni kujichanganya.

Tatizo la ajira nchini chanzo chake ni hapa mlipoamua kuwa na tamaa na mkakibariki hicho chuo cha kibabu hapo mzizima kitoe ngazi za taaluma za chini ndio kimeleta haya yote.

Maana wahitimu wa hapo wengi waliajiliwa vyuo vingine wakiamini watasaidia masikini wameenda na mawazo waliyoyaona walikotoka mwisho ndio tatizo sasa la ajira limetokea.

Nyinyi vyuo vikuu kwa taarifa yenu Afrika haihitaji wahitimu wa vyuo vikuu kabisa maana sio watendaji bali wafanya maamuzi sasa kwa wingi wa namna tuliozalisha hapa nchini kwa sababu za kisiasa wanaumia sana vijana. Nashangaa kwanini hamkuliona hili tatizo miaka ya 2000 kupitia nchi ya Nigeria.

Uzuri tafiti kuhusu hili zipo. Sio lazima watu wasome shahada ili iwe nini labda?

Unatakiwa uzalishe kitu ambacho utakitumia na kunitosheleza mwenyewe na utazalisha cha ziada na kukipeleka ng'ambo.

Badilikeni nyinyi vyuo vikuu acheni tamaa ya kuwa na makozi mengi mengi.
 
Back
Top Bottom