Eti Talaka ikiombwa na Mme ni makosa?

kokudo

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
2,535
1,651
Hiv mwanamme akiomba talaka kwa mkewe ni sawa au atadharaulika?kumbukeni haki sawa kwa wote....
 
Tumeshazoea ukipata talaka unarudi kwenu! Sasa mwanaume unaombaje talaka? Au wewe ndio uliolewa na kaz imekushnda
 
suala si kuomba tu talaka lazima kuwe na sababu za kuomba hiyo talaka,kwanza lazima mwomba talaka aonyeshe kuwa ndoa yake haiwezekaniki tena hivo lazima aende baraza la usuluhishi hapo kama watashindwa kusuluhisha ndio aende mahakamani akipeleka petition yake,barua kutoka baraza la usuluhishi kuwa wameshindwa kuwasuluhisha, nakala ya cheti cha ndoa na vielelezo vinginevyo vitakavoambana na hiyo petition yake. KTk hiyo petition lazima aeleze ni vitu ghani vinamsukuma kuomba talaka kama mwenzake ni mwasherati usiovumilika manake kumfumania mtu siku moja tu sii sababu ya kuomba talaka lazima uonyeshe umeumizwa vipi na huo uasherati wake, au kama umeumizwa sana kwa kichapo cha mda mrefu(phyisical inujuries nk......pia mwomba talaka aweza kuambatanisha na orodha ya mali walizochuma pamoja na uthibitisho wake kama nakala z ahati ya nyumba magari nk ili kuomba mgawanyo wa mali, na pia idadi ya watoto aliowazaa na ambao angetaka kuwalea(custody of a child nk????)ktk kutoa talaka mahaka lazima ijiridhshe kwanza na ushahidi husika na pia ktk mgawo watoto ndo wanapewa first priority,,,custody itategema kipato na mazingira watakayoishi hao watoto nk nk ......nimechoka mwenye Marriage Act 1971 R.E 2002 atacheki,,,....JAMANI KABLA YA KUONA CHUNGUZANENI VEMA MANAKE TALAKA SII NJEMA SANA INAHARIBU FUTURE YA WATOTO NA WENGI WANAISHI KTK STRESS NK...
 
Jamani husninyo mie akha hata ciombi nilikua natikisa kiberiti@ila hyo avatar ya jino kwa jino imenivnja mbavu
 
mbona wanaomba sana tu,style yao ya kuombea ni kumfanyia vituko mke mpaka achoke kuvumilia aombe yeye!
 
jamani nijuavyop mimi kidini ya islam ni mwanaume ndio mtoa talaka na ndio muomba talaka..... amelaaniwa yule atakaeinua kauli yake na kuimba talaka kwa mume wake....((allah atamkasirikia na hataitazama sura yake4 abadan))) na hakika huwa anajitengenezea janna...)) haya ni mafundisho kutoka kwenye hadith na ay aza qur an,,,, si mie niliesema.... sasa kidogo nimeshangaa kusikia ya kuwa ni jambo geni mume komba talaka.... allahu yaalam maybe..
 
kaka we huna dini..............? ndoa yako uliifunga kwa imani ipi.? angalia imani yako inasemaje kuhusu hiloo.? BALI KTK UISLAMU JAMBO HILO HALIPO. SIJUI KTK IMANI NYINGINE.
 
Back
Top Bottom