Eti ngeleja kupokewa kifalme! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti ngeleja kupokewa kifalme!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mageuzi1992, May 10, 2012.

 1. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Leo katika gazeti la majira nimesoma habari inayohusu mh ngeleja kupokewa kifalme huko kwao sengerema!!. Mwandishi wa gazeti ameandika kwamba uongozi wa ccm sengerema umemuandalia maandamano na mapokezi makubwa mh ngeleja...mapokezi hayo yameitwa ya kifalme!!1. Lengo eti kuthamini mchango wake!!. Habari imeenda mbali kwa kusema kuwa mjumbe wa ccm amesema eti kuondolewa kwa ngeleja ni chuki binafsi!!! Sasa mimi nabaki najiuliza hivi kumbe ccm wamekuwa na mchezo wa kuleana eh! Ndioa maana pamoja na kashfa zote hawa wajumbe wa ccm sengerema wanataka kumtukuza ngeleja kama mfalme!!! Aibu hii tena aibu sana mimi nazani hawa wajumbe wamepotoka kabisa!
   
 2. KANYIMBI

  KANYIMBI JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Rejao na Ritz watakuwepo kwenye hayo mapokezi?
   
 3. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  watanzania wengine hawajielewi,kuna mambo ya kusifia na mambo ya kulaani,sijaona ushujaa wa Ngeleja
   
 4. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,668
  Likes Received: 21,901
  Trophy Points: 280
  Ndio maana kila siku nasema kuwa mwanachama wa hii CCM ni aibu binafsi. Madhara yaliyosababishwa na Ngereja akiwa waziri yanamgusa mtu mmoja mmoja na taifa kwa jumla na hilo halihitaji elimu hata ya ngumbaru kulielewa.
  Sasa hawa Wana CCM wa Sengerema hawana hata hiyo elimu ya ngumbaru?
   
 5. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Mama wee! Kweli yule jamaa aliyesema ilikuwa graduation ya institute of corruption alipatia kabisa. Sasa kibushuti anakwenda kupokolewa na CCM wenzake baada ya ku-graduate na kutoka na Phd ya uzembe, uvivu na ufisadi.
   
Loading...