Eti mwana, mkoko na mjengo, uopi ndo' mpango? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti mwana, mkoko na mjengo, uopi ndo' mpango?

Discussion in 'Entertainment' started by Saint Ivuga, Jul 3, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,407
  Trophy Points: 280
  Wanangu niaje?
  Mi niko poa na Jumamosi ndio kama hii ishaibuka kudadadeki, kila ishu inanitaka mimi, ...dah...
  Dah nimechelewa kuamka leo halafu dizaini halafu nilikuwa na mpango wa kuruka tauni fasta kuna mchongo wangu, ila ndio nikisema niibuke na daladala ndio nitakua nimezingua mazima.

  Manake, mpaka nigombanie kwanza, nipate chansi watu watege mingo kituo kwa kituo, mpaka nifike tauni si jioni hiyo mwanangu?
  Hapo si bora uwe na mkoko wako mwenyewe unaumiliki? Manake hapo ukipata mchongo tu fasta unaruka nini, ..fresh unakamilisha ukirudi unarekebisha mitikasi mingine.
  Uongo mwanangu?

  Mkoko ndio mpango mzima kwa yanki ambaye unaishi tauni, asikudanganye mtu kama kweli we mtu wa michongo ingawa masela wanawacheka sana mayanki wenzao wanapowaona wamechukua mkopo, halafu siku mbili tatu unamuona mwana anasukuma ndinga, halafu mtu mzima anaishi kwenye nyumba ya kupanga.
  Huwa wanaonekana kama hawana akili watu dizaini hizi manake kwa mtazamo wa wana ambao wako kitaa ni kwamba ndinga inakuwa na mitikasi mingi kiasi kwamba itakusababishia ushindwe kupiga hatua nyingine za kimaendeleo, kwa sababu deile inakuwa inahitaji mkwanja ikae sawa.

  Si unajua tena ndinga?
  Mambo ya wese, mara kwenda kuipiga sopu, na hizi ishu kama za kupigwa pasi kitaa zinakuwa za kawaida tu kwa hiyo mambo ya gereji na fundi huwa yanakuja tu mara kwa mara.
  Umeona?
  Sasa hapo ndio unakuta mtu mzima hata ishu nyingine kama za kujipiga sopu mwenyewe, labda pamba, au kupiga jeki familia nini au hata watu wakikuibukia nini kutaka labda uwapige tafu kwa ishu flani unakuwa huna, na ukiwaambia huna ile kukutrasti moja kwa moja inakuwaga ngumu.

  Unasukuma mkoko wa maana halafu huna kitu?
  Ndio madongo yanapoanzia hapo kwamba labda mtu mzima bishoo, unamaindi kuonekana uko juu wakati huna lolote, kama vipi huo mkwanja wa ndunga si bora ungenunua mjengo ukalikita?
  Kutokana na mdongo hayo mtu mzima nikaona kama vipi nifunguke, kweli kuna watu wanafuata mkumbo, dizaini wanabugi kwa kuiga baada ya kuona Zee linasukuma ndinga, anaona na yeye asukume ili wawe levo, lakini anasahau kwamba mwenzake alifikiria mambo kwanza kabla hajaamua ile moja kwa moja kuchukua mkoko.

  Hizi ishu mjue zinaendana na mishemishe!
  Kwa mtu wa michongo, kukimbilia usafiri ndio mpango, si mtu wa ishu? Hizi muvumenti unafikiri unazimalizaje kama huwezi kumuvu hia endi zea?
  Ukisema uchukue mkebe mwanangu, unaweza kujikuta mkwanja wote unaumalizia kwenye mkebe manake jamaa nao wale ukimkodi kutoka hapa na pale tu utasikia mwekundu!

  Sasa kama una misele siku nzima si ndio itakutaka kilo nzima kwa kushughulikia mchongo wa kilo na nusu? Halafu hii michongo wanangu ndio unaweza kujikuta unapiga mkwanja wa kuangusha mjengo na mambo mengine kama haya kwa hiyo mimi kama Zee...

  . ..unanielewa lakini?
  Mimi kama Zee naona bwana suala la mkoko kwa mtu na mitikasi yake naona kama ni bora uanze na mkoko ili kurahisisha michongo halafu mambo ya mjengo yatakuja tu na huu ni mtazamo wangu uinaweza lakini ukawa na wako pia.

  Naweza kuwa najitetea!
  Si unanijua na mie tena mambo zangu?
  Ila kimsingi pa kulala muhimu lakini unawezaje kulala wakati huna mchongo?
  Imejini yuaself, mi nasepa wiki ijayo kama vipi mwanangu au sio?
  Wanlav
   
 2. Sugar wa Ukweli

  Sugar wa Ukweli JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa vijana ambao hawana familiy mkoko ni muhimu sana,kama una familia kubwa nyumba nayo inachukua nafasi kubwa kuliko mkoko kwenye priority!
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 6,999
  Trophy Points: 280
  umejibu vyema kabisa, we uko kwenye mkoko ama Nyumba?
   
 4. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 796
  Trophy Points: 280
  Kama uko stationed one place, mjengo muhimu, lkn kama haukai sehem moja more than 5 yrs, mjengo si issue sana! Mkoko muhimu ingawa waongeza vitambi!
   
 5. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kama unaishi DSM mkoko muhimu! Lakini kama upo mkoa, huitaji hata kuwa na mkoko!
  Kwa DSM mkoko ni basic need but kwa mkoani ni anasa!!!
   
 6. P

  Paul S.S Verified User

  #6
  Jul 3, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Tatizo ni swala la muda na mahela,
  unapata mkoko hadi kwa m3 lakini mjengo bila m40 hujahamia bado,
  Pia ni rahisi kupata mkopo wa m5 wa mkoko na ningumu kupata mkopo wa m50 wa mjengo,
  Uamuzi ni wako kusubiri miaka 10 ukamilishe mjengo ndio ununue mkoko au ununue mkoko ndani ya miezi mitatu kisha ujekujenga baada ya miaka 12.
  Ni mfano tu
   
 7. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 796
  Trophy Points: 280
  Kama uko stationed one place, mjengo muhimu, lkn kama haukai sehem moja more than 5 yrs, mjengo si issue sana! Mkoko muhimu ingawa waongeza vitambi!
   
 8. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,143
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  Mkoko mpango mzima then ishu za mjengo zinafata,kwan ishu ya mkoko m 2 kama vp unapata lakin kitu cha mjengo ebana da! M kadhaa hv ka 50,so kama vp wana mkoko ndo mpango.
   
 9. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #9
  Jul 3, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,127
  Trophy Points: 280
  Mkoko huku kwetu unaweza kurogwa labda pikipiki za kichina, baiskeli na kakibanda ka kishkaji ndio mpango mzima! Mkoko huko mjini kwenye foleni na daladala za kugombea ni muhimu kuliko mjengo!
   
 10. aikaruwa1983

  aikaruwa1983 JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,360
  Likes Received: 1,185
  Trophy Points: 280
  kwa mawazo yangu moto kaa ni added advantage....then if uko dsm ndinga inaplay part kibao kama nyumba vile esp giza linapoingia mara tax, commuter, lodge acha kbs!!!....so ndinga ndo mpango coz sisi wa gongo la mboto utamu wa ndinga tuliouona wakati wa ile "dhifa ya mabomu" kila mtu aliacha mjengo akasepa na mkoko....kimtindo tuliwapiga bao wanaotudai kodi za mijengo yao.....
   
Loading...