Highlander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 3,093
- 1,075
Wana Jukwaa salaam. Nimetoka Tukuyu na habari mbaya. Kaka yetu, rafiki yetu mpendwa DR.Mwakyusa hana bao 2015. Mwanachadema machachari sana Mama Slaa katoa onyo hili juzi akiwa tukuyu. Naweka picha yake hapa, na samahani nimechelewa kuleta picha hii na ujumbe huu mzito kutoka CHADEMA. Eti Rungwe Magharibi itachukuliwa na CHADEMA 2015 bila shaka yoyote. Haya yamesemwa na huyu Mwanachadema machachari sana Mama Slaa. sijui jina lake Josephine Nani vile? Jamani ee, hivi Mwakyusa ana sababu ya kuondolewa bungeni kweli? Mtu mpole vile?
Kilichonifuarahisha zaidi hata hivyo ni utulivu wa wana ccm pale tukuyu wakati wa mkutano huo. Mkutano ulifanyika kwenye uwanja uliopo makao makuu ya CCM wilaya ya Rungwe, lakini ulifanyika kwa amani na utulivu mkubwa sana pamoja na Huyu mwanasiasa hahiri kurusha vijembe vingi kuichoma ccm uwanjani pao, akisema CCM wauaji wakubwa hawatufai kabisa. Haya mada hiyo hapo. Mwakyusa tumng'oe? tumwache. Mi nadiriki kusema siyo mwizi, siyo muuaji. Mama Slaa alimpamba sana mpenzi wake Dr. Slaa kwenye mkutano huu na kuahidi kumleta huyu Mpinzani mkubwa wa Kikwete hapo Tukuyu kabla ya Julai. Dr. Mwakyusa upo? Taarifa nyingine zimesema Chadema na CCM wanaishi kidugu sana pale Tukuyu.