Eti Mkapa Asamehewe?


K

KunjyGroup

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2009
Messages
352
Likes
1
Points
33
K

KunjyGroup

JF-Expert Member
Joined Dec 7, 2009
352 1 33
Nimeandika hii article in response to 'Mkapa anataka azomewe vipi zaidi?' ya Raia Mwema
Very interesting article with a sad ending. Inanisikitisha sana!
‘Nina hakika Watanzania watamsamehe tu; maana kuna mengi mazuri aliyoyafanya kama vile kuanzisha TRA, kujenga barabara kwa pesa zetu wenyewe, kuanzisha TASAF na hata mradi wa maji wa Ziwa victoris nk.’
1. Kwanini unataka Mkapa asamehewe? Kwanini asishitakiwe kwa makosa yake? Fine wewe sio muamuzi wa hayo au utasema ana immunity, lakini kwanini una preach msamaha?
2. Kwani kufanya mazuri ni passport ya impunity? Kwani hizo sifa juu hapo umedai amefanya haikua kazi yake? He went an extra mile; unajaribu kutuaminisha hivyo? Unatakata rais akifanya kazi yake tumsifie? Kwanin tusimsifie tu akifanya zaidi ya kazi yake au akifanya yote aliyo ahidi wakati anaingia madarakani?
3. TASAF imefanya nini cha kujivunia? Hizo pesa za ndani kujenga bara bara, nizamfukoni mwake au sio kodi zetu? Tumsifie kwa kutumia pesa zetu kutujengea bara bara wakati ni jukumu lake?
4. Asamehewe baada ya press conference, how will you prove that tumemsamehe baada ya kutubu? Unadhani tunachotaka ni apology? Wrong Mr. Mwambo! Tunataka justice. Afikishwe makamani na kufirisiwa ikithibitika kwamba aliuibia umma na kuvinja katiba. Zombe alishutumiwa kwa (kushinikiza) mauagi ya watu 4, unaniambia tulitakiwa tumsamehe eti sababu alifanya mazuri mengi kukabiriana na ujambazi nchini? Babu Seya kafungwa, kwani hana mazuri aliyoyafanya? Basi na Lowassa tungemuacha aendelee na uwaziri mkuu eti sababu alikua kiongozi mwenye ufanisi mkubwa na msimamo. A STUPID CULTURE OF IMPUNITY BEING NOURISHED! Mazoe mabaya tunayapalilia.
5. Unajua madhala ya maneno yako ya kutaka asamehewe? Nitaeleza. Mwaka 2000 Mengi na ITV yake walikuwa wanatuonyesha vita vya Angola na nia yake ilikuwa kuaminisha kwamba tukichagua kiongozi wa upinzani, tutakaribisha vita. A powerful and sucessful propaganda. It worked. Leo hii Watanzania wanauoga wa kuchagua au kuamini chama cha upinzani. Last week nilithibisha hilo kwa mara nyingine nikiwa Mwembe Chai. Nilimwambia mama mmoja mfanya biashara kwamba asilalamike tu kwamba wameshindwa, afanye maamuzi ya kupiga kura ili chama tawala kitoke madarakani. Jibu lake lilikua , ‘Tunaishi kwa amani…”
Sasa ndugu Mbwambo unapo preach ‘msamaha’ kwa Mkapa inamaana wao they are above the law. Makosa yao yanafutika baada ya press conference na confession. Kwaiyo Kikwete akiamua kufanya yake na hata yakiwa na uzito gani, akitoka madarakana, atulie kidogo, wewe na wengine mta preach, “Call a press conference and confess” then ataomba msamaha and life will go on eti alifanya mazuri kama kufanikisha bank ya wanawake, alimwaga mabillioni ya Kikwete kwa wananchi na kugawa ambulance mbili kwa wilaya ya Mbozi na Longido. Atakuja rais mwingine pia, perhaps Waziri Mwinyi, Membe, Lowassa etc nao mtindo utakua uleule … Basi na Andrew Chenge, Mramba, Rostam, nk. wapewe nafasi hiyo. Mimi na Generali Ulimwengu tukifakiwa kuchomoka na hela za umma uta preach pia “Call a press conference and confess”? Unajua unajenga nini? Matabaka. Classes za watu. The untouchables and the commoners. Sisi tuishie jela wao wasemehewe. Hiyo ndie Tanzania unataka watoto wako waje waishi? Mimi hapana!

6. Mkapa contributed to making Tanzania kuwa nchi maskini wakutupa.Unataka tuamini kwamba ukiweka TRA, TASAF, barabara kujengwa kwa hela za ndani na mengine uliyoyataja na umaskini wetu katika mezani itabalance? Una tofauti gani na wale wanaedai Mkapa aliimarisha uchumi wa nchi wakati watuwake tulibake na maisha ya mlo mmoja, na hospitali zenye huduma mbovu kama Muhimbili, Amana, Mwanayamala, elimu iliyo chini ukilinganisha na nchi za jirani, shilling yenye bila thamani, mfumuko wa bei, bila ajira kwa graduates wetu, maji shida hadi Dae es Salaam, Umeme wa shida, mishahara kiduchu kwa wafanya kazi wa umma, nk. Kwani kipimo cha mafanikio ya Mkapa nikipi hasa? Kwanini hukurudisha ilani na ahadi za uchaguzi mwaka 1995 ili usemi amefanisha hili na lile na tumpe sifa kulingana na ahadi zake? Huwezi fanya hivyo ndie maana wakati anaondoka (na wengine pia) mnachofanya nikuangalia katika mfuko wa failures/taka taka na kuokota okota tumafanikio twa kutuonyesha (an act of mockery) kwamba eti alifanya mengi. Kwani hayo ndio mafanikio ya ziada baada ya kufanisha ahadi zake za uchaguzi? Kama ndio, mimi na wengine hatuna budi kuimba mbeleko yako ‘Mkapa alifanya mazuri.’ Na hapo, tutakubali “Call a press conference and confess the little crimes you did and we will forgive you.” Vinginevyo, tutaibiwa hata Benzi na BMW za Ikulu na tutawasame tu!
Nimesikitishwa sana,
 
Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Messages
2,525
Likes
8
Points
135
Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2009
2,525 8 135
Hakuna cha kusamehewa wala nini, kama ana makosa basi afikishwe mahakamani na sio wao kujitetea kwa watu, Kila mtu ana wajibu wa kutaka kusamehewa ila mbona hata wezi wa kuku wanafungwa??Sheria zipo kwa watu wote na wote ni waharibu tu
 
Jeremiah

Jeremiah

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2009
Messages
644
Likes
11
Points
35
Jeremiah

Jeremiah

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2009
644 11 35
Mimi binafsi ni mwathilika wa serikali ya mkapa . Haya yote in matokeo ya ulafi wa wa mali za umma . Mkapa alifanya vizuri wakati Mwalimu Nyerere yu hai . Baada ya kufa aliyasahau maadili ya uongozi na kufanya biashara ikulu. na hivyo kuwakosea watanzania. Na mateso yote tunapata inatokana na uongozi wa kiburi wa awamu yake. kama ni mateso niliwahi kuyapata basi ni awamu ya tatu ya uongozi wa mkapa. Na hizo shule za kata alizozijenga ndizo zitakuwa chanzo cha kifo cha serikali ya ccm. Division zero za kumwaga . Nampa pole sana mkapa aombe sana Mungu ampumuzishe mapema ili akiepuke kikombe kitakacho mkuta cha mateso. Lazima kizimbani asimame . hakuna cha utawala bora wala nini .Kama Msanii wetu JK anavyo nogesha wimbo huo kwa kuyakumbatia mafisadi ya RICHIMOND. OLE WAO WALIOHUSIKA KUTUNUNULIA RADA ,NDEGE,KUUZA NYUMBA ZA SERIKARI, MAJENGO PACHA, EPA. MEREMETA ,KIWIRA KAGODA, TRL, TICTS, na mengine mengi .
 
jmushi1

jmushi1

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2007
Messages
19,442
Likes
5,538
Points
280
jmushi1

jmushi1

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2007
19,442 5,538 280
Mimi binafsi ni mwathilika wa serikali ya mkapa . Haya yote in matokeo ya ulafi wa wa mali za umma . Mkapa alifanya vizuri wakati Mwalimu Nyerere yu hai . Baada ya kufa aliyasahau maadili ya uongozi na kufanya biashara ikulu. na hivyo kuwakosea watanzania. Na mateso yote tunapata inatokana na uongozi wa kiburi wa awamu yake. kama ni mateso niliwahi kuyapata basi ni awamu ya tatu ya uongozi wa mkapa. Na hizo shule za kata alizozijenga ndizo zitakuwa chanzo cha kifo cha serikali ya ccm. Division zero za kumwaga . Nampa pole sana mkapa aombe sana Mungu ampumuzishe mapema ili akiepuke kikombe kitakacho mkuta cha mateso. Lazima kizimbani asimame . hakuna cha utawala bora wala nini .Kama Msanii wetu JK anavyo nogesha wimbo huo kwa kuyakumbatia mafisadi ya RICHIMOND. OLE WAO WALIOHUSIKA KUTUNUNULIA RADA ,NDEGE,KUUZA NYUMBA ZA SERIKARI, MAJENGO PACHA, EPA. MEREMETA ,KIWIRA KAGODA, TRL, TICTS, na mengine mengi .
Pole sana kwa kuwa victim wa ufisadi kama ilivyo kwa wananchi wengi.
Kama ni kweli kuwa Mkapa alifanya vizuri wakati mwalimu yu hai na kufanya kinyume alipokufa,basi inamaana ali intend kufanya ufisadi,pointi hiyo kama ni kweli ni pointi nzuri kwasababu ina prove intension yake ya kuwafisadi watanzania,poleni.

Kwenye kuhusu kumsamehe sijui uamuzi huo unafanywa na nani kati ya mahakama,serikali ama wananchi,maana kwa siasa za kibongo anything is possible....Inavyoonekana kwasasa serikali imeshachukua uamuzi huo baada ya kauli ya JK kuwataka wananchi wamwache apumzike pamoja na kauli za waziri mkuu hivi karibuni kwamba watuhumiwa ni victims wa chuki binafsi tu.

Kwahiyo mwelekeo wa serikali unajulikana kuwa ni kwasafisha na kuwakumbatia mafisadi,ama kwa kifupi kuwasamehe,serikali inawataka wananchi nao wachukue hatua hiyo na kuachana na mambo ya madai ya ufisadi ambayo ni porojo....Wananchi wakiamini ni porojo,basi watawachagua mafisadi tena.
Kwa upande mwingine uamuzi unaweza kutolewa na mahakama only and only if serikali itaacha haki ichukue mkondo wake.
 
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined
Nov 21, 2009
Messages
2,974
Likes
32
Points
0
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined Nov 21, 2009
2,974 32 0
Kwanini asamehewe kwani maeomba msamaha lini na wapi?
 
jmushi1

jmushi1

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2007
Messages
19,442
Likes
5,538
Points
280
jmushi1

jmushi1

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2007
19,442 5,538 280
Kwanini asamehewe kwani maeomba msamaha lini na wapi?
Swali ni nani amsamehe na si tu "Asamehewe" Iwekwe wazi kwanza msamaha huo utoke wapi.
Ni kweli hajaomba msamaha lakini haina maana hana makosa.
 

Forum statistics

Threads 1,250,989
Members 481,550
Posts 29,753,440