Eti mfumo dume, thubutuuu, hamuwajui wanawake nyie.....!

Eti mfumo dume, thubutuuu, hamuwajui wanawake nyie.....!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,442


Inawezekana ni kweli wanaume wanaitawala dunia katika kile tunachokiita Mfumo Dume, lakini nao wanawake wanatawala kiota, siyo dunia. Ina maana gani? Kwa mujibu wa utafiti mpya wa hivi karibuni, inaonesha kwamba, wanawake wana nguvu kwenye maamuzi ya masuala ya nyumbani kuliko wanaume.

Watafiti wamegundua kwamba, wanawake kwa wastani, wanakuwa na nguvu kubwa ya uamuzi, unapokuja mjadala nyumbani unaohusu familia. Bila kujali kama ni mwanamke au mwanamume aliyeanzisha majadala huo, wanawake siku zote ndiyo wenye nguvu kwenye kauli ya mwisho.
Ndiyo maana ni rahisi hata kwa wanaume wakorofi kusikika wakisema, ‘nimeamua tufanye alivyotaka, ngoja mambo yaende vibaya, atanijua. Nimemwachia kusudi kama alivyotaka tufanye, lakini ataona mambo yakiharibika.’ Mara nyingi, mwanamke ndiye anayesikilizwa.

Lakini, inaonesha kwamba, kwenye zile ndoa ambapo wanawake husikilizwa zaidi yanapokuja masuala ya ndani, ndoa hizo zinakuwa imara zaidi.
Hii inaonesha kwamba, huenda mwanamke mahali pake siyo jikoni, bali ni nyumbani, yaani ni mtaalamu wa masuala ya familia na uhusiano kwa ujumla, ingawa mwenyewe hajui. Ndoa inapofikia miaka saba, kukawa na amani ya kuridhisha, kama wanawake kwenye ndoa hizo ndiyo wazungumzaji wakuu wa masuala ya ndani, mafanikio ya kindoa na kifamilia huwa mazuri, ukilinganisha na pale ambapo wanaume ndiyo wasemaji wakuu.

Hii ina maana kwamba, ili kufikia mafanikio ya juu katika familia, mwanamume anapaswa kufunga mdomo, kwani majibu mengi anayo mwanamke. Kwa wanaume ambao hawako tayari kuwasikiliza wanawake au kuwaacha wanawake kuwa wazungumzaji wakuu kwenye masuala ya nyumbani na familia, wanapata hasara kubwa. Ni hasara inayotokana na ukweli kwamba, wanaume wengi hawajui kitu kuhusu masuala ya nyumbani na familia kama wanavyojua wanawake.
 
Mwanaume ni kichwa cha familia,,
Mwanamke ni shingo ya familia ni kugeuza mambo.
 
tumeagizwa tuishi na wake zetu kwa akili,ila ni kweli hapo juu maoni
 
Mi akikataaa mitazamo yangu naenda mwelezea kitandani akiwa juu yangu .. Atachomoaje sasa kwi kwii kwiiiiiiiii

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Nadhani kaka Mtambuzi hapa unaongelea wanawake na si wasichana
 
Last edited by a moderator:
Mi akikataaa mitazamo yangu naenda mwelezea kitandani akiwa juu yangu .. Atachomoaje sasa kwi kwii kwiiiiiiiii

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
wewe sasa Una - bribe na ntakuitia TAKUKURU wakuchunguze hapo......???!!
 
hahahah mtani mbona unataka kuleta ubaguzi??/

hahaha naona wewe na amu mmeifurahia kweli hii mada na mmeweka machombezo ya hapa na pale sasa kabla picha halijaungua inabidi niombe muongozo
 
utaharibu bana....kwani galz wanatofautiana na wanawake???
hahaha naona wewe na amu mmeifurahia kweli hii mada na mmeweka machombezo ya hapa na pale sasa kabla picha halijaungua inabidi niombe muongozo
 
Back
Top Bottom