Munkari
JF-Expert Member
- Feb 9, 2013
- 8,084
- 4,365
Wataalamu wa masuala ya mapenzi wanaeleza kuwa penye penzi la kweli hakuna usiri.Mtaficha wee mwisho wa siku watu watajua,ila mkiona mmefanikiwa kuwafanya watu wasijue kwamba nyie ni wapenzi basi mnadanganyana.Hapo hakuna mapenzi ya kweli. Lakini wataalamu hao wa mapenzi wanasema,kama utakubali kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi wa siri,tarajia mambo MAWILI MAKUBWA kukutokea...,... KUSALITIWA-staili ya 'penzi letu liwe la siri hutumiwa sana na watu ambao wametawaliwa na tamaa za kijinga,wasioridhika na mpenzi mmoja.Matokeo yake sasa kila anayemtamani anamchomekea lakini anaomba ama kufanya penzi liwe la siri ili wengine wasijue...... Hivyo ukiona upo kwenye mapenzi ya siri kaa mkao wa kusalitiwa!! Chunga!! KUBAMBIKIWA-kama wewe ni mwanaume na ukakubali kuwa na uhusiano na msichana kwa siri,ni rahisi sana kubambikiwa mimba. Mpenzi wako anaweza kutembea na mwanaume mwingine kwa siri na akapewa ujauzito lakini kwa kuwa unajua wewe ndiye ambaye upo naye huwezi kukataa,utasema ni yako kumbe umeingia chaka.! Shtukaa!!! * ACHENI MAPENZI YA SIRI *