Kuna dhana kwamba wanawake walioajiriwa wanakabiliwa na mazingira ambayo yanawalazimisha kuingia kwenye vitendo vya kutoka nje ya ndoa zao, ukilinganisha na wanawake ambao hawajaajiriwa hususani mama wa nyumbani jambo ambalo katika maisha ya kawaida bila utafiti linaonekana kama vile ni kinyume yaani akina mama walio majumbani ndio ambao hutoka nje zaidi.

Niliwahi kuwahoji wanawake kadhaa jijini Dar, mwanamke mmoja kati ya watano alikiri kwamba yuko tayari kujitongozesha kwa bosi ili kujaribu kulinda nafasi yake kazini au kupandishwa cheo. Nilifanya mahojiano hayo ili kujua idadi wanaume wanaotumia nafasi zao kazini kuwadhalilisha wanawake kijinsia.

Lakini bila shaka suala la mapenzi kwa wanawake walioajiriwa lina nguvu na kwa hiyo limekuwa likifanyiwa tafiti katika sehemu mbalimbali duniani. Tofauti na tafiti ambazo zimefanywa hivi karibuni zinaonyesha kwamba mwanamke mmoja kati ya kumi walioajiriwa huwa anaonyesha tabia za kimapenzi au kujitongozesha kwa bosi wake.

Tafiti hizi zinaonyesha kuwa yule mmoja kati ya kumi ambaye hujitongozesha kwa bosi huishia kutembea naye au hata kuolewa naye kama hana mume na pengine kuvunja ndoa yake. Inaelezwa pia kuwa mmoja kati ya wanawake kumi wanaojitongozesha kwa mabosi huwa anapandishwa cheo. Hii ina maana kwamba wanawake wanaopandishwa vyeo kwenye maeneo ya kazi huenda mmoja kati ya kila kumi hupandishwa kwa sababu za kimapenzi hata hivyo siyo lazima iwe hivyo.

Tafiti hizo hata hivyo hazikulenga katika kuonyesha kwamba wanawake ni dhaifu bali huenda zimelenga katika kuonyesha kwamba idadi ya wanawake wanaojitongozesha kwa mabosi ni ndogo kuliko inavyotazamwa au kuaminika na pia kuonyesha kwamba bado wanawake walioajiriwa wako kwenye nafasi kubwa zaidi kushiriki mapenzi kuliko wale walioko majumbani. Ni juu ya wanawake ambao wanadhani ni halali kuuza thamani zao kwa ajili ya kazi kubadili mwenendo huo..
deep sanaHiii topic ni very deep
hv unajua procedure za kupandishwa cheo? sasa sijui utatembea na mabosi wangapi maana icho cheo kitakuwa cha kichina watu wajanja siku hz?
deep sana
Tafiti hizi zinaonyesha kuwa yule mmoja kati ya kumi ambaye hujitongozesha kwa bosi huishia kutembea naye au hata kuolewa naye kama hana mume na pengine kuvunja ndoa yake. Inaelezwa pia kuwa mmoja kati ya wanawake kumi wanaojitongozesha kwa mabosi huwa anapandishwa cheo. Hii ina maana kwamba wanawake wanaopandishwa vyeo kwenye maeneo ya kazi huenda mmoja kati ya kila kumi hupandishwa kwa sababu za kimapenzi hata hivyo siyo lazima iwe hivyo.
Hujaiweka vizuri, kujitongozesha au kutongoza ni jambo la kawaida sana, iwe kwenye daladala, kazini, shule au popote ndo wazazi wetu walivyokutana mpaka tukazaliwa. ngoja niinogeshe point yako, ila watoto najua hawatanielewa.
Wanawake au kwa maneno mengine, wake za watu walioolewa kutembea na mabosi au niite wafanyakazi wenzao imekuwa ni tatizo kubwa ambalo limeharibu familia nyingi sana, kama hujui uliza utaambiwa.
my take: Hii ni tabia ya malaya, hata kama jirani yake au mtu wa karibu atakuwa ni mbuzi au ng'ombe dume basi atatembea nae. mi nachukulia huyo atakuwa kama kunguru mwingine wa zanzibar yani hafugiki, ombi kwa wanaume wenzangu, ukigundua na ukawa na uhakika dont hestate, PIGA CHINI.

in comparison to what??????????????