Eti hiki ndicho kinachowakera wanaume kutoka kwa wadada?

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,317
7,509
Nimesikia wanaume wanasema wanakereka na hii tabia ya wanawake;

Mwanamke hamfahamiani na mwanaume, wanakutana may be njiani, sokoni, barabarani, kwenye usafiri au kwenye mitandao ya kijamii, Mwanaume anamuomba mwanamke mawasiliano anampa bila shida.

Baada ya saa kadhaa au siku kadhaa mwanaume anaanza kumtongoza huyo mwanamke, halafu mwanamke anamkataa ama anamwambia nina mchumba au nina mpenzi haitawezekana au anamwambia "Kwani nimekupa namba ili uniambie hizo habari?

Wanaume nimekutana nao kwenye panton wanasema bora huyo mdada asimpe namba kabisa maana atajua alishakataliwa kabla, badala ya kupewa na kupokea negative

Je, ni kweli hiki kitu kinawaudhi wanaume?

Je, kwani nikikupa namba ya simu ni kiashirio kuwa utakaloniambia nitalikubali?

Mwingine akatoa kauli kuwa kwani ulinipa namba tuwasiliane kwani wewe, ni ndugu? wanaume bwana

Hebu funguka hapa, kupewa namba na mwanamke huwa ni kiashirio cha awali cha kukubaliwa utakachoenda kumwambia baadae?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukinipa namba sio lazima nikutongoze Nina namba nyingi za wadada nilijikuta naomba tu baadae napotezea diwatafut na kuishia kuzifuta tu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Halafu wanawake mnajifanya tu hamuelewi lakini mnakuwa mashaelewa.
Sasa wewe tumekuatana tu leo nimeomba namba na katika mazungumzo hatukuwa na mazungumzo yeyote ya kibiashara wala kikazi. Unakuwa tu hujaelewa why nimeomba no yako?
 
Mbona unauliza mambo mepesi sana?

Kuna hapana yenye maana ya NDIYO na kuna hapana yenye maana ya HAPANA.

Pia kuna ndiyo yenye maana ya HAPANA na kuna ndiyo yenye maana ya NDIYO.

Kwa wanaume marijali haya mambo mepesi sana ila kwa vitoto vya mwaka 2000 ni mzigo kwao.
Unforgetable
 
Back
Top Bottom