Eti haya maswali majibu yake ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti haya maswali majibu yake ni nini?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Dena Amsi, Nov 4, 2011.

 1. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #1
  Nov 4, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Habari zenu wapendwa wote wa jukwaa letu pendwa la MMU.

  Natumaini wote muwazima kabisa na ni buheri wa afya japokuwa ya kwangu si njema sana ila nashukuru nimeweza hata kuandika haya.

  Nimekuwa nikisikia nikikutana na watu mbalimbali wakisema " Ningekuwa sijaoa ningekuoa wewe"

  AU "Ningekuwa sijaolewa ningeolewa na wewe" Nimejaribu kuzitafakari hizi kauli nimekosa majibu hebu waungwana na wataalamu hebu nisaidieni?

  Unaoa au kuolewa kwa lazima mpaka ufikie kusema maneno kama hayo???

  Au nitamaa tu ndo zinasumbua? Ama ni nini hasa?? Hebu nisaidieni

  Nawatakia maandalizi mema ya weekend.

  DA
   
 2. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ni kukosa staha! Mtu anayezungumza hivyo, mwangalie sana, analo lake jambo, tena si zuri! Message anayokuletea ni kwamba wewe ni bora kuliko aliyenaye huko kwenye mahusiano yake. Na kwamba haridhiki na hayo mahusiano yake. Hii kauli mara nyingi haiwezi kusemwa mbele ya yule mwenzie. Manake nini? Full unafiki na nia mbaya. Mara nyiingi anakupaka mafuta kwa mgongo wa chupa!!
   
 3. super thinker

  super thinker JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Binadamu kwa asili ana tamaa,hata baada ya kuoa haimaanishi ataacha kutamani anavyoviona nje,kwa anayeweza kumiliki hisia zake ndo yule anayetulia na ndoa yake na anayeshindwa anashawishika kirahisi sana kutoka nje ya ndoa yake kwa kupanga ama kutokupanga!!ANAYE SEMA maneno hayo akimaanisha ni yule aliyeshindwa kumiliki hisia/tamaa yake japokuwa wakati anaingia kwenye ndoa alihisi alicho nacho kimekidhi haja yake!!
  Tamaa haitamwishia bin-adamu ila "control over your tamaa" is what matters.
   
 4. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 526
  Trophy Points: 280
  mahanjam doti comu
   
 5. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  hizo ni lugha tu za kimihemko dada
  watu wakiwa kwenye mihemko akili na mdomo havifanyi kazi kwa ushirikiano
   
 6. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  ni kukuzuga tu apate anachohitaji toka kwako.
   
 7. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #7
  Nov 4, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Na saa nyingine huwa naona hata wanaanza kuzungumza mambo yao ya home oohh mume wangu yaani yuko hivi mara vile uliolewa ya nini sasa?? Nakosa majibu
   
 8. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  ...wakati mwingine kuoa au kuolewa hakutokani na dhamira za wahusika.

  ...kuna wale wanaolazishwa na wakati (umri) kabla hajafikia chaguo lake.

  ...kuna shurti kutoka kwa wazazi.

  ...hadhi ya mtu kwa wakati flani. Anaweza kujiona yuko juu au chini lakini akaoa au kuolewa na mtu aneona kuwa ni wa hadhi yake pasi na kumpenda moyoni.

  ...wazuri wanazaliwa kila wakati, binadamu siku zote ana tamaa na ndizo zinasukuma watu kutamka hayo.

  ...kero za ndani ya ndoa yake kwa wakati huo vinatoa msukumo kwa yule anaedhani anafaa na kumtamkia yale yaliopo moyoni mwake.

  ...simulizi kutoka kwa wengine kuhusu ndoa.

  ...nk...
   
 9. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #9
  Nov 4, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  IMO Ndoa ni mtihani saana… Kumpata mtu wa kuolewa/kuoa ni mtihani wa hali ya juu saana…. Wanadamu tunatabia mbali mbali, tokana na mazingira/tamaduni/malezi/exposure yalo pishana from one to another person. Bahati mbaya ni kua sasa hivi tunaoana na watu ambao hujawahi tia machoni mwako maybe for the last 28 years huko nyuma (depending na miaka yako); mnakutana mjini humo na kudondokeana na hatimae hata kuoana…. Kauli hizo ulitoa hutokana na the below causes….


  1. Upo dissapointed in your spouse… yaani baada ya kuingia katika ndoa ndio unagundua the true colors ya huyo spouse… Vitabia vyaweza kua vidogo dogo but vinakeara kamavile Uchoyo, Uvivu kupita mpaka, ubaguzi wa ndugu, annoying habits related to sex, tamaa ya vitu hivo kuto kua na focus ya future yenu na the like… Unapokutana na mtu ambae anaonekana ni nafuu ya huyo ulonae wajikuta ukongea hayo….
  2. Kutoendana na mwenza wako… Hana shida yoyote ile BUT interest zenu ni completely different.. Nitolee mfano kwangu; as much as ni mtu mzima I still love Music (hata ya vijana)-sina maana clubbing, napenda books hasa reading, napenda once in a while nitoke outing na ni dress up… Basi ingetokea napata mume ambae hapendi kabisa hayo mambo – yaani kitendo cha kuwasha bedside lamp nisome kitabu kabla ya kulala kwake yeye ni kero… Kitendo cha kusikiliza Music ya vijana hali labda yeye anataka ya dini ni kero…. Kitendo cha kusema natoka anitoe out kwake ni kero…. Ni vitu vidogo but sometimes unajuta!
  3. Nyingine ni simply tu because you don't feel loved but you do kwa huyo mtu – Hii sio nzuri saana for mara nyingi penzi jipya ni exciting, hivo new love feelings are in most cases "Stronger" than mtu ambae umeishi nae kwa mda mrefu…. Inahitaji busara ya hali ya juu saana (thou it is very straining)
  4. Lingine ni maneno yanatolewa bila kumaanisha – ili mradi tu kumfurahisha msikilizaji…. Ambae mara nyingi malengo ni kutaka tu kuvuana nguo….
   
 10. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #10
  Nov 4, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  hilo nalikubali lakini kwanini ufike kutamka ujinga kama huo kwani umeshindwa kumsomesha mtu akakubali mpaka utumie njia mbadala?? Mapenzi yenye haya ya dot.com??? wapi na wapi bana
   
 11. Ambakisye Lazar

  Ambakisye Lazar Member

  #11
  Nov 4, 2011
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  binafsi, nahc hlo lnawezekana na lina logic ndani yake kama hali ipo hivi:- wandugu, ni waz kua co wote wameoa/olewa na mtu ambae kweli alimpenda kwa dhati. Ndoa nyingi zmekua ni zenye motive nyingine other than true love. Watu wanakutana na kuoana ndani ya siku chache wakidhani wamependana kweli, kumbe ni :eek:bssession: tu. So anakuja kuktana na mtu mwingine, gafla moyo wake unatamani/penda tena au pia anakua obssessed tena. So its possible jamani. Tukumbuke true love is not something that one can force ata kama upo ndani ya kifungo cha ndoa.
   
 12. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #12
  Nov 4, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  hiyo red naona nikujiongezea matatizo tu mie naona anyway wengine wako hivyo
   
 13. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #13
  Nov 4, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye red nakubaliana na wewe kabisa maana baadae huwa wanaanza ni shetani kumbe hakuna cha shetani wala nini ni wao wenyewe kuyatengeneza mazingira
   
 14. s

  shalis JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  si unajua denna .. ukiwa nakitu huwezi jua dhamani yake mpaka kiondoke .lol
   
 15. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #15
  Nov 4, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Hiyo bluu haya bana
   
 16. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #16
  Nov 4, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  refer no moja sis sasa huyo suppose ni mume wa mtu anamwambia tu hawara anakuwa amemsoma vp hzo tabia maana tabia nyingine zinachukua muda mrefu kusomeka kumbuka
  ujue unavokaa na mtu muda mrefu ndo unavogundua weakness zake na magaps.
  kuna watu siku iyoiyo anasema loh ningekuwa nimekuona wewe ningekuoa loh? si mihemko tu jamani huyo maana sidhani kama in the first sight unaweza kuwa na sifa zooote kumzidi mwenza wake
   
 17. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #17
  Nov 4, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Shalis hapa umenena kweli naunga mkono
  Mara nyingi huyu mwanamke/mwanaume yukoje hata natamani
  asingenioa ngoja aondoke unaanza kulia lia he he he ndoa ngumu hizi mie haya
   
 18. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #18
  Nov 4, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Hiyo red Bebii ni ukweli kabisa tena mwingine hata kukuona hajawahi anaanza kukwambia maneno kama hayo si upuuzi tu huo jamani??

  Eti yaani mie nampenda kweli kaka yako ningekuwa sijaolewa angenioa kamuona tu kwenye picha hata hajawahi kumuona live kha wajameni
   
 19. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #19
  Nov 4, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Hahaha Dena Amsi. VIVA JF.
   
 20. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #20
  Nov 4, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hata kama hali halisi ni kama hivyo ulivyotaja; lakini si justification ya kusema hayo aliyoyasema mtoa mada. Hayo husemwa kwa lengo fulani tu! Kwani huyo anayemwambia angemuoa au angeolewa naye anamjua undani? Kama anasema hivyo kwa sababu kweli hali iko hivyo usemavyo basi ana matatizo ya kujiamini. Na in most cases hata ukikubali he/she will find other faults in you too!

  Mtu akisema hivyo mkubalie tu, ila atakachoomba baada ya hapo, mkumbushe kuwa hata wewe hakufahamu vizuri yanaweza yakatokea hayo hayo ya anayemsema kwako - Atajifunza kuwa na staha - ikiwa kweli anazungumza akimaanisha.

  Ila nijuavyo wengi hasa wanaume husema hivyo katika hali ya kubembeleza ili apewe yeye, basi. Akishapewa ... enough!!
   
Loading...