Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Kuna msemo kwamba uzuri huwa uko kwenye jicho la mtazamaji, sio kwa yule au kile kinachotazamwa. Bila shaka msemo huo una ukweli kidogo. Kwa nini? Kwa sababu watafiti wengi wa masuala ya saikolojia ya upendo wana ugunduzi tofauti.
Wanasema wamebaini kwamba, kunakuwa na makubaliano, yasiyo rasmi katika jamii kuhusu uso mzuri au mbaya. Ina maana kwamba, pamoja na kuwa, kila mtu ana namna yake ya kupima uzuri wa sura, bado kuna ule uzuri unaopangwa na jamii. Taarifa mbalimbali za utafiti, ukiwemo utafiti uliofanywa na jarida la Experimental Psychology; Human Perception and performance, zinaonesha kwamba, msemo huo wa zamani una nguvu yake, lakini siyo kwa asilimia mia moja.
Ni kama vile una nguvu nusu, na hili la jamii kuwa na vigezo vyake vya uzuri wa uso lina nguvu nusu.Hii ina maana gani? Kwamba unapoona mtu fulani ni mzuri au mbaya wa sura, ujue hapo kuna maono yako nusu na maono uliyofundishwa na jamii kuhusu uzuri, nayo ni nusu.Ndio maana kwa hali hiyo, unaweza kukuta idadi kubwa ya watu mahali wakasema fulani ni mzuri au mbaya.
Kama ingekuwa uzuri na ubaya uko kwenye macho ya mtazamaji, yaani yeye ndiye anayeamua siyo kile kinachotazamwa, basi kungekuwa hakuna mahali ambapo, watu wengi wangeunga mkono kuhusu uzuri au ubaya wa sura ya fulani.Kuwepo kwa hali hiyo, kunaonesha kwamba, jamii nayo, bila kuambiana au kufanya vikao, inakuwa tayari ina vigezo vyake kuhusu uzuri. Hiyo ipo kila mahali duniani. Kila unapoenda utakuta watu wanahesabu uzuri au ubaya kwa vigezo fulani.
Mara nyingi utakuta watu wengi wanasema mtu fulani n mzuri au mbaya, lakini utakuta watu wengine wanatofautiana na hao kwa kiasi fulani. Hawa ni wale ambao wanatumia upande ule mwingine wa mtu binafsi katika kuamua uzuri au ubaya………….Sasa mmeelewa eh!