Eti ameniacha kisa kofi moja tu

Eti ameniacha kisa kofi moja tu

nyaggad

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2014
Posts
1,160
Reaction score
694
Habari wandugu, natumaini mko poa.

Mimi nina mpenzi wangu tumekuwa nae kwenye mahusiano huu ni mwezi wa tatu,sio siri huyu binti nampenda sana, nimejitahidi kumhudumia kadri niwezavyo kwa mda mfupi nilikuwa nae, kwa sababu nina nia ya kumuoa, sasa juzi nilikuwa na rafiki yangu tupo maeneo ya Sinza tukapita kwenye bar moja hivi ghafla nikamuona mpenzi wangu nae yupo mle ndani ya bar anakunywa kinywaji wakiwa wamekaa na mwanaume mmi simjui, ndipo nikaamua kumpigia simu mpenzi wangu nakumuuliza yuko wapi.

Akapokea simu nakunijibu yupo nyumbani kwao anapika na wakati minamuona yupo na kijeba wanakunywa vinywaji huku wanacheka, sio siri nilipatwa na hasira ndipo nikaamua kumtuma rafiki yangu akamuite ili niongee, aliponiona alishangaa na aliponisogelea tu sikumsemesha neno lolote nikampiga kofi moja la nguvu rafiki yangu akanishika mikono na watu wakajaa kidogo, nikaamua kuondoka na yule binti akawa amekipingia.

Sasa zimepita siku mbili yule binti nimempigia simu akapokea akaniambia yule alikuwa kaka yake mtoto wa baba yake mdogo na pia ameniambia mimi na yeye basi amesema hawezi kuishi na mtu kama mmi tena, nimejaribu kumuomba msamaha lakini wapi amekataa katakata.

Naombeni msaada wa mawazo jamani nifanyeje? Eti kofi moja tu linikoseshe mke jamani.
 
Kama alikuwa na kaka hapakuwa na sababu ya kukwambia uwongo na pia asingeshtuka kukuona na vilevile asingekimbia..nadhani alikufanya ATM. Ndo dada zetu walivyo ck hizi..walio wengi japo wapo waaminifu wachache
 
Ungeuliza kwanz......ila isnt late yet,tongoza upya kama ulimpa vitu vya nguvu atarud tu ila kama ndo vilee hakunq namnaa
 
Kwanza unampiga mkeo? umemtolea mahari? mahusiano ya miezi mi3 unampiga yangekua miezi sita? au akitimiza mwaka na meno hana, Mwanamme anatakiwa awe muelewa ungemuuliza kwa hekma na upole ungejua yote lakini kwakipigo anajitambua huyo mwanamke ndio mana anaona naiwe basi, ivi mpaka leo kuna wanaume wanaopiga wanawake kweli?
Kaka kama mmeshindwana TABIA muache na huo mchezo kwanza amekufundisha nani au umeona wapi? huyo ni mtoto wawatu unampiga kofi na anakufia unafanyaje? tumia busara sana mara nyengine,sorry kama ntakua nimeongea sana.
 
Umefanya kosa kubwa sana kumpiga mtoto wa watu bila hta kumuuliza aliyekaa naye ni nani

ukaamua kuchukua silaha mkononi ona sasa ushakosa maji ya moto

kumbuka kuwa

HASIRA HASARA UMESHAJIKOROGA UNA BUDI KULINYWA

hata ingaekuwa mm umenidhalilisha kwa watu kiasi hicho umenipiga bila sababu nakusepa tu kimtindo bila hata kupiga honi
 
bora umempatia hichi kidonge chake maana wanmezidi kunyoosha mikono yao kupiga wanawake akome na huyo mwanamke amefanya jambo zuri kumwacha
Kwanza unampiga mkeo? umemtolea mahari? mahusiani ya miezi mi3 unampiga yangekua miezi sita? au akitimiza mwaka na meno hana, Mwanamme anatakiwa awe muelewa ungemuuliza kwa hekma na upole ungejua yote lakini kwakipigo anajitambua huyo mwanamke ndio mana anaona naiwe basi, ivi mpaka leo kuna wanaume wanaopiga wanawake kweli?
Kaka kama mmeshindwana TABIA muache na huo mchezo kwanza amekufundisha nani au umeona wapi? huyo ni mtoto wawatu unampiga kofi na anakufia unafanyaje? tumia busara sana mara nyengine,sorry kama ntakua nimeongea sana.
 
We jamaa boya sana ...na nakuona kama unakosa "socialization" kwani kama ni mtu wa busara ilibidi umuulize mwenzangu kunani, huyu bwana ni nani....na sio kumchara kofi a kufa mtu ghafla bin vuu. hapo umebugiii...
Ila demu wako nae haache kisirani namna hiyo kama kweli anakupenda kwa dhati.
 
Back
Top Bottom