Ethiopia yakataa wachunguzi wa kigeni

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Ethiopia imepuuza pendekezo la Umoja wa mataifa na Muungano wa EU wa kutaka wachunguzi wa kimataifa kuingia nchini humo na kuchunguza vifo vya mamia ya watu wanaodaiwa kuuwawa kufuatia miezi kadhaa ya maandamano ya kuipinga serikali.

Waziri Mkuu Hailemariam Desalegn ameiambia BBC kuwa tume ya kitaifa ya haki za Kibinadamu tayari inachunguza visa hivyo. Mapema mwezi huu mjumbe maalum wa Muungano wa EU kuhusu haki za kibinadamu aliitaka Ethiopia kushirikiana na Umoja wa mataifa kuhusu suala hilo.

Bunge la nchi hiyo hivi majuzi liliongeza muda wa hali ya hatari iliyotangazwa mwezi Oktoba mwaka kwa miezi minne zaidi.

Akizungumza na BBC Waziri mkuu huyo ametetea hatua ya serikali yake kuongezea muda tangazo la hali ya hatari iliyotangazwa mwezi Oktoba mwaka jana,akidai hali hiyo ilihitajika ili kuweza kukabiliana na baadhi ya watu ambao bado wana nia ya kuleta ghasia.

Kuhusu uchunguzi wa vifo vya mamia ya Watu waziri Desalegn amesema ni lazima haki ipatikane kwa sababu kuna nia ya kushughulikia hilo ndani ya Serikali. Amesema uchunguzi umefanywa na matokeo yake yatawekwa wazi.

Chanzo: BBC
 
Mamia ya wa oromo wamefungwa jela

Mamia ya wa oromo wameuliwa

Mamia ya wa oromo wamepata vilema vya maisha

Kwanini anakataa wachunguzi wa nje wakati aliamrisha polisi na jeshi wawaue watu na kuwakamata wapinzani na kuwafunga jela?
 
Mbona Syria walipigwa, wapige na Ethiopia kwa mauaji haya si kwenda North Korea kutafuta chokochoko.
Trump bwana, au Ethiopia hakuna maslahi yake?
 
Acha sisi tuzalishe gesi kwa wingi, tuchimbe uranium yetu selous na turekebishe mikataba ya madini na gesi hahahahahaha
 
Kumbe UN wana macho makali hivyo wameona mpaka Ethiopia duuh!!!! aisee sijui nani anawapa info
 
Back
Top Bottom