Ethiopia yajiondoa wenyeji michuano ya Challenge

Ethiopia yajiondoa wenyeji michuano ya Challenge

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,175
Reaction score
64,552
Baada ya Ethiopia kujiondoa kuwa mwenyeji wa michuano Soka ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na kati CECAFA mwaka huu, Timu ya Taifa ya Tanzania, taifa Stars imevunja kambi ambayo ilikuwa ni sehemu ya kujiandaa na michuano hiyo.


Akizungumza jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Boniface Wambura amesema kocha Mart Nooij alishaanza maandalizi ya michuano hiyo ambapo timu ilitakiwa kuweka kambi nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo.
Wambura amesema CECAFA itakapotangaza nchi mwenyeji wa michuano hiyo, kocha ataandaa programu kwa ajili ya mandalizi ya michuano hiyo.

chanzo:EATV
 
Cecafa ni full usanii,imefikia muda wa kujiunga Cosafa,maana vigezo vyote vya kuwa wanachama wa Cosafa tunao
 
Hili shirikisho sasa ni sawa tu na ile kamati ya miss tanzania.
 
Naunga hoja bora tujiunge COSAFA kwanza wapo juu kisoka na watatusaidia sana katika uendeshaji na mfumo mzima wa kiutendaji Jamal Malinzi muda ndo huu wa kujiunga na cosafa. Regards.
 
Last edited by a moderator:
Naunga mkona hoja...Twende Cosafa....na tutoke EAC tUBAKI sadc PEKE YAKE
 
Back
Top Bottom