esther mashiker
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 616
- 555
Imeelezwa kuwa nchi ya Ethiopia inaanza programu ya kufundisha lugha ya Kiswahili katika ngazi ya cheti, stashahada na shahada katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa, ifikapo Septemba 2019.
Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya mazungumzo yaliyofanywa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia namna ya kutekeleza programu hiyo.
Hatua ya UDSM imekuja ikiwa ni miaka miwili tangu Rais John Magufuli ahutubie kwa lugha ya Kiswahili akiwa Jiji la Addis Ababa Ethiopia kwenye mkutano wa Wakuu wa nchi za umoja wa Afrika, pamoja na mambo mengine, alitangaza rasmi kuanza kufanya kazi kwa jengo lililopewa jina la Julius Nyerere ambalo limejengwa Addis Ababa.