Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,565
- 7,993
Mbunge wa viti maalum kupitia kundi la vijana toka chama cha mapinduzi akiwakilisha mkoa wa Mara wilaya ya Bunda alikuwa akifanyiwa mahojiano katika kipindi cha ''hot mix'' kinachorushwa kupitia kituo cha television cha EATV - Chanel 5!
Akaulizwa swali kuwa nje ya siasa anapenda kufanya shughuli gani?mojawapo ya shughuli aliyoitaja kwamba huifanya ni pamoja na kusoma vitabu na kusikiliza hotuba za wanaharakati kama Martin Luther King Jr., Mwalimu Nyerere na Mandela!
Katika kukoleza maelezo yake akasema anapenda sana kusoma kitabu kinachoitwa ''How to be a Good Political Leader''. Mtangazaji akamuuliza jina la Author wa hicho kitabu lakini mheshimiwa mbunge akashindwa kumtaja kwakuwa alikuwa hamkumbuki pamoja na kuomba apewe muda ili amkumbuke!!
MY TAKE:
Kwa mtazamo wangu si rahisi mtu kusahau jina la author wa kitabu unachokipenda kukisoma mara kwa mara! Pengine Mh.Esther alikuwa anatafuta mileage kwamba ni msomaji mzuri wa vitabu lakini kachemka kwa kutomjua author wa kitabu akipendacho!
Esther Bulaya ndie nani?
Esther Bulaya wala siyo kiongozi kama anavyojitanabaisha. Tena anajitahidi sana kukaa karibu na Halima Mdee ili amsaidie mambo ya kiuanaharakati, lakini wapi! Hawezi kuwa mwanaharakati hata chembe.
Pamoja na kuonekana amechemka ila nasikia ni kipenzi kikubwa kwa wananchi wa jimbo la Bunda, na kwa kiasi kikubwa anatishia maisha ya kisiasa ya Mzee Tyson, watu wa Jimbo la Bunda wanaweza kutupatia ukweli
Esther Bulaya ndie nani?
Esther Bulaya wala siyo kiongozi kama anavyojitanabaisha. Tena anajitahidi sana kukaa karibu na Halima Mdee ili amsaidie mambo ya kiuanaharakati, lakini wapi! Hawezi kuwa mwanaharakati hata chembe.
Mie nimeshangaa jibu lake. Maana kaulizwa nje ya siasa hupenda kufanya kazi gani? Eti anasikiza hotuba za Martin Luther King jr, Nyerere na Mandela. Hivi kusikiliza ni kazi? Au mie ndio mshamba! Yaani kuna watu ambao kazi zao ni kusikiliza hotuba tu?
Nilitegemea aseme labda anafundisha, au analima anafanya biashara au hata anaandika vitabu n.k na si kusikiliza tu kama kazi yake zaidi ya siasa.