Ester Bulaya: Game ya Kinondoni ni kama 'Escape from Sobibor'. Vita ni vita mura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ester Bulaya: Game ya Kinondoni ni kama 'Escape from Sobibor'. Vita ni vita mura

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Hivi punde, Feb 13, 2018.

 1. Hivi punde

  Hivi punde JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2018
  Joined: Apr 1, 2017
  Messages: 1,012
  Likes Received: 2,327
  Trophy Points: 280
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Mbunge wa Bunda, Mhe. Ester Bulaya ametangaza vita katika Jimbo la Kinondoni huku akiapia kwa Mungu wake kuwa atalinda kura za mgombea wao na lazima atangazwe mshindi kwa madai wamejipanga vilivyo.

  Bulaya ametoa kauli hiyo zikiwa zimebakia takribani siku nne pekee kuelekea marudio ya uchaguzi mdogo katika majimbo ya Siha na Kinondoni ili wananchi wa maeneo hayo kupiga kura kwa mtu anayemuhitaji kuwa muwakilishi wake katika jimbo.

  "Haki ya Mungu, Baba wa Taifa angekuwa hai angetoka CCM kwa sababu CCM ile sio hii ya sasa ambayo haifuati utaratibu, poleni wanaccm wenzangu wa zamani mmedharauliwa kwa kutoshiriki kura za maoni kumpata Maulid Mtulia. Baba wa Taifa alikuwa haendekezi vitu kama hivyo, lakini anafanya hivyo akiamini kabisa wanakinondoni mtachagua mgombea mnaemtaka halafu watatumia nguvu", amesema Bulaya.

  Pamoja na hayo, Bulaya ameendelea kwa kusema "haki ya Mungu ngojeeni niwaambie hii ni 'game' ni sawa na 'Escape from Sobibor' yaani tunapiga kura, tunalinda kura na lazima mtu atangazwe. Sisi kule kwetu tunasema vita ni vita mura na nipo hapa lazima mtu atangazwe, polisi wananisikia yaani mara mia wao wahamishe kituo chao lakini sisi mtu wetu lazima ashinde. Tumerudi kwa kujipanga".

  Kwa upande mwingine, Bulaya amewataka wananchi wa jimbo hilo kutorudia kosa kwa kumchagua mtu ambae atawarudisha tena kwenye sakata la uchaguzi kama ilivyokuwa sasa.
   
 2. chuma cha mjerumani

  chuma cha mjerumani JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2018
  Joined: Dec 4, 2013
  Messages: 5,048
  Likes Received: 7,129
  Trophy Points: 280
  Mtulia anaacha ubunge alafu anagombania ubunge.

  Kweli hii dunia kuna watu hawana akili.
   
 3. k

  kigogo warioba JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2018
  Joined: Jul 11, 2015
  Messages: 2,287
  Likes Received: 1,902
  Trophy Points: 280
  Kamanda esta amewakumbusha freshi wasifanye makosa ya kuchagua msaliti, atakayekuja kusababisha kurudiwa kura tena! wazee wa manunuzi mpo hapo.?
   
 4. MBIIRWA

  MBIIRWA JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2018
  Joined: May 24, 2013
  Messages: 2,226
  Likes Received: 4,160
  Trophy Points: 280
  PMU wanakusikia mkuu
   
 5. bandamo

  bandamo JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2018
  Joined: Aug 5, 2017
  Messages: 1,925
  Likes Received: 1,254
  Trophy Points: 280
  Sawa safi kabisaa
   
 6. k

  kigogo warioba JF-Expert Member

  #6
  Feb 13, 2018
  Joined: Jul 11, 2015
  Messages: 2,287
  Likes Received: 1,902
  Trophy Points: 280
  Teh, hata mi nawaskia!
   
 7. E

  Earthmover JF-Expert Member

  #7
  Feb 13, 2018
  Joined: Sep 28, 2012
  Messages: 13,784
  Likes Received: 3,885
  Trophy Points: 280
  ......
  .......sisiemu chaliiii mbendembende
   
 8. mng'ato

  mng'ato JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2018
  Joined: Oct 27, 2014
  Messages: 6,640
  Likes Received: 4,216
  Trophy Points: 280
  Mungu amsaidie dada Ester polisi wasianze nae tena.

  Mara ya mwisho polisi walimdaka kule jimboni kwake akawekwa mahabusu mpk akaumwa ikabd akodiwe ndege kumleta dar.Hatariiii
   
Loading...