GE2025 Ester Bulaya aliyekuwa CHADEMA atimkia CCM, achukua fomu ya Ubunge Bunda Mjini

GE2025 Ester Bulaya aliyekuwa CHADEMA atimkia CCM, achukua fomu ya Ubunge Bunda Mjini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Ester Bulaya ametangaza kuwa atachukua fomu Jimbo la Bunda Mjini kupitia CCM.

Bulaya pia alishawahi kuwa Mbunge wa Jimbo hilo kupitia CHADEMA, amesema anajiandaa kuchukua fomu katika zoezi ndani ya CCM lililoanza leo.

1751098511237.png

Aliyekuwa Mbunge wa viti Maalum Esther Bulaya ametangaza kuwa atachukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania Ubunge Jimbo la Bunda Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuelekea uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Bulaya ambaye awali alikuwa mwanachama wa CCM kabla ya kujiunga na CHADEMA na kurejea CCM hivi karibuni, aliingia kwenye mgogoro na CHADEMA yeye pamoja na Wabunge wenzake 18 mara baada ya kuelezwa kuwa taratibu za wao kupata Ubunge wa viti maalum hazikuzingatia Miongozo na kanuni za CHADEMA, suala ambalo liliwafanya kuwa kimya mpaka Bunge lilipohitimishwa, wachache wao wakionekana kuhamia Vyama vingine.

Bulaya ni miongoni mwa wanawake waliowahi kupata Tuzo ya umahiri kwenye masuala ya jinsia, ikilenga kutambua mchango wake katika kupambana kwenye majukwaa ya kisiasa na kumshinda mwanasiasa mkongwe Steven Wasira kwenye Jimbo la Bunda mwaka 2015
 
Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ester Bulaya ametangaza kuwa atachukua fomu Jimbo la Bunda Mjini kupitia CCM.

Bulaya pia alishawahi kuwa Mbunge wa Jimbo hilo kupitia CHADEMA, amesema anajiandaa kuchukua fomu katika zoezi ndani ya CCM lililoanza leo.

Kafail huyu kabisa, wajumbe ndo watamuangusha.
 
Wajumbe watakuwa wapuuzi kama watapitisha hawa covid waliotangaza nia kugombea ubunge kwenye majimbo. Yaani wana ccm mkipambanie chama chenu halafu aje mbwa koko mmpe tu ulaji na kuwaacha wenzenu mtakuwa majuha
Usiteseke mkuu
 
😄😄😂😄😄🤣🤣😁😁🤣😄😄🤣😄
 
Hawa kina esta matiko/bulaya na msigwa ni bora wakapisha wana ccm ambao hawajawahi kuhama chama wagombee kuliko kwenda kuziba nafasi kwa waliokipambania chama
 
Lini amekuwa mwana ccm make tunajua ana kesi mahakamani yeye na wenzake,hivo bdo mahakama haikuwahi kuwavua ubunge wa chadema!maajabu ya name yako Tz
 
Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Ester Bulaya ametangaza kuwa atachukua fomu Jimbo la Bunda Mjini kupitia CCM.

Bulaya pia alishawahi kuwa Mbunge wa Jimbo hilo kupitia CHADEMA, amesema anajiandaa kuchukua fomu katika zoezi ndani ya CCM lililoanza leo.

Hajachoka tu kuliwa na wenzake jamani au anatafuta damu mpya?
 
Back
Top Bottom