ESCROW scandal: Pinda apata watetezi

Huyu jamaa huwa anakurupuka ktk kauli zake bungeni na hizo ndiyo kitanzi chake, mara pesa za ESCROW siyo za umma, mara mihimili isiingiliane yaani ilimradi ripoti isisomwe,huyu ni kama chura tu hasafishiki.
 

mkuu, nakumbuka MALKIA WA NYUKI ndiye aliyeagiza iundwe kamati ya zitto kwa ajili ya kuchunguza skandali hii. hata hivyo, matarajio yake yalikuwa kwamba kamati itamlinda badala yake wamemkaanga sawia!
 
Hata wewe unakuja na hoja marehemu hapo hakuna kupanga ngoja ukweli uchukue mkondo wake....Mzee Pinda yuko vizuri....ni ukweli usiopingika kuwa Pinda ni kati ya PMs waadilifu na waelewa ukimtoa Mzee wetu late Moringe S....tusubili...

huyo pinda wako amelifanyia nini taifa hili tangu awe waziri mkuu? njaa zitakuua!
 
Kweli hata mimi namtetea kwa sababu yeye alishasema ni mtoto wa mkulima lakini mkampa ofisi.
Mlitegemea nini?
 
mi sijatumwa na yeyote lakini kiukweli kutoka moyoni pindahana hatia,kuagiza tu uchunguzi ufanyike ni kutekeleza wajibu wake.
 
Huyu jamaa is so weak bdo tu anataka Kuwa Rais?for that matter bora ya Lowassa kuliko PM ingawa wote wezi

ni bora FISADI Lowasa awe rais wa nchi kuliko Pinda--mtu dhaifu kuliko wote nchi hii.
 
Doesn't help. Huyu aondoke tu. Hii ni laana aliyoipata baada ya kuamrisha raia wapigwe bila kufuata sheria. Sasa anapigwa yeye. Na sisi tunasema apigwe tu maana sasa tumechoka
 
Watu kama Ole Sendeka wanajifanya hawajui kuwajibika maana yake ni nini. Pinda must go.
 

Tupo source mkuu,isije zikawa ni hisia zako na walio katika malango yako
 
kwa jinsi skandali hii ilivyokaa, pinda ajiudhuru ama asijiudhuru, tayari serikali na chama chake imechafuka kwa kiasi cha kutosha.
 
Pinda akitoka leo,basi nitaamini ana ushawishi mkubwa kuliko NGOYAY
 
Hii ingekuwa Rwanda wallahi ujinga huu usingetokea na hawa mafisadi wangeipata fresh...
Tanzania sio nchi ya kuwa masikini kiasi hiki. Tunakosa uongozi bora.
 
Kuna njama kati ya spika makinda na serikali, wanataka kuchelewesha muda, ili kesho wahairishe mjadala! Kama taifa tumekwama, bunge linatumika kutetea mafisadi!
 
Tutaendelea kubadili chupa tu lakini gongo itaendelea kubaki palepale.Dawa ni kuweka mfumo imara wa kitaasisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…