Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,016
- 2,195
Siku haziendi kabisa, kiu yangu nione kile ambacho kitawapata viongozi wapigaji, waliodiriki kuchota zaidi ya shilingi bilioni 300 za Watanzania. Wanaovaa suti, wenye ratiba nzuri ya kula, kulala na kuamka, wamekwenda shule vizuri, ni akina baba wazuri wa familia, ila ni majambazi kuliko watumiao bunduki.
Wasio na huruma na nchi! Wengi wamesomeshwa kwa kodi za walalahoi, wakapewa ‘michongo' ya kwenda kusoma mpaka vyuo vikuu vya nje, wamerudi na kupata kazi, badala ya kutumia elimu yao kizalendo kuwasaidia Watanzania wenzao kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho, wanaamua kuiba.
Ni wasaliti wapanga mipango isiyotekelezeka. Miradi mingi haitekelezwi mpaka fedha za wahisani. Shule zetu hali mbaya, vijijini madarasa ni majanga, kote mpaka mijini hakuna vifaa vya kufundishia, maabara ni tatizo la miaka yote 53 ya uhuru. Hospitali hazina dawa, wagonjwa wanalazwa chini, halafu watu wanachota mabilioni.
Wanahusika uporaji wa mabilioni ya shilingi halafu hawataki wasemwe. Walipoambiwa ukweli, wakachukia, wakaamua kutukana wabunge waibua hoja, mara "tumbili", wakawaita "wabunge washenzi", nao walipojibiwa ni wezi, ‘wakapaniki', wakaropoka "I shall cut your neck."
Ni Escrow, hoja ya kwanza tuliambiwa zaidi ya shilingi bilioni 200 zilitafunwa. Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), inasema zaidi ya shilingi bilioni 300 zimeliwa. Sasa tunaona kila dalili kwamba fedha zote, zaidi ya shilingi bilioni 400 katika akaunti ya Tegeta Escrow zimebebwa kihuni. Huu ni ufisadi mkubwa kuwahi kutokea nchini.
Zipo taarifa kuwa PAP, ile kampuni ya ‘Singasinga' (kama anavyoitwa na David Kafulila), ikiwa na mtaji wake wa shilingi milioni 500, ilijitwalia zaidi ya shilingi bilioni 270. Kwa namna ilivyo, ni mpango wa wavaa suti waliokwenda shule na kubeba dhamana katika nchi, kupora fedha kihuni.
Kabla hata CAG hajakamilisha uchunguzi wake, binafsi nilikuwa naamini kwa asilimia zote kuwa wahuni wameshafanya yao. Shaka ilikuwa kubwa sana kutokana na mazingira halisi ya utoaji wa fedha hizo. PAP shaka! VIP majanga! Haraka ya kulipa fedha za IPTL ilitokea wapi?
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Fredrick Werema, wao wanawatumikia akina nani mpaka waone sawa fedha za Escrow zilipwe haraka wakati Tanesco ya Watanzania ndiyo walalamikaji wa kukamuliwa tozo kubwa kuliko kiwango halisi?
Hata hivyo, sakata zima la Escrow na jinsi ambavyo lilifanyiwa majaribio ya kuzimwa, linanikumbusha mchezo mchafu wa Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na wabunge kadhaa wahuni, walivyozima hoja ya ukiukwaji wa sheria ya manunuzi wakati wa kununua mafuta mazito kwa ajili ya mitambo ya umeme. Nitaeleza!
KWANZA ESCROW NI NINI?
Escrow ni neno lililotoholewa kutoka kwenye kamusi ya kizamani ya Kifaransa. Neno halisi ni "escroue" likiwa na tafsiri yenye kuelekeza upande wa tatu unaoshikilia amana ya watu wanaolumbana mpaka pale ufumbuzi wa kisheria unapopatikana na kukubalika nani apate stahili ipi.
Tafsiri ni ileile; Escrow ni fedha katika akaunti ya tatu kwa niaba ya pande mbili zinazosuguana katika malipo. A anatakiwa kulipwa fedha zake na B, lakini A na B wanaingia kwenye mgogoro, kwa hiyo C anafungua akaunti ya Escrow na fedha zote zinawekwa humo kusubiri mwafaka wa A na B.
Vivyo hivyo, Tanesco ilifugua kesi kulalamika chaji kubwa iliyokuwa inatozwa na IPTL. Kwa kifupi ni kwamba Tanesco ilifungua madai kwamba IPTL ilikuwa inaipiga, kwa kuitoza gharama kubwa kinyume na kiwago halisi kinachotakiwa.
Tanesco mlipaji, IPTL mlipwaji, kukawa kuna utata, mwamala hauwezi kufanyika moja kwa moja, kwa hiyo Benki Kuu iliagizwa kufungua akaunti ya Escrow, ili fedha zote zinazolipwa na Tanesco zihifadhiwe humo mpaka pale kesi ya msingi itakapokamilika na hukumu kutolewa.
Waliokuwa wanalipa fedha ni Tanesco ambazo zinatokana na viwango wanavyotozwa Watanzania. Halafu mtu anathubutu kusema zile fedha hazikuwa za umma, ni za IPTL. Hao IPTL walikuwa wanapata fedha wapi? Na kwa nini zikae Benki Kuu ya Tanzania?
Tanesco waliendelea kulipa mpaka zikafikia zaidi ya shilingi bilioni 400 (dola milioni 270). Fedha zipo Benki Kuu. Watu wakaona zimekaa tu, ikabidi waanze mchakato wa kuzipiga kama vile ilivyotokea katika Fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).
Ikaibuka PAP eti ikauziwa hisa za Kampuni ya Menchmar iliyokuwa inamiliki asilimia 70 za IPTL, na kwa mtaji wake wa shilingi milioni 500, PAP ikatengenezewa mazingira kisha ikapiga bilioni 270 (Singasinga hakula peke yake, atataja aliokula nao). VIP nayo ikajitwalia mabilioni yaliyosalia. Tanzania yenye neema tele!
Niulize tena, Maswi na Werema, waliharakisha malipo ya nini na kwa faida ya nani ikiwa hakukuwa na hukumu inayosema Tanesco imeshindwa kesi? Maana kama ingeshinda, ingebidi fedha zirudi na fidia. Tanesco ilifungua kesi kwa ajili ya kurudisha unafuu wa maisha kwa Watanzania, sasa hao Maswi na Werema ni wana wa taifa gani?
KUSEMA NA KUUMBUANA BUNGENI HAISAIDII
Kusema sana na kuumbuana bungeni haisaidii. Tatizo kubwa la nchi yetu ni mfumo uliokosa maadili ya utumishi. Taifa limejaza viongozi na watendaji wabinafsi ambao kwao maisha yao binafsi yana maana kubwa kuliko maendeleo ya nchi.
Janga kubwa linaanzia Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (PCCB). Hii ni taasisi nyeti sana lakini sheria za nchi na mtindo wake wa kufanya kazi, haupambani na watoa rushwa, bali unasaidia maofisa wa Takukuru nao kula kwa urefu wa kamba zao.
Takukuru inavyofanya kazi hivi sasa, inawalinda watoa rushwa na kuwakamata wasiowapa rushwa. Kwa sura hiyo, unadhani kigogo gani atakamatwa? Kigogo gani mla rushwa atakosa uwezo wa kuhonga maofisa wa Takukuru wanapomzonga kumkamata?
Takukuru ipo mitaani ikishughulikia rushwa ndogondogo, haijikiti kwenye mitandao ya taasisi binafsi zinazofanya kazi na serikali ili kushughulikia rushwa kubwakubwa. Maana huko ndiko kwenye upigwaji wa mabilioni mamia kwa mamia.
Kati ya taasisi binafsi na serikali, ndipo kwenye biashara ya kuuziana tenda, malipo kuongezwa cha juu ili kiwe kinanufaisha watendaji wa serikali walioidhinisha biashara kufanyika kati ya serikali na kampuni fulani binafsi. Tuachane na rushwa za trafiki, shilingi 10,000, Takukuru ijikite kwenye rushwa kubwa ili kuokoa nchi.
Natamani kuona Escrow inakuwa kashfa ya mwisho ya wizi wa fedha za Watanzania. Nikitumai ya kwamba baada ya skendo hii, tutaona muundo mpya wa njia za kudhibiti rushwa nchini na wala rushwa pamoja na wapokeaji, wanapewa kibano cha maana ili wakome pia iwe fundisho kwa wapigaji wengine.
Escrow isiishie kama Richmond. Serikali ilipata hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 200 kwa kitendo chake cha kuipa tenda kimagumashi Kampuni ya Richmond. Mpaka leo, tangu mwaka 2008, ukiachana na adhabu ya kuumbuana bungeni na kukoseshana tonge (kulazimishana kujiuzulu), hakuna hatua kali zilizochukuliwa.
Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu (AG), Johnson Mwanyika yupo zake anaendelea na maisha, licha ya kuhusika na hasara hiyo. Kwa nafasi yake, aliwajibika kuishauri serikali isiingie mkataba na Richmond lakini hakufanya hivyo. Angepelekwa kortini, tungejua kama alihongwa au vipi.
Aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, mawaziri wa Nishati na Madini waliopokezana ofisi, Nazir Karamagi na Ibrahim Msahaba (alikuwa Wizara ya Afrika Mashariki wakati anaumbuliwa), baada ya kudhalilishwa bungeni, hakuna hatua yoyote iliyofuata.
Huu ni mwaka wa sita na miezi tisa (tangu Februari 2008), Richmond ilinyamazishwa kwa staili ya kufunika kombe mwanaharamu apite. EPA tunakumbuka ilivyokuwa moto, wezi waliambiwa warudishe fedha zaidi ya shilingi bilioni 130 walizoiba kisha wakasamehewa, walioshindwa kulipa (wale dagaa), walitolewa kafara.
Ni zaidi ya aibu kama yaleyale ya Richmond na EPA, yatajirudia kwenye Escrow. Tunahitaji kuona mabadiliko ya hatua za kinidhamu kwa watendaji waovu. Familia zao zitaumia ila si vibaya zikionja matokeo ya kuwa na akina baba wasio na maadili, wenye hulka ya kuifilisi nchi.
KILIO CHANGU NA WABUNGE WAHUNI
Wakati wa Bunge la Bajeti mwaka huu ndipo hoja ya Escrow ilipoibuliwa. Wabunge walioanzisha hoja, Kafulila, Christopher Ole Sendeka na Zitto Kabwe (aliyechangia kwa maandishi), walisemwa kuwa wanatumika na kwamba wamehongwa ili kudhoofisha jitihada njema zinazofanywa na Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo pamoja na Maswi.
Wapo wabunge walisimama na kuwasuta wenzao waziwazi. Hawakutaka kabisa Muhongo na Maswi wasemwe. Eti wabunge hao wanatumiwa na wakili tajiri, Nimrod Mkono pamoja na mfanyabiashara, Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi.
Nilimshuhudia Muhongo akiwatusi Ole Sendeka (eti hakuwa na akili darasani), kisha akamwambia John Mnyika ni sifuri. Kundi kubwa la wabunge, wakiwemo wa upinzani, walishangilia matusi ambayo Muhongo aliyatoa.
Kwenye korido, baadhi ya wabunge walikuwa imara kupakaza; "wale jamaa wamelipwa kukwamisha bajeti ya Nishati na Madini lazima tuwashughulikie." Huu ndiyo uhuni wa baadhi ya wabunge wetu. Ni rahisi kurubuniwa kwa uongo kisha kuwasaliti wenzao wanaoanzisha hoja zenye maslahi kwa taifa.
Kuna katabia haka bungeni; wabunge wakiambiwa wenzao wamekula mlungula, wanakuwa na hasira kali kuwashughulikia bila hata hoja wala ushahidi. Si kwamba kwa vile hawapendi rushwa, bali kwa kijicho "kwa nini wale peke yao?"
Mwaka 2012, mtikisiko mkubwa ulitokea pale Zitto Kabwe alipoomba idhini ya Spika wa Bunge, Anne Makinda ili kamati yake ya Hesabu za Mashirika ya Umaa (siku hizi haipo) ichunguze mgogoro wa Tanesco, kati ya bodi na mkurugenzi aliyefukuzwa, William Mhando, kwa vile ilitajwa skendo ya ukiukwaji wa sheria ya manunuzi wakati wa kununua mafuta mazito (ghafi).
Zitto akaunganishwa na wabunge wengine, Sara Msafiri, Christopher Ole Sendeka, Munde Tambwe na wengine wote waliokuwa wanaunda Kamati ya Bunge Nishati na Madini, kwamba walihongwa kila mmoja shilingi milioni 10 kukwamisha bajeti.
Bungeni palinuka, Zitto (kutokana na umaarufu wake), akaona yeye ndiye mlengwa hasa. Dodoma hapakukalika na Dar hapakumfaa. Siku bajeti inapitishwa, wabunge tajwa wote hao hawakuwepo bungeni kwa aibu. Walivaa sura mbaya, wenzao waliwasakama.
Makinda kwa hatua ya haraka, aliivunja Kamati ya Nishati na Madini, vilevile akaunda kamati teule iliyoongozwa na Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi ambayo ilibaini kuwa ile kashfa kwa akina Zitto na wenzake, ilikuwa janja ya nyani ya Maswi na Muhongo kuficha madudu yao.
Kamati ilibaini kuwa bodi ya Tanesco ilikiuka sheria ya manunuzi kwa kumpa tenda mzabuni aliyeshindwa. Upo ufisadi na mambo ya kimapenzi yaliyobainishwa lakini acha tu. Spika akasema, sasa natoa adhabu kali, watu tukatega sikio, kumbe adhabu yenyewe aliyosema ni kali, iliishia kuwapa onyo Maswi na Muhongo kwa kulidanganya bunge.
Onyo halikuwa na mashiko kama hoja stahili ingepewa nafasi yake. Hata hivyo, ilifunikwa kwa staili ya kuwashambulia wabunge waanzisha hoja. Na Escrow ilianza hivyohivyo, akina Maswi walidhani ya 2012 yangejirudia tena, imeshindikana.
Wabunge wabebe heshima yao, waache kutumika na kusimamia hoja ambazo hawana ukweli nazo. Sijui Kangi Lugora anasimamia wapi leo? Maana aliwatetea Maswi na Muhongo mpaka mwisho. Waziri Mkuu, Mizenge Pinda, naye yupo mguu ndani mguu nje kwa kitendo chake cha kutamka tu kuwa fedha za Escrow si mali ya serikali.
By Luqman Maloto