Shy land
JF-Expert Member
- Jul 28, 2013
- 6,245
- 2,848
NAIBU Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema Januari mwaka huu kabla ya kuanza kwa vikao vya kamati za Bunge, wajumbe wa kamati tatu watakuwa na kazi ya kuchagua wenyeviti wapya ili kuziba nafasi za wale ambao wanatuhumiwa kwenye sakata la Escrow.
Kauli hiyo inakuja siku chache tu, baada ya Rais Jakaya Kikwete kuliambia taifa kuwa, wenyeviti wa kamati wanaotuhumiwa kwenye sakata la Escrow, hao watawajibishwa na Bunge na si kazi yake yeye.
Moja ya maazimio ya Bunge ni kwamba, wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge ambao wanahusishwa kwenye sakata hilo ni vema wakawajibishwa kwa kuondolewa kwenye nafasi za kuwa wenyeviti wa Kamati za Bunge.
Akizungumza na gazeti hili jana, Naibu Spika wa Bunge, alisema vikao vya Bunge vinatarajia kuanza Januari 27, mwakani na moja ya majukumu ya kamati ambazo wenyeviti wake wanatuhumiwa watakuwa na kazi ya kufanya uchaguzi wa wenyeviti wapya.
Wenyeviti wanaotuhumiwa kwenye sakata hilo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Andrew Chenge, Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Victor Mwambalaswa na Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria, William Ngeleja.
Akifafanua zaidi Ndugai wakati akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu akiwa jimboni kwake Kongwa mkoani Dodoma, alisema kamati husika zinawajibu wa kufanya uchaguzi wa wenyeviti na kazi hiyo itafanyika siku ya kwanza wakati wa vikao vya kamati za Bunge ambavyo vitaanza wiki mbili, kabla ya kuanza kwa Bunge.
Kwa mujibu wa Ndugai, vikao hivyo vya kamati vitafanyika katika Ofisi ndogo za Bunge zilizopo jijini Dar es Salaam.
Ndugai alisema baada ya kamati hizo kufanya uchaguzi, zitapeleka majina ya wenyeviti wapya kwenye Ofisi ya Bunge na kisha wataendelea na vikao vya kamati kwa mujibu wa kanuni.
"Suala la kupatikana kwa wenyeviti wa Kamati hizo tatu ambazo wenyeviti wao wanahusishwa na sakata la Escrow, lipo katika mamlaka ya kamati husika. Hivyo, taratibu za Bunge ni kwamba, lazima wafanye uchaguzi kwanza, ndiyo waendelee na vikao," alisema.
Kwa mujibu wa Ndugai alisema kimsingi wenyeviti hao walikosa uhalali wa kuwa, viongozi wa kamati hizo tangu siku ambayo Bunge lilipitisha mazimio yake, kilichobakia ni uchaguzi wa kuhakikisha kuwa, wanapatikana wapya.
"Bunge linavyopitisha maazimio kuhusu wao wenyewe ni wajibu wao kuhakikisha utekelezaji wake unafanyika kwa maslahi ya Bunge na taifa," alisisitiza.
Aidha, Naibu Spika Ndugai alisema kuhusu utekelezwaji wa maazimio ya Bunge kwa watu wengine ambao Bunge haliwajibiki nao katika kuwawajibisha, alisema taarifa yake wataipata Bunge litakapoanza, ambapo Spika wa Bunge hilo atatoa taarifa za utekelezaji wake.
Alisisitiza, kabla ya kuanza kwa shughuli nyingine za vikao vya Bunge, wabunge watapewa taarifa ya Serikali ilivyoshughulikia maazimio ya Bunge.
Ndugai aliwataka wananchi kuwaamini wabunge wao kwa kuwa, watahakikisha maazimio yote yaliyotolewa na Bunge yanatekelezwa kwa misingi inayofaa kwa maslahi ya nchi na wananchi wake.
Wakati huo huo, Ndugai aliwashukuru wananchi wa jimbo lake kwa kuwachagua wenyeviti wa vijiji na vitongoji wa CCM kwa asilimia 99 na kuwaahidi kuwa, watajitahidi kufanya nao kazi kwa moyo wote.
Chanzo:Jamboleo