Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,655
- 729,730
Je, hii yaweza kuwa mwanzo wa kuanguka kwa mbuyu? Mfupa uliowashinda wengi?
Kampuni ya uwakili ya Mkono & advocates, inayomilikiwa na mzee mmoja anayeheshimika na tajiri sana huku akiwa mahiri kwenye sheria imeingia matatani na mamlaka ya mapato Tanzania(TRA)ikisemekana kudaiwa zaidi ya bilioni moja fedha za ki Tanzania kama kodi ya mapato.
Hatua iliyofikia ya kwenda kupiga kufuli na kuweka notice ya mnada pengine ni hatua ya mwisho baada ya juhudi nyingine zote kushindikana..!
Hii ni mbaya mno kwa legacy ya Mzee Nimrod, status yake na taaluma yake ya uwakili kitaifa na kimataifa, hawa ndio walikuwa untouchables wa chama waliokisaidia sana kwenye upande wa cash.
Lakini kiserikali ndio kampuni ya uwakili iliyolalamikiwa sana kwenye sakata zima la Escrow kwamba Mkono & advocates iliishauri vibaya serikali huku ikiwa imelipwa mabilioni ya pesa na mwisho ukawa mbaya....limekuwa ni suala linaloibuka na kufa kila wakati.
Kwa hatua hii ya sasa;
Je ndio mwanzo wa sakata la escrow kuanza kushunghulikiwa?
Je ndio mwanzo wa mwisho wa Mkono & advocates?
Au je ndio mwanzo wa tamthilia nyingine tamu zinazoanza kwa mbwembwe nyingi na kuishia kusikojulikana?
Ni suala la muda tuu..