Errol Spence vs Danny Garcia wanazichapa muda huu

screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
10,791
15,693
Wapenzi wa ndondi, leo ni siku nyingine dunia inashuhudia pambano jingine kali la kufungia mwaka kati ya hawa mafundi wawili wa uzito wa 'welterweight'; Errol Spence ambaye ni bingwa, na Danny Garcia ambaye aliwahi kuwa bingwa wa dunia ambapo siku ya leo Errol Spence ana kazi ya kutetea mkanda wake wa WBC.

Japokuwa wengi wanampa zaidi nafasi Spence kutetea ubingwa wake ila ikumbukwe kwamba mwishoni mwa mwaka jana alipata ajali mbaya ya gari na kujeruhiwa vibaya maeneo ya kichwa hivyo kukaa muda mrefu nje ya ulingo, wasiwasi wangu ni je leo hii tutampata yule Spence tuliyemzoea?

Je haitakuwa advantage kwa Garcia ukizingatia ni moja ya hardest puncher kwenye hiyo division?

Jibu tutalipata dakika kadhaa zijazo.

pbconfox_20201206_070156_0.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom