Kwa muda mrefu sasa hii kampuni inayojiita Erolink recruitment agency imekuwa ikiuza kazi kwa bei Nafuu baada ya kuzinunua kwa bei ghali. Inanunua kazi ya Vodacom customer care kwa tsh 861,000/= inaiuza kwa tsh 246,000/=. Kutokana na ugumu wa kazi basi watanzania watoto wa masikini wananunua kazi hizo kwa bei ya kutupa ilihali ndani ya kazi hizo kuna mateso makali na hatari za kupata tatizo la kiafya kutokana na mionzi. Watu wamekuwa wakiteswa sana lakini walioshindwa kuvumilia mateso na vijembe waliondoka wenyewe. Rais kikwete alijitahidi kulitatua lakini lilishindikana. Mimi binafsi niliondoka baada ya juhudi za jk kugonga mwamba. Ila zimekuwa nikifwatilia kwa karibu kama kuna mwokozi anayeweza kulivalia njuga maana pale niliacha kama milioni mbili hivi kwa kuwa walikuwa wananilipa 246,000 badala ya 400,000 kama Sheria inavyoagiza. Bado overtime ambazo kisheria zina malipo yake au kama mwajiri hataki basi asifanyishe kazi wafanyakazi kwa siku hiyo.
Nimefarijika baada ya kuona JPM chini ya waziri wake wa kazi ameamua Erolink sasa baaasi. Binafsi roho yangu imejisikia bwerere. Pamoja na hayo ameagizi mishahara elekezi ilipwe na stahiki za wafanyakazi pia. Kilichonigusa mimi direct ni malimbikizo ya mishahara iliyo languliwa kipindi cha nyuma ambapo hata mimi nadai.
Kwa kiongozi yoyote wa erolink anayesoma sms hii akamweleze afisa mwajiri alipe malimbikizo kwa wafanyakazi wote hata sisi tulioondoka baada ya kushinda kuvumilia mambo yenu. Salary slip binafsi ninazo na endapo sitalipwa mtafanya yaibuke mengine makubwa zaidi.
Mungu awape hekima katika kipindi hiki ambapo kupitia mtumishi wake Mheshimiwa John Pombe Magufuli tunapata kupona. Hata ninapokuwa na njaa nikimtazama nahisi nimeshiba. Siku aliyotoa mshahara wake pale muhimbili kwa ajili ya yule mgonjwa nilijikuta nalia machozi kwani sinawahi ona wala kutaraji kuona tukio kama lile. Mungu yuko pamoja na wewe raisi wetu na atakuwekea malaika wake pande zote ili wakulinde usiku na mchana.