Umewahi kusikia kuhusu ergonomic keyboards? Ni computer keyboards ambazo, funguo zake zimepangwa kwenye muundo tofauti kitaalam kulingana na mwelekeo wa mwili wa mwanadamu. Kwamba computer keyboards zile za kawaida funguo zake zinakua zimepangwa tu kwenye safu zilizo nyooka, na kumfanya anayechapisha kubana viwiko kwenye ubavu. Lakini hizi zinampa mtu nafasi ya kujiachia kidogo kama kujinafasi.
Niliposoma article fulani kuhusu keyboard hizi nikapuuzia, nikajua zitakua zinapatikana mbele.
Juzi katika pitapita yangu Kariakoo, kwenye duka la vifaa used vya computer, nikaona keyboard hizi. Nikauliza nikatajiwa 10,000. Nikaombaomba hadi 5,000 nikachukua. Ni moja yenye muundo wa "V"
Hasara ya keyboard ya namna hii ni kwamba inahitaji kamuda kidogo kuzoea, pia inawafaa zaidi wale wanaochapisha bila kuangalia keyboard. Wachunguliaji wasinunue maana italeta ugumu zaidi katika kutafuta herufi. Wakati fulani nilijizoesha kuchapisha herufi "B" kwa mkono wa kulia, baadae nikagundua ni makosa, nikaanza kuirudisha kwenye mkono wa kushoto, sasa naona faida yake. Maana hapa B imewekwa kushoto.
Hapa nimeshajizoesha kidogo na imeanza kunoga. Wakati mwingine kujaribu mambo tofauti, inapendeza zaidi.