Erasto Zambi, umesikia maajabu ya CCM Mbozi?

Erasto Zambi, umesikia maajabu ya CCM Mbozi?

Ringo Edmund

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2010
Posts
4,879
Reaction score
1,134
Nimeiskia kutoka taarifa ya habari TBC kutoka Mbozi eti kufaulu kuingia sekondari kwa wanafunzi wasiojua kusoma wala kuandika ni kutokana na kuwa na msongamano wa wanafunzi madarasani na kuwa na waalimu wachache.

Hili kwangu ni ajabu la dunia kwa sababu CCM sasa imeamua kujitoa akili,haiingii akilini msongamano wa wanafunzi na uchache wa waalimu inahusiana vipi na kufaulu.

Namwomba mbunge Erasto Zambi wa Mbozi aje hapa atuelezee mafanikio ya ilani ya CCM Mbozi na hili ajabu la dunia huko.

Hii ni sehemu ndogo tu ya Tanzania.je hali ikoje nchi nzima.
 
Sasa hili ni ajabu la dunia kivipi? kwamba hizo sio sababu za kufeli kwa wanafunzi au nini?
 
hao waliofaulu katika shule hizo hizo walifauluje watu wa ccm siku hizi wanazidiwa akili hata na kinyesi
 
Maajbu ya duni ni yale tuliyoletewa na Waziri wetu wa Elimu,ambaye ameleta mitaala isiyokidhi na ya udanganyifu.
 
Hata yule dogo masalia anaweza kuja kufafanua. Whoever is not with us, is with them.
 
Ebwana eeeh, unashtua mtumishi, Erasto Zambi ni marehemu, tulimhifadhi mwaka jana.
 
Mkuu wa wilaya Mbozi; watoto 70% waliyochaguliwa kuingia kidato cha kwanza na watoto 28,000 waliyopo sekondari wilaya hiyo hawajui kusoma na kuandika:

Hii ni taarifa ya habari ya saa 4 asubuhi leo -TBC, hili tatizo liko Tanzania nzima kila wilaya ina wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wasiyojua kusoma na kuandika! hii serikali hafai hafai na haistahili tena kuongoza nchi yetu, huu ni mkakati mahsusi wa kufanya watotot wa maskini wasipate elimu kwani wakipata elimu watatambua haki zao.......kwa namna hii hakuna taifa hapa huwezi kuwa na taifa ambalo halina elimu ukasema una taifa, na hili limejidhihirisha wazi baada ya Mh. Mbatia kuleta hoja ya kuundwa tume ya kuangalia udhaifu wa elimu tanzania ikakataliwa na spika wa bunge pamoja na wabunge wa maccm........kukataa jambo ambalo lina maslahi ya taifa ni kwamba kuna agenda ya siri imefichwa na wanaokataa, Mh. lowasa alisema hoja ya mbatia ni ya msingi na akaenda mbali zaid akaongeza kanunu za bunge zinaweza kuvunjwa ili kuruhusu hoja au jambo muhimu lenye maslahi ya taifa yafanyike, hatuwezi kuendelea kunyayaswa kwa makusudi na hii serikali tena, sisi wananchi tutatumia maombi, nguvu na akili zetu zote kuondoa hii serikali madarakani hata ikibidi baadhi yetu kupoteza uhai kwa ajili ya ukombozi wa wengi tutafanya hivyo. ee Mwenyezi Mungu tusaidie tulikomboe taifa hili. AMEN
 
Kufeli ni kufeli, hakuna haja ya kuhalalisha, eti kwa sababu hii au ile. Je mwanafunzu wa urubani akishindwa mitihani kwa sababu ya uhaba wa vifaa vya kufundishia utamruhusu kurusha ndege? Tuache bla bla.
 
wanawapasisha ili kumridhisha yule jamaa wa magogoni.
 
Sasa hili ni ajabu la dunia kivipi? kwamba hizo sio sababu za kufeli kwa wanafunzi au nini?

wewe akili yako inakaa katika kiungo gani cha mwili.

wanadai kuwa wanafunzi wa sekondari hawajui kuandika na kusoma kwa sababu ya msongamano darasani.
kwa akili yako kama kuna msongamano ni lazima wafaulu,na je huo msongamano sekondari umepunguza akili za wanafunzi.
na kama ni msongamano wa shule za msingi unahusika vipi na kufaulu.
 
Nadhani ulitaka kusema Godfrey Zambi, sio Erasto Zambi.

asanteni wadau kwa kunielewa,unajua hawa magamba wanatuchanganya kiasi kwamba tunachanganyikiwa.

nilikuwa na maana ya godfrey.

mungu amlaze mahala pema peponi erasto.
 
Huyu Godfrey Zambi alianza kuchakachua TAZARA,Mamlaka ya hali ya hewa na sasa ameamua kumaliza nyumabani kwake mbozi...yaani mbozi sasa hatutaki magamba maana hawa ni majambazi tu...kuanzia mwenyekiti na vijinyekiti vyote.
 
Ebwana eeeh, unashtua mtumishi, Erasto Zambi ni marehemu, tulimhifadhi mwaka jana.
Erasto Zambi mwalimu wangu siku nyingi, amefariki?
Alikuwa kikaa sehemu za Ubungo nafikiri Extnal au Mabibo, ndiye huyo!
Hebu nipe details mkuu!
 
Erato Zambia ni ,walimu wangu wa geography mbeya day. Huyo ni Godfrey zambi
 
Back
Top Bottom