Equatorial Guinea mwenyeji wa AFCON 2015

Equatorial Guinea mwenyeji wa AFCON 2015

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,158
Reaction score
64,499
EQUATORIAL GUINEA MWENYEJI WA ‪#‎AFCON2015‬

Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF limeitangaza Equatorial Guinea kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Mataifa Afrika baada ya Morocco kukataa kuandaa michuano hiyo kwa hofu ya kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola.

CAF imeiondoa kabisa Morocco katika timu zitakazoshiriki, na sasa nafasi yake inakwenda kwa Equatorial Guinea ambayo mwaka 2012 iliandaa mashindano hayo kwa kushirikiana na Gabon.

Chanzo:EATV
 
Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015 sasa itafanyika nchini Equatorial Guinea baada ya kutokea sintofahamu ya nchi gani itakuwa mwenyeji kufuatia kujitoa kwa dakika za mwisho kwa Moroko kutokana hofu ya Ebola.

Mazungumzo kati ya Rais wa CAF, Issa HAyatou na rais wa Equatorial Guinea, Theodoro Nguema yaliyofanyika mapema asubuhi ya leo mjini Malabo yalipelekea makubaliano ya nchi hiyo kuwa mwenyeji.

Gharama za maisha na upungufu wa vyumba vya hoteli ilikuwa changamoto wakati taifa hilo lilipoandaa makala ya michuano hiyo mwaka 2012 kwa kushirikiana na Gabon.

Moroko ambayo ilikua imeshajihakikishia ushiriki wa moja kwa moja sasa imeondolewa mashindanoni na huenda adhabu zaidi ikafuata kufuatia kitendo hicho cha kuukacha wenyeji katika hatua za mwisho.

====================
====================

It is now official that Equatorial Guinea, who co-hosted AFCON 2012, will stage the 2015 tournament.

French newspaper L'Equipe, reported on Friday that Equatorial Guinea will host the 2015 AFCON from January 17 to February 8 in place of Morocco, who were disqualified.

ConfirmationThe confirmation has been given by sources in Equatorial Guinea with the official announcement to come later on Friday.

CAF President Issa Hayatou reached Malabo early on Friday to handle talks with Equatorial Guinea Head of State Teodoro Obiang Nguema.

An Equatorial Guinea team lavishly garnished with foreigners, reached the last eight when they co-hosted the competition along with Gabon. They were trounced 3-0 by Cote d'Ivoire.

ChallengesHigh costs of living and shortage of hotel rooms were the major challenges when the oil-rich island first hosted the competition two years and it is left to be seen how they will now cope with 16 teams and not eight teams like in 2012.

Original AFCON 2015 hosts Morocco had insisted the competition be postponed after they expressed fears over the Ebola Virus Disease, which has killed over 5,000 people in West Africa thus far.

The North Africans have since been disqualified from next year's tourney and more sanctions are expected to be imposed on them.

Futaa

 
Safi sana, na sasa wamoroko waende wakashiriki Euro kama wanavyoota mchana mchana.
 
Afadhali, nilidhani ndio yanakufa taratibu kama cecafa
 
Sasa kwanini wameondolewa wakati wana sababu inayoeleweka kabisa? Sijaelewa
 
Safi sana, na sasa wamoroko waende wakashiriki Euro kama wanavyoota mchana mchana.
Kuna siku hawa wamoroko wataomba kujiunga na umoja wa kiuchumi wa nchi za ulaya.....ndoto mbaya kweli kweli.....
 
Kuna siku hawa wamoroko wataomba kujiunga na umoja wa kiuchumi wa nchi za ulaya.....ndoto mbaya kweli kweli.....

Mbona hizo ndio ndoto zao, na mfalme wao anavyojipendekeza kwa nchi flani flani, halafu wenzie walivyo wabaguzi anaonekana kichekesho tu. Kuna wamoroko wamejaa hapa nilipo hata siku moja hawajihesabu kama ni waafrika, labda kwenye hilo soka tu.
 
Jamani mi hapa nilipo naagalia African Cup Of Nation, kumbe hata Malawi imo inacheza humu! Sasa how come Taifa Stars siioni? Au haturuhusiwi kucheza?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom