ochu hulker
Member
- Apr 16, 2013
- 18
- 5
Ndugu zanguni siku hizi katika mtandao wa Facebook kuna utapeli mtindo wanaotumia ni huu na mara nyingi hawa ni watu kutoka ktika nchi za magharibi mtindo wenyewe ni huu. Anakutumia msg inbox kwamba amependa profile yako na angependa muendelee kuwasiliana kwa kutumia email na anakutumia email yake na wewe anaomba umtumie email yako na ukishamtumia email yako anakutumia historia ya uongo kuhusu maisha yake kwamba "yeye ni msichana anayeishi katika kambi ya wakimbizi kama mkimbizi wa kivita lakini Baba yake ni meneja katika kampuni moja kubwa na ana pesa sana na anataka kumtumia pesa lakini yeye hana akaunti ya benki kwa hiyo anakuomba wewe umtumie namba ya akaunti ya benki ili baba yake atume perj kupiti akaunti yako.Na nasikia ukishamtumia hiyo akaunti anakuibia pesa katika akaunti yako.Sifa za kujua msg yao n kama zifuatazo.Hukutumia msg bila bila kukuomba urafiki,Huweka profile picha ya mwanamke mzuri na huwa ni moja tu, Huwaga na marafiki wachache sana na Pia hutumia kiingereza chepesi sana ambacho mtu mwenye kichwa kibovu uelewa kwa uwepesi na mwisho nchi wanazoandika wanaishi ni za kutoka afrika magharibi katika miji mikuu.NINA MSG KAMA HIZO KAMA 10 MWISHO LEO NIMETUMIWA.